Niezeke bati la kiwanda gani kati ya Alaf na Sunshare?

Niezeke bati la kiwanda gani kati ya Alaf na Sunshare?

Alaf miaka minne mingi yanachuja tu.

kile kilichoandikwa miaka 10 ni lugha za biashara tu. Wanajua huwezi kuwafata ni usumbufu tu
Sio kweli nimeezeka kwa bati za ALAF toka mwaka 1994 bado bati zina ubora wa hali ya juu hazijaweka kutu wala kufubaa na kupauka.
Pia nimepaua kwa ALAF Mjengo wa pili toka mwaka 2002 hadi leo hii paa langu ni bora halija Pauka wala kufubaa.
 
Sio lweli nomeezeka kwa bati xa ALAF toka mwaka 1994 bado bati zina u ora wa hali ya juu hazijaweka kutu wala kufubaa na kupauka.
Pia nimepaua kwa ALAF Mjengo wa pili tika mwaka 2002 hadi leo hii paa langu ni bora halika Paula wala kufubaa.
Mkuu sema ukweli ndugu yangu au wewe ndio Mwenye Hisa na ALAF kiasi unasema uongo??

Bati la 1994 halijafubaa wala kuweka Kutu?? Do you know how many years past??🤣🤣
 
Mkuu sema ukweli ndugu yangu au wewe ndio Mwenye Hisa na ALAF kiasi unasema uongo??

Bati la 1994 halijafubaa wala kuweka Kutu?? Do you know how many years past??🤣🤣
Mkuu sina sababu ya kudanganya kwani naphtali faida gani nijikudanganya
Mkuu sema ukweli ndugu yangu au wewe ndio Mwenye Hisa na ALAF kiasi unasema uongo??

Bati la 1994 halijafubaa wala kuweka Kutu?? Do you know how many years past??🤣🤣
Mkuu huo ndo ukweli sina sababu ya kudanganya. Sina maslahi yoyote ALAF labda nina fanya kazi hapo au nina ndugu au hata rafiki anaefanya kazi hapo hapana .Nilicho andika ni ukweli kuhusu ninavyo fahamu ubora wa bati za ALAF
 
Mkuu sina sababu ya kudanganya kwani naphtali faida gani nijikudanganya

Mkuu huo ndo ukweli sina sababu ya kudanganya. Sina maslahi yoyote ALAF labda nina fanya kazi hapo au nina ndugu au hata rafiki anaefanya kazi hapo hapana .Nilicho andika ni ukweli kuhusu ninavyo fahamu ubora wa bati za ALAF
weka photo hilo paa
 
Mtaalamu Wa Finishing kali zenye viwango vya juu vya ubora ....nipo DSM na mikoani nafika

Tunashughulika na Yafuatayo

[emoji3502] UREMBO WA KISASA

[emoji3502]PLASTA ZA KISASA

[emoji3502]SKIMING NA RANGI

[emoji3502]TILES

[emoji3502]USIMAMIZI WA KAZI

[emoji3502]TUPO TEMEKE

[emoji830]CONT. [emoji336]0789005562

Kwa bei ya kizalendo nitafanya nyumba yako ipendeze na ivutie kwa kazi Nzuri

Na kwa sasa tuna offer

Dirisha Tsh 35,000

Kona Tsh 35,000

Nguzo Tsh 40,000

Mlango Tsh 30,000

Dining (Arch) 80,000

Arch ya nje Tsh 20,000

Skating nzima Tsh 2,000,00

Nipigie kwa namba hii 0789005562View attachment 2117514View attachment 2117516View attachment 2117517View attachment 2117513View attachment 2117515View attachment 2117519View attachment 2117521View attachment 2117518View attachment 2117520
Ungeanzisha uzi basi, afu uweke picha kadhaa za vitu ulivyokamilisha
 
Mabati yalichukuliwa kiwandani ALAF
Ukichukua bati kiwandani ALAF hakikisha unafanya escort mwenyewe mpaka site na wakati wa kupaua uwe hapo hapo ukikwepesha macho kidogo tu watu wanaingia nayo buguruni wanabadilisha faster unakua umepigwa
 
Ningeonapo kapicha ka nyumba iliyopauliwa kwa mtindo huo ningeweza kuhamasika zaidi,nina nyumba ya kupaua nakusanya nguvu

IMG-20220430-WA0034.jpg


IMG-20220430-WA0035.jpg


IMG-20220430-WA0036.jpg


IMG-20220430-WA0038.jpg


IMG-20220430-WA0032.jpg
 
Nenda kachukue sunshare.Kwanza wana vipimo vya huakika wanapima uber sawa rangi na uimara wa bati.Alaf ni jina tu lakini bati zao ni za kawaida sana.kachukue gauge 30 pale sunshare huto juta.
Hilo jina limetokana na nini?
 
najua ALAF na SUNSHARE hazipauki lakini siwezi nunua bati moja elfu 40 ni bora hiyo pesa nifanyie finishing ya maana ndani.
 
Naomba nitoe mchango wangu kutokana na nilichojifunza kwa muda mfupi kwenye hii industry ya roofing.

Kwanza nisema watu wengi kila siku wanajenga au kufanya biashara hizi lakini kuna mahali wanafeli ku grasp taarifa sahihi za kitaalam.

Nitazungumzia viwanda nilivyotembelea Alaf, Sunshare, Bati Bomba na kingine pale Tabata..

Gauge za mabati hutofautiana kulingana na unene au thickness ya bati, G30 inakadiriwa kuwa na thickness ya 0.25mm na G28 ni 0.35mm. This is techinical diferences. Na pia kuna chemical diferences lakini karibu zote zinafanana maana zimeundwa na Aluminium na Zinc ktk ratio tofauti tofauti. Zinc na Aluminium ndio properties zinazozui bati kuota kutu kama ikiform zinc oxide au Aluminium Oxide.

Matumizi ya Gauge ktk nyumba.

Kama mleta mada alivyouliza nini tofauti ya matumizi ya bati G28 dhidi ya G30.

1. Hutegemea na mahitaji ya mjengaji, mfano serikali inayojenga majengo makubwa kama kiwanda, godauni, shule au hospitali hutumia bati zenye thickness kubwa kutokana na umuhimu wa jengo lenyewe tofauti na mtu binafsi anayejenga nyumba ya vyumba vitatu.

2. Uimara wa nyumba, msingi na teknolojia ya ujenzi. Hapa tunaona kuwa nyumba kubwa inahitaji mabati mengi zaidi. Lakini pia kama nyumba imejengwa na Fundi Maico yatarajiwa viwango vyake vya uimara( strength) ya msingi na ukuta vitakuwa si mujarabu hivyo kuezeka nyumba hii kwa G28 inaweza kupeleka uzito mkubwa unaoweza kuhatarisha maisha ya nyumba yako. Vile vile kama hali ya hewa ya udongo, maji kutwama, mmomonyoko n.k vyaweza kupelekea nyumba kutitia.

Hii ni muhimu kwa sababu Bando la bati 16 , G28 lina karibu uzito wa kilo 92 wakati bando la bati 16 G30 lina uzito wa takribani kilo 50. Kwahiyo nyumba kubwa kama shule, godauni, kanisa au hospitali utajenga kwa bando ngapi na huo msingi na ardhi vitahimili hizo tani za uzito wa paa??

3. Teknolojia ya uezekaji. Hii inaenda sambamba na ukubwa wa jengo. Nyumba zetu hizi kenchi hadi kenchi ni mita moja tu au chini ya hapo. Shule na kanisa au msikiti vipimo ni vikubwa zaidi so yafaa G28.


Kuhusu Bei za Mabati kutofautiana.


Katika uchunguzi wangu nilifikia hitimisho kuwa hakuna tofauti kubwa ktk bei na utofauti wa bei haumanishi yenye bei kubwa ni imara na bora zaidi. Fuatana nami:


Wauzaji wengi watakueleza kuhusu Gauge ya bati, rangi, na urefu na bei kamwe hawakwambii upana wa bati.

Mfano. Kiwanda cha tabata bati la G30. Migongo mipana( msauzi) urefu futi 10 linauzwa elfu 30. Bati hilo hilo Kiwanda cha Bati Bomba wanauza elfu 28,500. Lakini ni hivi upana kwa Tabata ni 750mm wakati BatiBomba ni 90mm. Vivyo hivyo Sunshare bati zao upana ni 870mm na wanauza elfu 34,500 kwa bati hilo hilo la urefu futi 10, G30 na rangi ile ile.

Kwa G28 Batibomba wanauza futi 10 migongo mipana kwa 34500 wakati ALAF wanauza takriban 55,500. Unaweza kudhani Alaf wanauza bei kubwa sana lakini ALAF bati zao upana ni 1220mm wakati Batibomba ni 900mm. Hapa utaona kuna tofauti kubwa sana. Uki converge hizi factors kwa pamoja utakuta wote bei karibu sawa.

Mfano huo huo unaenda kwa Sunshare na Tabata.
So utahitaji kununua mabati machache ALAF a utahitaji mabati mengi Sunshare.

Jambo lingine linaloweza kuchangia utofauti wa Bei( usihusishwe na ubora au uimara) ni miundo mbinu ya uzalishaji mali pamoja na rasilimali watu.

Mfano. ALAF wana majengo mazuri ya kisasa ya kibiashara full kiyoyozi na ukifika pale kama uko nyumbani au ofisi ya CAG Kichere. Wakati ukifika Tabata na Batibomba joto na vumbi mwendo mdundo wanazalisha kwenye magodown hapo hapo ndio wateja wanachukulia mizigo yao. Hawa watu hawawezi kuchaji bei sawa. Lazima bei za pango na mandhari mazuri uyalipie. Hivyo hivyo kwa Makampuni mengine.

Ushindani wa kibiashara: makampuni mengine nje ya ALAF ni mapya na mageni. Hivyo wanaunafuu kidogo kutokana na mahitaji ya kujitangaza na kujitanua. ALAF tayari ni mkongwe wajenzi wa viwanda na serikali inachukua mizigo mikubwa kwake. Hana shida na hizo milioni zako 2,3, 4, 5...


Kuhusu Malighafi

Wote wananunua kwa supplier wanaofanana. Aidha South afrika au China na india. Na wote mali zao huingizwa zikiwa tayari zimeshachanganywa materials na Rangi. Kazi yao hapa Dar ni kukata na kukunja muundo unaotaka IT4, IT5, Versatile, Romantile....etc.

NB: mimi sio Injinia wa ujenzi wala sina any formal profession kwenye industry hii. Hii ni kutokana na elimu ya hapa na pale niliyodanya mimi mwenyewe kwa kuona, kuuliza, kushika na kusikia viwandani.

Penye makosa/ mapungufu wataalam karubuni kurekebisha.

Bro should i have your number tafadhali
 
Back
Top Bottom