Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nimeenda kufungua banda la kuku nmerudi uzi unatembea hivi....duuuuh Nifah kweli kiboko

Yani vile ulikuwa unaleta habari za ma celeb na ubuyu pambeee bs huu uzi lazma wajuba wafunguke sana ya mioyoni mwao...!!

Leo utakula sana vichambo kutoka kwa vibungo na feminist yani wewe na dada ASHA_DII wa jamii ya twitter mnamaliza mwka mkiwa

Kwenye flow inayofanana

Sent from Hisense Smart Tv
Bwana eeeh? 🤣🤣🤣
Uzuri muda umepita niko sawa hivyo nawamudu.
Binadamu wana mengi, huwezi kuwazuia kusema.
 
Mimi kama Muhuyul wa Six flying dragon jamaa hajawahi kufocous na mademu zaidi ya kazi yake ya Ugeneral na akafanikiwa haswa , mwengine ni General Ohyi(Oi) wa kwenye Jumong tokea ateswe na mapenzi kizembe jamaa hakutamani kupenda tena zaidi ya kufocous na goals zake na akawa mtu mbadi sana na hawakula nyetoh kama dronedrake ..

Lee Min ho shombe shombe analeta sana mapenzi kwenye kazi , hayo mambo nimepiga chuma tatu Kali kama miongoni mwa adui wangu mkuu ,ukitaka uone nimepigaje rejea katika Uzi wetu wa Wakorea Ile video ya jamaa wa Joseon Gunman anavyopiga chuma kwa hasira utapata picha halisi..
Oya adriz ile joseon gun man ni 🔥🔥, eti ana piga chuma kwa hasira😂🤣
 
Nimeenda kufungua banda la kuku nmerudi uzi unatembea hivi....duuuuh Nifah kweli kiboko

Yani vile ulikuwa unaleta habari za ma celeb na ubuyu pambeee bs huu uzi lazma wajuba wafunguke sana ya mioyoni mwao...!!

Leo utakula sana vichambo kutoka kwa vibungo na feminist yani wewe na dada ASHA_DII wa jamii ya twitter mnamaliza mwka mkiwa

Kwenye flow inayofanana

Sent from Hisense Smart Tv
Kwamba "Yowe halichagui umri" [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Break up: mwezi August.

Press release: kuelekea sikukuu ya mwaka mpya (January) 😄

Mleta mada hebu subiri kwanza January iishe afu ndipo utukumbushe hii 'public notice' yako. Kwasasa tunaipuuza kwanza. 😎

-Kaveli-
Ungeipuuza usingechangia 🤣🤣🤣

Ushauri nakupa, ukitokea kuachana na mwenzi wako jipe muda kabla ya kusema. Hakikisha umekaa sawa na kusahau.

Hii inakupa uhakika wa unachokifanya kuwa ni sahihi, na pia unakuwa na uwezo wa kulimudu kwa hekima.

Si unaona mimi? Sina makasiriko.
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Sasa nafasi ipo wazi, ngoja tuanze kutuma application mapema 2024 ni mwaka wa kuoa
 
Back
Top Bottom