Nidhamu katika Matumizi ya Kodi za Wananchi kwa Serikali na Viongozi wa Umma

Mapato yameshuka wanahaha.
 
Hela za umma kwao ni chereko!
Kama DAWASA wasivyojali maji kumwagika mtaani hovyo hovyo na bila kujali gharama wala raia wengine kukosa maji!
Viongozi wa hovyo hovyo SANA SANA HAWA!
 
Katiba iliyopo inatoa msingi wa madaraka kwa wananchi.
Kinachokosekana siyo katiba bali watu wa kuisimamia na kuitetea katiba yenyewe (pamoja na mapungufu ya katiba iliyopo).
Mapambano dhidi ya nira za utumwa yapo tangu enzi na enzi na hayapatikani kwa kuomba maandishi bali vitendo (maandishi yaweza kuwepo, vitendo vikawa tofauti).
Lazima wananchi wajengewe fikra za madai ya vitendo kwanza, maandishi yafuate..
 
Waandishi wa Katiba hii walijua kuwa wakiweka kila kitu wazi wananchi watafunguka akili mapema sana.

Madaraka yamewekwa kwa wananchi na wakati huo huo inasema Rais halazimiki kutekeleza ushauri wowote anaopewa.

Kwa hilo tu Rais kawekwa juu ya hao wananchi.
 
Katiba hiyo hiyo imewapa wananchi namna ya kumuondoa Rais na serikali yake kwa uchaguzi.
Hata hivyo, kuna maelezo kwamba tume haitoi matokeo ya haki.
Hayo malalamiko yanajengeka kwenye fikra hasi kwa sababu tume, serikali, na hata vyombo vya dola ni wachache sana kupinga maamuzi ya mamilioni ya wananchi wenye akili, nguvu na fikra chanya.
 
Umeongea kitu sahihi kabisa nakupongeza kwa mtizamo wako ndugu yangu. Kama nchi yetu ingekuwa, na kitu ambacho wana uchumi wanakiita scale of preference., basi tungeweza kuwa na lami kila kijiji cha Tanzania.
 
Umeongea kitu sahihi kabisa nakupongeza kwa mtizamo wako ndugu yangu. Kama nchi yetu ingekuwa, na kitu ambacho wana uchumi wanakiita scale of preference., basi tungeweza kuwa na lami kila kijiji cha Tanzania.
Sahihi kabisa. Na sio lami tu. Haya masuala ya kujenga madarasa ya wanafunzi, sijui vyoo tungekuwa tumeshaachana nayo kitambo sana!

Kuna hela nyingi sana zinafujwa vibaya sana hapa Tanzania. Alafu kwa kuwa wananchi hawaongei basi na viongozi wanaona ni sawa tu kufuja hizo hela.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kwa harusi zitakazofungwa Arusha Ofisi yake italipia. Ingekuwa nchi za wenzetu huko leo asubuhi angekuwa anekaliwa kooni na walipakodi hadi ameomba radhi maana huwezi tumia fedha za walipakodi namna unavyojisikia tu!
 
"Njia pekee ambayo Wananchi wataitukia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa KUPITIA MTUTU WA BUNDUKI."
Jeff's O'Brien.
 
Kazi yao kuwahubiria wananchi, hii nchi ni masikini sana. Tunahitaji kukopa, toeni kodi kwa maendeleo ya nchi. (Hapa tusikubwa sana)

Nawaambia hii nchi wala siyo masikini, ila wananchi wake ndiyo wamefanywa masikini ili viongozi waishi kitajiri.

Zaidi ya miaka 60 bado tunahangaika na umeme, maji, barabara, madarasa n.k wanakopa kila mara, hizo pesa zinatumiwa kwenye nini? Kama haya matatizo bado tunayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…