NIDA; urasimu wa upatikanaji wa NIN number online, umegeuka fursa(dili) kwenye ofisi za wilaya. Kupata NIN yako bila kutoa chochote, sahau!

TATACHACHA

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
793
Reaction score
1,671
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa tanzania ( NIDA) sidhani kama walikuwa na lengo la kukamilisha mradi huu kwa wakati,

Nahisi kuna watu ndani ama nje ya idara hii kwa makusudi na kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wanaosababisha kadhia hii iendelee kwa makusudi kabisa.

Urasimu huu unakuja hasa kutokana na kitambulisho hichi ama namba kuhitajika sehemu mbali mbali hasa katika kupata ajira mahali fulani, na hii sheria imeletwa na serikali yenyewe huku ikijua kabisa haijajipanga kikamilifu( kiteknolojia) kumalizia kadhia hii kwa wananchi.

Haiingii akilini zoezi lilioanza kiujumla kwa nchi nzima zaidi ya miaka mitano iliyopita, mpaka sasa bado watu hawajapata namba wala vitambulisho kweli!?

Nimekwisha kuijaribu hii system yao ya kufetch NIN number online pia nikiwa na details Kamili na vitambulisho vitatu tofauti ( halali kabisa!) Na hakuna details iliyokosewa. Lakini inaleta msg " unable to fetch nin number!" What a hell!

Ni system gani ya kipuuzi hii inayoshindwa kutambua hata kitambulisho ilichokitengeneza yenyewe!?

....inachekesha na kusikitisha sana!...

Kisingizio kimekuwa kile kile eti " vinachapishwa kwa awamu!" Nonsense!

Kwa sasa vijana wanaoomba ajira kwenye kampuni yoyote kigezo cha kwanza ni kuwa na NIN number, na hii imepelekea urasimu ofisi za NIDA wilaya hasa hapa nilipo, kupata NIN number kwa haraka bila kuwa na 30k-50k kuendelea ndipo unapewa NIN kwa haraka. Imegeuzwa mradi kama urasimu uliopo kwenye kupata leseni ya udereva na hati ya kusafiria.

Mamlaka hii akiwemo mkurugenzi wake inapaswa kujipima, kujitathmini kama kweli inatosha kuwahudumia wananchi.
 
Copy ya kitambulisho nakipateje wakuu
 
Mkuu mtoa hoja pole sana,ulichokielezea kwenye mada yako ni vielelezi kuwa tunaishi in a shithole country, ID ni life book yako unazaliwa nayo na unakufa nayo na ni haki ya kila raia, mtoto anapozaliwa wazazi/mzazi anampa Jina ili amtambue na nchi ilitakiwa ifanye hivyo hivyo, kabla mtoto hajaruhusiwa kutoka alipozaliwa ni lazima nchi imperative Jina ili imtambue na Jina hili ni ID number, mtoto huyu ataishi na number hii na kufa nayo!,for now endelea kulalamika humu na ID fake zetu
 
Hakika hili limekuwa tatizo maana nimeona bila ya kurefusha mkono hufanikiwi mimi mwenyewe ni mhanga wa hii issue
 
Failed state
 
Ili kupata hii namba mtu inabidi uende ulikozaliwa au unaweza kuipata ukiwa po pote ali mradi una vielelezo vyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…