Nicole joyberry apandishwa kizimbani, akosa dhamana apelekwa segerea

PSL god

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2023
Posts
8,435
Reaction score
6,476
Joyce Mbaga (32) maarufu kwa jina la (Nicole Berry) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Ramadhan Rugemalira kwa tuhuma za kupokea Shilingi milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Mbali na Berry, mshtakiwa mwingine ni Rehema Mahanyu (31). Kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makosa matatu, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa umma na kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24, 2025, ambapo washtakiwa hao wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili na kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.


 
Mbona hapo Tako silioni?
 
Matapeli wengisanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…