muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Juzi kocha wa Taifa Stars, Emanuel Amunike raia wa Nigeria aliamua kuwafuta wachezaji takribani wa tano wa timu ya Simba ambao ni Dilunga, Bocco, Mkude, kichuya, Nyoni kwa kile kinachodaiwa ni kuchelewa kufika kwenye kambi ya Timu ya Taifa.
haibishaniwi wachezaji hao inawezekana walichelewa kufika kwenye kambi hiyo, je walipewa muda wa kujieleza? Right to be heard....., wachezaji hao ni waajiriwa wa klabu zao, lazima wapewe maelekezo na klabu zao, je kabla ya kupiga hilo panga mlifanya mawasiliano yoyote kujua sababu za wao kuchelewa.
Kama hamjafanya hivyo,Tff pamoja na kocha kwa ujumla amuoni mnatengeneza chuki kati ya wachezaji na watanzania wapenda soka, Leo hii watu waone Mkude au Dilunga anachelewa kwenye kambi ya Taifa, kiurahisi sisi mashabiki tutatafsiri kuwa anaringa, sasa tutaanza kujiuliza anaringa ana nini? wakifika huko kwa kina farid musa au samatha itakuaje sasa? na hapa kwetu kuna uyanga na usimba, ukiwakuta wale wa upande mwingine lawama zote wanawapa wachezaji kwa maneno mengi ya kebehi.
Lakini ikumbukwe kama ili limefanyika kwasababu ya kupata kick na kufanya amsha amsha kwa wapenda soka, mmewaaribia hawa vijana kwa mashabiki wao wanavyo tafsiriwa inawezekana tofauti, na hii ndiyo inatengeneza chuki kati ya kocha na wachezaji nakufanya wachezaji wacheze chini ya kiwango.
Hakuna kitu kizuri kama kuthamini, kujali mtu mwingine kuliko kufanya kazi kwa mihemuko ili upate kick kwa kuwadharirisha wengine kwenye jamii, Amunike kama umefanya hivyo kwa kushinikizwa na hao watanzania wenzetu hapo Tff, kuwa makini miluzi mingi inampoteza mbwa.
Hakuna kipindi ambacho hamasa ya soka ilikuwa juu kama kipindi cha Maximo kwenye timu ya Taifa, na alikuwa mkali na misimamo hatari sana lakini hakuwahi kufanya hiki ambacho kimefanyika, sio kwamba adhabu haziitajiki la asha.....tufuate taratibu na kanuni tulizojiwekea, soka ni mchezo wa hisia unaweza ukatengeneza chuki, wachezaji wasikae kwa raha mtaani kwao, kwasababu ya chuki na hasira za mashabiki.
Tutafute njia sahihi ya amsha amsha tusitake kupitia kwa wachezaji walioichezea timu yetu kwa muda mrefu alafu leo mnataka waishie kwenye dimbwi la aibu.........
TAIFA STARZ "THE BLUE OF AFRICA "
Sent using Jamii Forums mobile app