Nico Zengekala: Mwanamuziki kipofu aliyetikisa Tanzania

Nico Zengekala: Mwanamuziki kipofu aliyetikisa Tanzania

Huyu jamaa alikuwa na sauti tamu sana. Kila nikisikiliza nyimbo zake huwa namkumbuka marehemu baba.
Kumbukumbu inanirudisha mwaka 1995 wakati ambapo baba alininunulia suti ya kaptula, wakati ananikabidhi kuna wimbo wa hasira hasara ambao kuna sauti yake.
Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho kupokea zawadi kwa baba kwani alifariki miezi michache baadae.
Pole saana mzee.
 
Sikuwahi kujia kama jamaa alikuwa kipofu, sio wa enzi zangu, lakini nyimbo zake nilizipenda kupitia mzazi wangu alikuwa akizisikiliza saana, santuri zilikuwepo za kutosha maskani za mgoma za kale..

Nikaleta utoto teknolojia ya santuri ilivyoanza kuisha nikawa nazibeba naenda kuchezea baharini. [emoji23]
 
ILIPOSIKIKA sauti yake kila mpenzi wa muziki anayefuatilia bendi za hapa nyumbani alihisi kuna kitu kipya kimeingia katika tasnia ya
muziki wa dansi. Hiyo ilikuwa mwaka 1982 alipoingia kwa mara ya kwanza nchini mwimbaji hatari kutoka mkoa wa Pwani nchini Kenya Nico Zengekala akiwa ni mwimbaji tumaini wa bendi ya Les Quban.

Bendi hiyo ilianzishwa nchini Kenya lakini ilikuwa na wanamuziki kutoka Tanzania ambapo awali ilikuwa pamoja na mwimbaji maarufu Juma Kilaza aliyetamba sana mkoani Morogoro kabla ya kufanyika mapinduzi ya uongozi yaliyomnyang'anya Kilaza uongozi na pia kumtimua kwenye bendi na jahazi hilo kushikwa na mpuliza saxophone marehemu Comson Mkomwa.

Walipoingia katika kumbi za burudani za jijini Dar bendi hiyo ikiwa pia na mpiga gitaa la solo Mohamed Tungwa, wapuliza ala za
upepo kama Said Makelele, Jumanne Mwamzungu, akina Majuto Mbungani na Shaibu Monduli bendi hiyo iliweza kuingiza
ushindani kwa bendi kongwe kama Juwata wakati huo, Mlimani Park na hata bendi zilizokuwa na asili ya wanamuziki kutoka nchini Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kama vile Orchestra Safari Sound, Marquiz du Zaire na Matimila.

Nyimbo zilizozipeleka puta bendi nyingine pamoja na mashabiki kwa ujumla ni pamoja na Shemango, Kambarage Nyerere, Jack na
nyingine kadhaa. Uimbaji wa Zengekala ulianza kupata sifa ndani na nje ya bendi hiyo na watabiri wa masuala ya muziki wakati huo walithubutu hata kueleza wazi kwamba mwanamuziki huyo kamwe asingedumu katika bendi hiyo.

Hatimaye, mawazo hayo yakawa kweli kwani Zengekala mwenyewe alimueleza mwimbaji mwenzake wa karibu wakati huo, Shaibu Monduli kwamba yeye alitamani sana kuiimbia bendi ya Juwata Jazz inayotumia mtindo wa Msondo Ngoma. Akamsisitizia kwamba dhamira hiyo alikuwa nayo tangu alipokuwa nchini kwao Kenya ambako alizisikia nyimbo za bendi hiyo na pia akatamani siku moja kuimba na akina Hassan Bitchuka, Shaaban Dede, Joseph Lusungu na waimbaji wengine wakongwe.

Hivyo alitaka hatua yake ya kufika nchini Tanzania iende na dhamira yake ya kujiunga na bendi hiyo endapo atakubaliwa. Vurumai kubwa ilijitokeza miongoni mwa viongozi wa bendi ya Les Quban waliokuwa wakitumia mtindo wa Vinavina na wale wa Juwata baada ya kujua nyota ile ya jaha inaangazia kwenye bendi yao.

Hatimaye Zengekala akatua Msondo na kuweka mapenzi makubwa ya urafiki na mwimbaji mwingine chipukizi aliyemkuta
Msondo marehemu Tino Masinge. Alipojiunga tayari bendi hiyo ilishawakamata waimbaji mbalimbali akiwemo TX Moshi William kutoka bendi ya Polisi Jazz.

Wimbo wake wa kwanza na bendi ya Juwata ulikuwa ni Solemba ambao alipenda apigiwe solo na gwiji la chombo hicho Dk
Saidi Mabela na yeye akashirikiana kuimba akiwa na Suleyman Mbwembwe na Tx Moshi William. Enzi hizo tayari Hassan Bitchuka alishaihama Msondo na kujiunga na Mlimani Park lakini ikatokea siku moja bendi hiyo kufanya shoo katika ukumbi mmoja pale DDC Magomeni Kondoa.

Kwa kuwa siku hiyo Bitchuka naye alikuwemo ukumbini na Msondo ndiyo iliyopata nafasi ya kufungua pazia la burudani ile basi umati wa watu uliojaa ulidhani Bicthuka ameamua kwenda kuipiga tafu Sikinde kumbe ilikuwa ni sauti ya Nico Zengekala aliyekuwa akiimba wimbo uitwao Sogea karibu.
Solemba ni nyimbo nzuri nikiwa mdogo hadi sasa mtu mzima huwa naisikiliza ni nyimbo nzuri sana. Aendelee kupumzika kwa amani mtunzi nico zengekala!!!
 
Bujibuji

Duu hii kitu ya 2011, wengi watakujibu wako mwaka watatu au pili chuo kikuu ,wakija hapa wakisona mada zako wanachukulia poa poa ,kumbe ungamua kuwaacha kiuononi kwako wasingeona nyuzi zako
 
[Mwanzo] Rudi Table
Solemba - JUWATA JAZZ(Nico Zengekala)]
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
Nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na
dharau tele
Ungenieleza ukweli solemba,
Kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya
kweli.
(Chorus)
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba sababu ya
kukungoja wewe
Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
Nimeshituka Solemba ,
Nimeshituka Solemba
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Sikutaki tenaaa, sina haja nawe,nimeshapata
mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha
kama mimi
Huna huruma Solemba.......Aloi I love you
baby
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
Rudi mwanzo
[TUMA - Nico Zengekala]
Nilisimama kwenye kona, ya uhuru na
msimbazi,
Natizama wanaopita , wanaorudi mamaaaa,
Huenda nikaiona sura yake tuma.
Nasimama nikiwaza, ahadi yetu tuliopanga,
Tukutane Darisalama, Tuma mama,
Nia na madhumuni wazazi watuone.
Nilishikwa na mnutsuko shoga yake
aliniponiejia na kunieleza
Tuma ee tuma ee keshaolewa
Nilishikwa na mshituko mapigo ya moyo
enda mbio
Sikutegemea Tuma, kama angevunja ahadi
yetu ama kweli penye uzia hupenyeza rupia
CHORUS:
Usinione nimekonda ewe Tuma, hakuna
lingine mama
Ila ni wewe Tuma.
(Usiku wote nalala nikikuwaza nakuita jina
lako oh oh Tuma)
Repeat: Usinione nimekonda ewe Tuma.
Rudi mwanzo

Duuh Kumbe alikuwa ni Mlemavu wa Macho? Sasa hii TUMA mbona kama aliimba TX Moshi WIlliam? Nimesimama njia Panda ya Uhuru na Msimbazi.
 
Mola amuweke pema. Alikuwa machine ya kuimba yenye thamani kubwa sana. Ile sauti kunamo solemba haina mfano ina mtetemo wa aina yake. Sifa kwa Muumba.
 
Kifo kifo

Kifo ni wa Baba Romee,

Kifo ni wa Lushiku,

Kifo ni wa Masia wee,

Kifo ni wa Mohammed Kipande,

Kifo ni wa Salumu abdala,

Kifo ni wangu baba,

Kifo we kifo wee,

Kifo ni wa Niko Zengekala,

Kifo unaua hata kipofu kifo weee,

Kifo siku ya mwisho kweli walimwengu hatukupendi,

.....

Remmy Ongala & Super Matimila - Kifo.
 
Kifo kifo

Kifo ni wa Baba Romee,

Kifo ni wa Lushiku,

Kifo ni wa Masia wee,

Kifo ni wa Mohammed Kipande,

Kifo ni wa Salumu abdala,

Kifo ni wangu baba,

Kifo we kifo wee,

Kifo ni wa Niko Zengekala,

Kifo unaua hata kipofu kifo weee,

Kifo siku ya mwisho kweli walimwengu hatukupendi,

.....

Remmy Ongala & Super Matimila - Kifo.
Just refer him as Doctor
 
..... nilikupenda kimapenzi solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
 
Huyu jamaa alikuwa na sauti tamu sana. Kila nikisikiliza nyimbo zake huwa namkumbuka marehemu baba.
Kumbukumbu inanirudisha mwaka 1995 wakati ambapo baba alininunulia suti ya kaptula, wakati ananikabidhi kuna wimbo wa hasira hasara ambao kuna sauti yake.
Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho kupokea zawadi kwa baba kwani alifariki miezi michache baadae.
Pole saana mkuu
 
[Mwanzo] Rudi Table
Solemba - JUWATA JAZZ(Nico Zengekala)]
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
Nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na
dharau tele
Ungenieleza ukweli solemba,
Kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya
kweli.
(Chorus)
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba sababu ya
kukungoja wewe
Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
Nimeshituka Solemba ,
Nimeshituka Solemba
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Sikutaki tenaaa, sina haja nawe,nimeshapata
mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha
kama mimi
Huna huruma Solemba.......Aloi I love you
baby
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
Rudi mwanzo
[TUMA - Nico Zengekala]
Nilisimama kwenye kona, ya uhuru na
msimbazi,
Natizama wanaopita , wanaorudi mamaaaa,
Huenda nikaiona sura yake tuma.
Nasimama nikiwaza, ahadi yetu tuliopanga,
Tukutane Darisalama, Tuma mama,
Nia na madhumuni wazazi watuone.
Nilishikwa na mnutsuko shoga yake
aliniponiejia na kunieleza
Tuma ee tuma ee keshaolewa
Nilishikwa na mshituko mapigo ya moyo
enda mbio
Sikutegemea Tuma, kama angevunja ahadi
yetu ama kweli penye uzia hupenyeza rupia
CHORUS:
Usinione nimekonda ewe Tuma, hakuna
lingine mama
Ila ni wewe Tuma.
(Usiku wote nalala nikikuwaza nakuita jina
lako oh oh Tuma)
Repeat: Usinione nimekonda ewe Tuma.
Rudi mwanzo
Nimeimba hadi mwisho
 
Back
Top Bottom