Nieleweshwe hizi zawadi za Jackpot zinavyotolewa

Nieleweshwe hizi zawadi za Jackpot zinavyotolewa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna jambo limekuwa linanitatiza muda mrefu. Embu wadau nielewesheni.

Mfano jackpot ya Sportpesa inasema jackpot ni 1.2B, ila kuna zawadi kwa kupata mechi 16/17 hadi 12/17 na zawadi zinatajwa. Cha kushangaza, ukija kuangalia matokeo na zawadi zilizotolewa ni kiduchu sana kulinganisha na ile iliyotajwa awali.

1000026519.jpg

1000026518.jpg

Mfano angalia kwenye picha hizo. Mshindi wa mechi 14 walisema anapata 400M, ila alipokuja kupata tena ni mtu mmoja tu kwa hiyo hakuna kugawana, kapewa 4.8M tu.

Hata ukiangalia hao wa 13/17, ukizidisha idadi yao kwa hiyo zawadi waliyopewa inakuja jumla kama 6M tu wakati inaonyesha walitakiwa kugawana 240M.

Hii imekaaje? Au kuna jambo sijalielewa katika hii michezo?
 
Betting inautapeli ndani yake,hawa ni matapeli kama matapeli wengine mkuu
 
Ni hivi wewe umecheza Jackpot ya mechi 17 zote ukakosa tatu ukapata hizo 14 kwahiyo kiufupi umekosa 3 ila umeambulia hiyo bonasi....ili upate hiyo milion 400 ilitakiwa uchague mechi 14 tu kati ya hizo 17 na upate zote 14 ndipo ungekuwa mshindi
Asante kwa ufafanuzi. Nimeelewa. Natumaini ulichosema ndiyo sahihi.
 
Asante kwa ufafanuzi. Nimeelewa. Natumaini ulichosema ndiyo sahihi.
Hizo wanaita bonus, kwenye kila aina ya jackpot yao kuna kila kiasi cha bonus.

Mfano:Kwenye jackpot ya mechi 13 labda mshindi anatakiwa apate milioni 200 kama akitabiri zote 13 kwa usahihi ,bonusi ni kuanzia mechi 10 na 12.

Shida ya bonus ni lazima kushare, mfano kwenye mechi 10 wametenga bonus milioni 5, mkiwa 10 mtaigwana hiyo milioni 5, ila ikitokea ukiwa peke yako utapata yote!

Hali hii huenda pia kwenye ushindi wa hiyo jackpot, ukitabiri zote 13 na ukiwa peke yako utapewa zote! Ila mkiwa zaidi ya mmoja mtaigwana hiyo zawadi!

Mfano mzuri ni ile jackpot ya Jumatano zawadi ilikuwa inasoma zaidi ya bilioni moja ila wakatokea washindi sita! Ikabidi watu sita wagawane hiyo bilioni moja na ushee!
 
Unalazimisha nisome kitu nilichokielewa? Tuanze kwanza una umri gani?
una uhakika uko TIMAMU lakini?... maana, uliposema watu wamenidi kila kitu, nikajua kabisa neno timamu hujalisoma wala kulielewa,....by the way hauko timamu 🚮🚮🚮
Ila endelea kubet, utatoboa tu!...komaaa
 
Ninachojua jackpot mnagawana yaani washindi mkiwa wengi.
 
Kuna tofauti kati ya 14/17 na 14/14.

Aliyepata mechi 14 kati ya 17 ndo kapata mgawo wake wa bonus sh mil 4, lakini hiyo 400 waliyoweka kwa timu 14 means kwenye 17 unachagua zako 14 zilizobaki huchezi na unapata hizo 14 zako (14/14 mil 400)
 
Kuna tofauti kati ya 14/17 na 14/14.

Aliyepata mechi 14 kati ya 17 ndo kapata mgawo wake wa bonus sh mil 4, lakini hiyo 400 waliyoweka kwa timu 14 means kwenye 17 unachagua zako 14 zilizobaki huchezi na unapata hizo 14 zako (14/14 mil 400)
YES MKUU KUNA JACKPOT YA TIMU 14 PEKEE UKISHINDA ZOTE PEKE YAKO MILIONI 400 MKIIWA WENGI MNAGAWANA
 
Back
Top Bottom