NIDA mliangalie hili

NIDA mliangalie hili

Wewe ni mmoja wa wale mabinti wa NIDA ambao tunawakutaga ofisini mnachati huku wateja wamekaa kwenye bench wanasubiri? Na mkisalimiwa au kuelezwa shida mnabinua midomo kwa nini?
Shida ni wewe unapo download kitambulisho kinakuja katika mfumo wa pdf

Inawezekana wewe ,wakati una download kifaa chako hakikuwa na app ya ADOBE PDF ,

Mabadiliko ya kimfumo huwa yanakuja na changamoto tatixo hatukubali changamoto zilizopo tunataka kuwa kama makinda ya ndege kila kitu kulishwa

Tubadilike ...Taifa letu lilikuwa nyuma sana , mfumo km huo wa nida nimekuta ujerumani mwaka 2006 wanatumia na watu walishazoea kabisa

Tatizo upuuziaji wa mambo ndio unapelekea leo wananchi wengi kuanza kuhangaika kama popo

Mfumo wa portal umeanzishwa ni kwa kila mtu tukiamni kuwa karibu kila familia moja kuna mwana familia anamiliki ....smart phone ,sio kwenda stetionary

Ukienda stetionary lazima wakuchaji gharama na wao si wanataka faida ......

Tubadilike tukubali ...mabadiliko ya kiteknolojia ndio mwanzo wa huduma nyingi kuboreshwa

Na mwisho wale ambao hawajajisajili kabisa nida naomba waaanze kulipia , kuanzia wenye miaka 19. Na kuendelea ambao zoezi limefanyika wapo tu wanajidai wazee wa mishe

Huduma iendelee kiwa bure kwa wale waliokuwa na sababu maalumu tu kama ugonjwa,ajali ,safari na ambao hawakuwa wamefikisha miaka 18

MUNGU IBARIKI ...NIDA HASA MKURUGENZI WAKE ..PAMOJA NA MA I.T OFICER WA KILA MKOA , MBARIKI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AENDELEE NA MSIMAMO HUO HUO !!

Sent using i phone x

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hela ya chapati mbili....
jamaa bahili kinyama...
muda atakaotumia utakuwa ni mwingi sana kuliko hiyo bk 4
Nshapiga na Picha Jombaa, 4000 niliona nyingi coz natumia computer tangu laptop hazijaingia so sikuona kwa nini iwe gharama hivyo, imagine kuprint ni 500 afu tuseme nimeenda internet cafe nikalipia 700 nusu saa nkafanya na mishe zingine huko net halafu jumla ikawa 1200, tuache hiyo nilitumia bando langu na sikusota kama unavyozani, kama unabisha nitumie 2000 hapo 0000124587265
 
Ndugu mpaka nimepost ni jambo limenikera sana, pia nikujulishe PC yangu ina run paid version of adobe(Premium) coz naitumia kwa ishu muhimu, another thing ni kuwa in case you don't know i am an IT guru. Nachojaribu kukwambia ni kuwa sacha kuwa unahukumu watu kwa kesi usizozijua. Pia uache kiherehere, Serikali imesema ID ni bure we unataka watu walipie kwa kuwa we umepata sio? Jitafakari roho ya kichoyo haitakupeleka popote. Sijakasirika nimekuambia tu kukushauri maana siku hizi watoto mkiwa na 10,000 mfukoni mnadhani hamna mtu mwingine atakuwa na 10000. Pia ujue portal ya NIDA haipo tu mtu kuona ID yake kuna watu walienda kuandikisha wakaombwa ID za wazazi ikabidi wasubiri zitoke waprint na NIDA wanatambua hilo, wewe tu ndo bado hujajua.
Ww ndiye mbishi mm ninacuokuelekeza nakijua kuliko hata wewe

Sent using i phone x
 
mara zote ambazo mimi nimedownload inakuja in PDF format. lakini hata kama machine haina Adobe reader sidhani kama inawezekana ikaconvert to other format bila wewe kuiamrisha ifanye hivyo. naomba wasamehe wote, hasahasa NIDA wenyewe labda kwa sababu sasa hivi they are running to meet the ultimatum.
 
kitu ambacho nakiona pia ni unnecessary kero ni hii ya kuambiwa taarifa zako zote zipo isipokuwa picha ndiyo haipo!! hivyo anza upya mchakato. allas! mpaka taarifa zote kuwapo maana yake nilipigwa picha. ok inawezekana kabisa picha ikakosekana baada ya kusave maana hayo hutokea pia kutegemea na ujuzi wa mtu. kwa nini msinipige tu picha badala ya kuniambia nianze upya??!???!!!?.
 
Leo uzi wangu naikosoa NIDA hasa katika kipengere hiki cha kuprint ID copy online. Ni jambo zuri na mnastahii kupongezwa kwa hilo ila mtu aliyepitia adha za huduma hii hawezi kuwapongeza, mimi nikiwemo.

Tuanze hivi, nilienda statinary kuprint ID nikaambiwa 4000, nikaona siwezi kuvumilia ujinga wa wafanya biashara wa kibongo kupandisha bei inapotoea dili, basi nikarudi zangu maskani nikaingia NIDA id verfication portal nikadowload ID yangu ili nikai print nipeleke inapohitajika.

Mama weeeee! ikaja katika mfumo wa .gif. Tuzungumzie GIF kidogo, hii ni kifupisho cha GRAPHICS INTERCHANGE FORMAT, ambayo huwa haipotezi ubora wa picha (lossless format), mfano wake ni vile vipicha unaona kitacheza na hakina sauti. Ok huu ni mfumo mzuri wa kuhifadhi ubora lakini hata mifumo mingine kama PNG, JPEG nk nayo haipotezi ubora kiasi cha macho kuona ubora umepungua.

Shida ni kuwa hizi .gif files huwezi kuzifungua moja kwa moja kwenye computer mpaka uwe na software tool, au unajua kucheza na computer (jambo ambalo kwa watanzania lipo kushoto). Hapa nachojiuliza ni kuwa kwa nini NIDA waweke kwenye mfumo huu wakati lengo lao ni kumrahisishia mwananchi mnyonge apate Copy ya ID yake kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Binafsi nimekerwa sana na watu wa stationary maana wamekuwa kama wauza nyama buchani na NIDA ndiyo sikukuu yao. NIDA nadhani mmeliona hili hakuna point ya kuwa na hii service kama mtu hawezi kujihudumia mwenyewe. Sometimes unaambiwa tuma picha ya ID sasa wew mwenyewe huwezi ifungua utamtumiaje mtu ambaye pengine ni ajira au unataka mkopo.
YANGU NI HAYO.
Bora hata wewe hii hatua umeifikia.. Kuna kina sisi kila siku tunaliwa mia mia zetu kupata namba tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naweza pata wapi Online id copy kwa Sasa.Maana nida wamesitisha kutoa katika website yao
 
Back
Top Bottom