Nidhamu katika Matumizi ya Kodi za Wananchi kwa Serikali na Viongozi wa Umma

Nidhamu katika Matumizi ya Kodi za Wananchi kwa Serikali na Viongozi wa Umma

Amani iwe nanyi wanabodi!

Hata tuwe na makusanyo kikodi ya trilioni 100 kwa mwezi kama hatutakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za wananchi nchi yetu itaendelea kuwa maskini milele!

Ukweli ni kwamba, hata haya makusanyo madogo tunayokusanya kupitia TRA, endapo Viongozi wetu wangeheshimu kuwa hizi ni kodi za wananchi na kuzitumia kwa nidhamu Nchi yetu ingepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kwa haraka sana!

Leo hii tunaona wasanii wakisafirishwa kwa makundi kwenda nchi za Nje kwa kodi za wananchi.

Leo hii tunaona Serikali ikinunua magari ya kifahari kwa viongozi wake na wakati mwingine magari hayo yanatumika katika shughuli za Chama cha Mapinduzi. Haya yote ni kodi za wananchi

Leo hii tunaona kiongozi anaamua tu kugawa pesa anavyojisikia. Kwa kuwa haulizwi kazitoa wapi na ni za kwake au za Serikali basi anagawa tu atakavyo. Hizi nazo ni kodi za Wananchi

Leo hii tunaona mabango na picha za Viongozi kila mahala hadi kwenye mechi za mpira watu wanaingia na picha na tshirt zilizokuwa printed za Viongozi. Ukiangalia haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za Wananchi.

Tuliona awamu ya Tano, Rais Magufuli alikuwa anatembea na mabulungutu ya hela huku akigawa kwa mtu yeyote anayejiskia mtaani. Zote zile ni kodi za wananchi.

Leo tunaona shughuli sizizo na msingi, mara kupokea Mwenge, mara kupokea ndege, mara uzinduzi wa hiki na kile. Yote haya ni matumizi yasiyo sahihi ya kodi za wananchi.

Nipende kuwaasa Viongozi. Ingawa Watanzania wanaweza kuwa wajinga kwa wakati huu ila nina uhakika hawatakuwa wajinga milele. Kuna siku watapata akili na kuhoji namna mnavyotumia vibaya kodi zao.

Ipo siku wanaweza kugoma hata kulipa kodi maana wanaona kodi wanayolipa inamsafirisha na kumpa hela Irene Uwoya aende Korea kusini kupiga picha na kuuza sura.

Kwa Wananchi.
Pambaneni sana kupata Katiba Mpya. Katiba inayoweka misingi ya uwajibikaji na kuwawajibisha Viongozi wanaotenda kinyume chake au kinyume na Sheria za Nchi.

Msingi wa Uwajibikaji ni Katiba. Msingi wa kuheshimu Sheria za Nchi na Katiba ni Katiba yenyewe.

Machawa tunaowalalamikia wanatunzwa na fedha zetu / kodi zetu ambazo zinatumiwa hovyo kwa sababu Katiba haijaweka misingi mizuri ya kuheshimu kodi za wananchi.
Kama waziri wa fedha aliingia bungeni na msafara usio tija kwenda kusoma bajeti ili kukoga wananchi, usitegemee matumizi sahihi ya fedha za wananchi. Kila siku nasema bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi, tusitegemee mabadiliko yoyote ya maana hapa nchini. Hii nchi inatakiwa factory reset ili tuanze upya kiutawala.
 
Aaah mkuu acha hizi bhana ......usitaje majina ya watu kwa kuwatweza hivyo bhana.
Muhuni mtaje kwa jina ili ujumbe ufike kwa usahihi. Hii tabia ya kutaja kwa kufichaficha ndio imesababisha tuendelee kupigwa.
 
Kiukweli viongozi wetu hawafanani kabisa na wapigakura wao..wanakula hadi wanavimbirwa ndio maana wakitenguliwa kwenye hizo nafasi WANAPAGAWA

Magari ya kifahari ilihali hali ya barabara kwa sasa ni nzuri,lami sehemu kubwa ya nchi
Kutwa wapo barabarani Dar - Dom - Dar

Nyumba mbili mbili ,Dar na Dodoma na zote zinahudumiwa

Misafara ya kutisha wawapo kwenye shughuli za kiserikali mikoani

TUANZE KWA KUDAI KWA NGUVU ,KATIBA MPYA ILIYO BORA KAMA MSINGI NA DIRA YA UWAJIBIKAJI
Hakuna uwezekano wa kupata katiba mpya nchi hii kwa njia ya amani. Machafuko pekee ndio njia itatupatia katiba halisi ya wananchi.
 
Muhuni mtaje kwa jina ili ujumbe ufike kwa usahihi. Hii tabia ya kutaja kwa kufichaficha ndio imesababisha tuendelee kupigwa.
Alafu wanapiga picha wenyewe na kutuma kwenye akaunti zao za mitandao!
 
Tatizo kubwa zaidi lililopo kwa Watawala wa Afrika ni UKOSEFU MKUBWA SANA WA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA KODI ZA WANANCHI.

Hili ni janga kubwa Sana ktk nchi zote kabisa zilizopo barani Afrika
Na kwa hili tutaendelea kupiga mark time mpaka watanzania tutakapojielewa. Watanzania tumedumazwa kiakili na wachache wanaoliewa hili wameshatumia nguvu nyingi kuwaelewesha watanzania mpaka kuyaweka maisha yao rehani lakini wanakosa support mpaka wanakata tamaa. Wacha tuendelee hivi hivi ni Mungu mwenye ataingilia kati "Heri ya wale wenye mioyo ya huruma juu ya wengine na Mungu anawaona"🙏
 
Kama Nchi yale mambo yaliyotokea kwa majirani mpaka kupelekea Rais wao kuunda kamati kufuatilia mikopo,kusitisha ununuzi wa magari kwa miezi 12 isipokuwa ya usalama nk. Ingekuwa busara kubwa kama yote yanayofanyiwa kazi na majirani basi nasi tuyafanyie kazi tusisubiri Generation Z ya Tanzania ilazimishe mambo.
 
Sidhani kama kuna nchi ambayo kodi za wananchi zinatumiwa vibaya kama Tanzania.

Viongozi wetu wasipobadilika kuna siku yatakuja kutokea ambayo wataomba dunia ipasuke katikati waingie
 
Kama Nchi yale mambo yaliyotokea kwa majirani mpaka kupelekea Rais wao kuunda kamati kufuatilia mikopo,kusitisha ununuzi wa magari kwa miezi 12 isipokuwa ya usalama nk. Ingekuwa busara kubwa kama yote yanayofanyiwa kazi na majirani basi nasi tuyafanyie kazi tusisubiri Generation Z ya Tanzania ilazimishe mambo.
Akili na busara hiyo, hawana...wamejawa na KIBRI na DHARAU
 
Hakuna uwezekano wa kupata katiba mpya nchi hii kwa njia ya amani. Machafuko pekee ndio njia itatupatia katiba halisi ya wananchi.
Tuwape muda.
Kama wanaona mbele watafanya bila kushurutishwa
 
Tuwape muda.
Kama wanaona mbele watafanya bila kushurutisha
Tuko nje ya muda kwenye madai ya katiba mpya, kwa bahati mbaya mchakato wa katiba mpya unaporwa na wasioitaka katiba mpya. Nasisitiza hakuna uwezekano wa kupata katiba mpya ya wananchi itakayoratibiwa na hawa hawa wasioitaka.
 
Nasema hivi katiba haiwezi saidia chochote kama wananchi wenyewe wasipobadilika. Taifa lenye raia wasiojiamini ni rahisi wanasiasa kujiona na miungu watu. Taifa ambalo kila msomi na asiye msomi anaamini ili awe tajiri ni lazima aingie kwenye siasa ili apate teuzi, cheo au madaraka ni ngumu kuendelea.
Katiba ni mwarubaini mkubwa.mambo mengi yanayotukia sasa nikwasababu ya katiba.huu uchawa na matumizi ya ovyo nikwasababu ya ubovu wa katiba kumpa mtu mmoja madaraka ya kila kitu.Ukiwa na katiba bora wananchi wenyewe watajitune kuishi jinsi ilivyo kama sasa tunavyoishi na hii ya sasa.Kila mtu anaweza kua rais wa nchi itategemea tu na miongozo ikoje.
 
Kweli kabisa

Ingekuwa busara kubwa kama yote yanayofanyiwa kazi na majirani basi nasi tuyafanyie kazi tusisubiri Generation Z ya Tanzania ilazimishe mambo.
Badala ya kurekebisha mambo wanatutaka tumwombe mungu, sijui ni mungu wao yupi huyo anayependa hizi dhulma tunazofanyiwa.
 
Badala ya kurekebisha mambo wanatutaka tumwombe mungu, sijui ni mungu wao yupi huyo anayependa hizi dhulma tunazofanyiwa.
Dini ni kichaka cha wenye nguvu kufanya dhuluma
 
Shirika la reli ni kielelezo cha viongozi wa nchi hii wasivyojua vipaumbele vyao ni nini.

Shirika la reli linamiliki magari hayo ya kifahari mengi kuliko idadi ya mabehewa na injini za kusafirisha mizigo na abiria.

Daah Niliona LC300 ya MKK ni balaaaa.
 
[emoji116]
JamiiForums-1176904024.jpg
 
Back
Top Bottom