NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao

NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao

Hawa NIDA wanashangaza sana, huwezi kutoa muda mfupi kiasi hicho maana wengine tulihama mkoa kutokana na ajira halafu hata help line zao wameweka namba za simu mtandaoni ukipiga muda wote simu inatumika. Nimewatumia email kuwajulisha kuwa nimehama mkoa kikazi hata hawajibu. Hizi taasisi za serikali zinaendeshwa kihunihuni utafaikiri hamna watu wenye weledi.
 
nILIENDA SERIKALI ZA MITAA HAPO KAWE ET WANATAKA PESA WAKAKIFUATE NIKAAMUA NI SEPE NIKARUDI TENA SIKU NYINGINE HIVYIHOIVYO LEO NIMEENDA WILAYANI ET SUBIRI SMS SI UFWALA HUO WANAFIKIRI NAULI TUNAOKOTA AU?
WAMEKAA KITAPETAPELI KAMA VILE HIVYO VITAMBULISHO TUNAENDA NAVYO PEPONI WABAKI NAVYO
 
Kuna baadhi ya ofisi za NIDA wamekataa kuruhusu watu kuchukua vitambulisho mpaka waonyeshe sms ya NIDA kwenye simu.
Kuna watu wamefuta sms kwa bahati mbaya,wengine simu zimeibiwa,wengine simu zimeharibika na laini,nk
Sasa hapa kuna logic gani ya kuwazuia wasichukue vitambulisho?
 
Naona changu wameshafunga wapuuzi Hawa.
Nilituma mtu Hadi nilipojiandikishia Arusha Wakakataa. Foolish.
 
NIDA wanakurupusha wananchi, kuna wengine walijiandikisha mbali mikoani na walihama bila kuondoka na vitambulisho hivyo kwani wakati wanahama vilikuwa bado havijatoka. Watoe muda mrefu angalau miezi mitatu wananchi wafanye follow up kufuatilia vitambulisho vyao huko mbali kabla hawajasitisha matumizi ya namba hizo
Pia kitambulisho cha mtu kikiwa tayari ataarifiwe kwa ujumbe wa simu
 
Tayari kuna wananchi namba zao zimesitishwa na NIDA/TCRA baada ya muda wa mwezi mmoja kukamilika bila kwenda huko mikoani kuchukua vitambulisho vyao. Kikubwa TCRA wasiwaamuru makampuni ya simu kuzima namba za simu zilizosajiliwa kwa NIDA, watambue wenye vitambulisho wapo hai na vitambulisho vyao watavichukua, isiwe kero
 
Back
Top Bottom