Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Habari zenu wakuu.
Kwa kadri miaka inavyosogea, ndivyo mahitaji ya huduma za haraka na zenye ufanisi yanaongezeka.
"Being Quick, Efficient and Consistent is being Good"
Kasi ya maisha ya mwaka 1980 haiwezi kuwa sawa na ile ya 2020.
Katika taratibu za kawaida za kazi, kuanzia siku ambayo utakua umekamilishia taratibu zote (umepiga picha na kuchukuliwa fingerprints) pale uhamiaji, unapewa passport yako baada ya wiki mbili.
Kwa upande mwingine, kuanzia siku ambayo umekamilisha taratibu zote (umepiga picha na kuchukuliwa fingerprints) pale NIDA, itakuchukua Mwaka mmoja, hadi miwili au awamu nzima (miaka mitano) kupata kitambulisho chako.
Mnaojua hebu tujuzeni na sisi, kwani kuna ugumu gani kutengeneza kitambulisho cha taifa ukilinganisha na ugumu uliopo kwenye kutengeneza passport ?
Pili, ukishakamilisha "taratibu zote" pale NIDA, unapewa wiki tatu ili upate namba ya NIDA (NIN) ? How comes a computerised system generates "numbers" at such a slow pace ?
Yaani siku zote 21 namba tu ?
Tatu, uki "renew" kadi yako (baada ya ile ya awali kupotea au kuharibika, n.k), inaweza kukuchukua miezi sita hadi mwaka kuipata tena, mara baada ya kukamilisha taratibu zote.
Na hii ni hata kama haubadilishi chochote katika taarifa zako.
Yaani ku "reprint" tu, utasubiri miezi sita hadi mwaka.
Tusiwe wasiri, kuna ugumu upi ?
Juzi hapa "tumesaini" mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Makutupora kuelekea Tabora, kwa mtu ambaye alijiandikisha NIDA siku hiyo, anaweza kujikuta anapanda treni ya umeme kutoka Makutupora kuelekea Tabora akiwa hana kadi yake ya NIDA kwenye wallet (bado haijatoka).