Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Ahahahaha....wote wanakikuta majasusi!? 😂😂😂.
Ila she is strong kwakwel. Kwakwel na declare interest leo kwamba Nifah Ume qualify kuwa mleta ubuyu mwenye quality unbiased standard..unoko wa watu unatuletea na wakwako umetuwekea, tuseme nini tena?
Wa kwake huo sio unoko maana hajasema sababu.
Bila shaka tatizo lipo kwake.
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Aloo, nimesahau jina lako moja ila la pili ni Kimaro na umeshawahi nitumia hela Kwa maelekezo ya the Bold. He is a good man. Mengine tuyaache kama yalivyo. Kutofautina ni jambo la kawaida
 
ukisikia kenge anapiga kelele jua amefinywa sawasawa. Mwamba ukute hata alishamsahau dada yetu ila dada yetu bado anamkumbuka tangu August huko, hapo ndio utajua aliyeachwa ni nani
Ila watu bhana...

Nifah ameamua kuandika sababu yeye ndiyo yupo active JF kwa sasa kuliko jamaa...na amekuwa akiulizwa maswali mengi kuhusiana na mahusiano yake na The Bold.. Na aliahidi ataleta uzi kabla ya mwaka kuisha au mwanzo wa mwaka( 2024) ataeleza kila kitu....

Sasa kosa lake hapo ni nini?

Wanaume acheni kujihesabia haki kwenye Mahusiano....
 
Back
Top Bottom