Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Mahusiano yakivunjika yanaumiza, hata useme siumii kiukweli ni kuwa wahusika wanaumia.Mume na mke wenye watoto huachana na maisha yanaendelea.
Hiyo Galaxy ya mapenzi ukiishi salama mshukuru sana Mungu, binafsi ni muathirika wa hilo ila nataka ujue kuna maisha nje ya hiyo galaxy. Karibu ukaperani, hii timu inasajili kila uchao. Pole
 
Nifah your brain work is next level. Salute!

Ninayo Imani ya kutosha kuamini kuwa msingi wa mgogoro ama tofauti za penzi lenu ni penzi lenu wenyewe. Kimombo niseme: methodological implementation and presentation of your love life. Hili ni hitimisho nimeikia baada ya kusoma maandiko yako kwenye sakata hili.

Imani yangu kwenu ni kuwa ikitokea mkaketi chini na kuamua kutanzua tofauti hizo, ikiwapendeza msione shida kupandisha daraja mahusiano yenu. Maana mnachopitia wakati huu ni misukosuko wa kawaida kabisa kwenye maisha ya mapenzi na mahusiano.

Hivyo wala usiwaze sana, wala usiumie moyo sana. Maana that's how the love pendulum swing on its axis

Best wishes
Oh, thank you.
Happy New Year
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Mtoto je?
Kwa maoni yangu usingelisema ungeacha tuu yapite! Watu wa hapa watakukosesha amani sana!
 
Back
Top Bottom