Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi wanabodi!
Hata tuwe na makusanyo kikodi ya trilioni 100 kwa mwezi kama hatutakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za wananchi nchi yetu itaendelea kuwa maskini milele!
Ukweli ni kwamba, hata haya makusanyo madogo tunayokusanya kupitia TRA, endapo Viongozi wetu wangeheshimu kuwa hizi ni kodi za wananchi na kuzitumia kwa nidhamu Nchi yetu ingepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka sana!
Leo hii tunaona wasanii wakisafirishwa kwa makundi kwenda nchi za Nje kwa kodi za wananchi.
Leo hii tunaona Serikali ikinunua magari ya kifahari kwa viongozi wake na wakati mwingine magari hayo yanatumika katika shughuli za Chama cha Mapinduzi. Haya yote ni kodi za wananchi
Leo hii tunaona kiongozi anaamua tu kugawa pesa anavyojisikia. Kwa kuwa haulizwi kazitoa wapi na ni za kwake au za Serikali basi anagawa tu atakavyo. Hizi nazo ni kodi za Wananchi
Leo hii tunaona mabango na picha za Viongozi kila mahala hadi kwenye mechi za mpira watu wanaingia na picha na tshirt zilizokuwa printed za Viongozi. Ukiangalia haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za Wananchi.
Tuliona awamu ya Tano, Rais Magufuli alikuwa anatembea na mabulungutu ya hela huku akigawa kwa mtu yeyote anayejiskia mtaani. Zote zile ni kodi za wananchi.
Leo tunaona shughuli sizizo na msingi, mara kupokea Mwenge, mara kupokea ndege, mara uzinduzi wa hiki na kile. Yote haya ni matumizi yasiyo sahihi ya kodi za wananchi.
Nipende kuwaasa Viongozi. Ingawa Watanzania wanaweza kuwa wajinga kwa wakati huu ila nina uhakika hawatakuwa wajinga milele. Kuna siku watapata akili na kuhoji namna mnavyotumia vibaya kodi zao.
Ipo siku wanaweza kugoma hata kulipa kodi maana wanaona kodi wanayolipa inamsafirisha na kumpa hela Irene Uwoya aende Korea kusini kupiga picha na kuuza sura.
Kwa Wananchi.
Pambaneni sana kupata Katiba Mpya. Katiba inayoweka misingi ya uwajibikaji na kuwawajibisha Viongozi wanaotenda kinyume chake au kinyume na Sheria za Nchi.
Msingi wa Uwajibikaji ni Katiba. Msingi wa kuheshimu Sheria za Nchi na Katiba ni Katiba yenyewe.
Machawa tunaowalalamikia wanatunzwa na fedha zetu / kodi zetu ambazo zinatumiwa hovyo kwa sababu Katiba haijaweka misingi mizuri ya kuheshimu kodi za wananchi.