Nidhamu ya uwoga iliyozuia wizi kwa Manunuzi pale MSD, ndiyo tunaitaka haraka sana irejee!

Nidhamu ya uwoga iliyozuia wizi kwa Manunuzi pale MSD, ndiyo tunaitaka haraka sana irejee!

Paulsylvester

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2021
Posts
1,464
Reaction score
3,379
Ndiyo,
Tunaitaka haraka sana hiyo nidhamu ya uwoga ambayo Leo tunaona ilikuwa na mapungufu na haifai kumbe iliweza kuzuia ufisadi MSD

Nidhamu ya uwoga ndiyo iliyoleta ufanisi Mkubwa na usimamizi mzuri wa kodi za wananchi karibu kila pahala

Haitoshi tuu kuwa kiongozi sehemu Fulani na uongozi wako usiwe na matokeo yoyote kwa unaowaongoza! Ila itakuwa ni jambo la heshima kubwa na utajivunia popote ikiwa uongozi wako utaleta matokeo kwa walengwa

Jiulize,

Kipngozi, unapata vipi furaha ya kuwa kiongozi ikiwa umekuwa sababu ya watu kupoteza maisha na wengine kupoteza viungo vyao kwa sababu tuu umeshindwa kusimamia vema ili watu wapate huduma?

Ikiwa nidhamu ya uwoga ndiyo inayoweza kusaidia kuondoa wizi na ufisadi, tunaanza vipi kuiponda?

Nakumbuka usemi wa kiongozi mmoja aliyefariki kipindi cha hivi karibuni alisema kwa uchungu hivii

Nyinyi wawekezaji ambao mnaiibia nchi na kwa sababu yenu wananchi wamekosa huduma za msingi, wanakufa kwa sababu mahosipitali hayana dawa, wanakufa kwa sababu wanakosa sehemu ya kujifungulia, wanakufa kwa sababu tuu wamekosa ambulance ya kuwawahisha ili wakapate huduma, mnapata wapi hiyo furaha ya kufurahia watu wakifa kwa sababu tuu mnawaibia Mali zali zao na hamlipi kodi?

Vipi kwako wewe kiongozi uliyepewa dhamana, Utaishambuliaje hiyo nidhamu ya uwoga iliyozuia wizi wa manunuzi ya hovyo MsD na wananchi kupata huduma bora?

Kwa ripoti ya SAG, kuna wizi wa mamiloni pale MSD na hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka sasa, hiyo ndiyo nidhamu tunayoitaka?
 
Kabla ya hasara tunayoipata kupitia MSD huyu mama nae ni hasara kwetu. Nawaza katika safu yake ukianza na yeye mwenyewe , Nape , Riziwani kikwete , nk hivi kuna mwenye uchungu wa.kufikia hata robo ya hayo maneno kweli? Naamini wasingekuwa wanaruka na chopa , wasingeruhusu nguzo ziwe imported , wasingeruhusu MSD iwe shamba la.bibi, tuna ombwe la.uongozi kwa mara nyingine kama nchi tunaandika historia
 
Back
Top Bottom