DOKEZO NIDA wanatoa vitambulisho kwa madereva wa kigeni kwa lengo la kuwasadia wapate pasipoti za Tanzania; kitambulisho kimoja kinalipiwa hadi milioni moja

DOKEZO NIDA wanatoa vitambulisho kwa madereva wa kigeni kwa lengo la kuwasadia wapate pasipoti za Tanzania; kitambulisho kimoja kinalipiwa hadi milioni moja

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hadi Nelson Mandela na Thabo Mbeki walikuwa na passports za Tanzania.

Ni mambo ya ujamaa hayo.
 
Kama ni hivyo huo uovu wa kiwango Cha juu kabisa Cha kuhatarisha usalama wa taifa kisingefanyika na wahusika wangekuwa wananyea debe cha ajabu ndo wanakula kiyoyozi Cha V8 na ulinzi juu
Ni uzushi tu, ndio maana kashindwa kutaja kampuni husika
 
Nakuomba , kwa gharama zako ufike pale upanga makao makuu ya PCCB, toa taarifa rasmi na kama una jua majibna ya kampuni na ofisi zilipo waambie PCCB. Wanafanya kazi kwa weledi na usiri mubwa.
Utalindwa, utarudishiwa gharama zako, utaweza hata kiupewa nishani kwakuwa umesaidia si tu seriali ila taifa kwa ujumla.
Hawana lolote wale takataka tu, nimeshakwenda mara kibao pale bure kabisa.
 
asee hizo allegations unazotoa pasipo uthibitisho ni matumizi mabaya ya demokrasia
acha kabisa kutoa shutuma kwa namna hiyo kwa taasisi za serikali
 
Ukiwa na hela unaweza kupata cheti cha kuzaliwa, nida, passport na kila kitu hata kama haustahili.

Unampa elfu hamsini tu anakuchongea vyeti vyote kiulaini.

Nchi ina njaa kali, elfu hamsinii unakula hadi unasaza, na kinyeo anakupa BUUREEEEEEE......

Cc: Poor Brain Extrovert
Tatizo bichwa uwezi andika kitu mpaka uweke neno kinyeo 😁😁😁🚬🚬.
Hapo naomba usirudie tena bana plzi
 
upuuzi mtupu na kumbuka mwaka jana nilifika office za Nida nikiwa na vielelezo kasoro cheti chakumaliza darasa la saba, wakauliza kiko wapi nikawapa maelezo kwamba toka nilivyo maliza shule ya msingi siku fuatiliaga coz niliondokaga mikoani kujitafuta. walinikatalia eti mpaka niwe nacho, nawakati kuna watu nili washuhudia kwa macho yangu wakipitishwa mlango wa pili wanaingia wanapigwa picha nakupewa namba kabisa kwasababu ya rushwa, kifupi hao NIDA na immigration wana njaa za kijinga wana nyanyasa wazawa nakukumbatia wageni
 
Kwa sisi wamiliki wa makampuni ya usafirishaji mizigo ambao kwa kiasi kikubwa tumeishi nje tunaona kama hali hii siyo salama kwa nchi yetu .
Ondoa neno "Kama", Uko sahihi, Na kwa hili dokezo ndio uzalendo wenyewe, Hongera kwa hili.

Mamlaka husika iangaziwe, hili ni tatizo likomeshe haraka iwezekanavyo.
 
Nasimama na maofisa wa NIDA waliopo katika maeneo mengi nchini. Madereva na wasaidizi wao wanaofanya safari kwenda nje ya nchi kupeleka mizigo wanapewa vitambulisho vya Tanzania na baadaye zile pasipoti za muda mfupi.

Vitambulisho hivi vinatolewa zaidi kwa wageni waliopo DAR es salaam. Makampuni mengi Yenye umiliki wa watu wenye asili ya Burundi, Malawi, Nigeria, Kenya, Somalia,Rwanda na Waarabu wafanya kazi wake uanza kazi kama wageni then after short time kwa lengo la kukwepa kusumbuliwa na Uhamiaji utafuta vitambulisho vya NIDA na pasipoti wawe kama watanzania.

Vitambulisho hivi utolewa zaidi kwa mtandao wa wanahisa ambao ni wanasiasa wanaelekeza maafisa watoe vitambulisho na Pasipoti Ubungo, Temeke, Kinondoni, Ilala, Kahama, Makambako, MBEYA, Songwe, Arusha, Ngara, Karagwe, Ushirombo, Kigoma na Nyakanazi.

Mbinu zinazotumika ni pamoja na
1. Wamiliki wa makampuni wanazungumza na viongozi wakubwa wa taasisi wakiwadanyanya kwamba kuna ndugu yao anahitaji NIDA au pasipoti ya haraka na kwamba maafisa wanawakwamisha. Zinapigwa simu maelekezo yanatoka wanapata documents

2. Kuna Vishoka maalumu ambao wanachukua si chini ya milioni mbili hadi tatu kwa kitambulisho kimoja. Ikumbukwe kwamba wengi wa watu hawa ni wanafamilia wa matajiri wa kigeni waliopo hapa nchni ambao wanakosa sifa za ajira kama wageni.

3. Wanatumia maafisa wa NIDA wasio waaminifu kupata vitambulisho. Sometimes baadhi wanapewa hadi vitambulisho zaidi ya kimoja na wao ugawana na wale ambao lugha ya kiswahili inasumbua.

4. Wanapokwenda kuomba pasipoti utuma watu kwani wanaogopa kushtukiwa kwa lafudhi zao.

5. Wanatumia familia za kitanzania kama vile wao ni watoto wa hizo familia.

Kwa sisi wamiliki wa makampuni ya usafirishaji mizigo ambao kwa kiasi kikubwa tumeishi nje tunaona kama hali hii siyo salama kwa nchi yetu . Wanasiasa na viongozi wakubwa wanapotumika kuelekeza wageni wapewe huduma si jambo jema.

Wateja wanapotumia vishoka kutekeleza uhalifu si jambo la afya sana kwa nchi. Lakini pia watanzania wengi wanakosa kazi kwa sababu ya wageni kupeana kazi hasa eneo la bandari ya DAR es salaam. Tunakumbuka tukio la Westgate. Hawa wanaotumia fedha na connection kujipatia Utanzania wanatupelekea tuwe hatarini.

Lakini pia changamoto nyingine ipo kwenye sheria za NIDA na UHAMIAJI; nimeripoti mara kadhaa wageni wenye vitambulisho vya NIDA Uhamiaji. Niwapongeze sana UHAMIAJI wanapopata hizi taarifa wanafanikisha kuwakamata wahusika na kuwapeleka mahakamani.

Lakini chakushangaza wakikamatwa wanafika mahakamani asubuhi mchana wamelipa faini na kuachiwa. Unajiuliza kweli faini ya mtu aliyejipatia uraia wetu kinyume cha sheria inakuwaje laki tano?

Mgeni anagushi taarifa anapata kitambulisho cha NIDA analipaje faini ya laki mbili mahakamani? Mawakili kwenye kesi moja wanalipwa kati ya milioni ishirini hadi hamsini kusimamia kesi ya msomali mmoja anapofikishwa mahakamani. Sheria inasema faini laki tano huku watanzania wanasota mahabusu bila dhamana kwa makosa ya kawaida kabisa.

Tunapeleka wapi hii nchi? Kwanini tusiweka adhabu ya kifungo cha miaka kumi na tano ukikutwa na kitambulisho au pasipoti ya Tanzania?
Lakini pia wanasiasa wengi hata wakisikia mgeni amekamatwa na NIDA wanaingilia kati asifikishwe mahakamani....nchi yangu Tanzania mambo yamebadilika sana. Viongozi someni habari za Kongo, South Afrika, Kenya, Syria mk mtaona madhara ya kuachia usalama wa nchi kuingiliwa na matajiri.

Hawa matajiri wanaolindwa na wanasiasa na viongozi wetu wana nchi zao za asili ila sisi watanzania hatuna nchi nyingine. Pelekeni sheria ya Uhamiaji, RITA na NIDA bungeni mkaondoe mafaini hawa watu wakaozeee jela kwa usalama wetu. Mkiendelea kutoza laki tano mahakamani ipo siku tutalipuliwa huku ndani kwani kila mtu anatamani kuwa mtanzania .

Lindeni madereva, maafisa masoko, Wasafirishaji wa Tanzania kwani wageni wameona fursa ya DP world lakini pia wapo maadui wanatumia uzembe wa dola kuifanya biashara ya Tanzania isistawi. Amkeni Amkeni Amkeni tupige vita wageni kupewa pasipoti na vitambulisho vya Tanzania.

Watanzania amkeni amkeni acheni kuwakumbatia wagen kwa kudanganya kwamba ni wanafamilia wenzenu........
Nchi ina laana hii,ujinga kama huo huwezi kufanya hata hapo rwanda tu,miaka ijayo tusipokuwa makini Tanzania yetu itakuja kuongozwa na raisi au mkuu wa vyombo vya ulinzi asiye raia,
na hii ni hatari kwa usalama wa Taifa, halafu mbona kawaida kila taasisi ya serikali huwa kuna maofisa wa usalama wa Taifa wasiotambulikana, sasa inakuaje hujuma kama hizo kutokea?au na wao ndio tuseme binadamu na watoto zao wanaitaji kwenda toilet!!!?
 
Nakuomba , kwa gharama zako ufike pale upanga makao makuu ya PCCB, toa taarifa rasmi na kama una jua majibna ya kampuni na ofisi zilipo waambie PCCB. Wanafanya kazi kwa weledi na usiri mubwa.
Utalindwa, utarudishiwa gharama zako, utaweza hata kiupewa nishani kwakuwa umesaidia si tu seriali ila taifa kwa ujumla.
Ili afe,dada humtakii mema mwenzio
 
Tanzania Imekumbwa Na Nini Sasa Hivi? Mpaka Hali Imekuwa Hivi
 
Back
Top Bottom