Nifanye kazi gani nipate laki tano kwa siku 30?

Nifanye kazi gani nipate laki tano kwa siku 30?

Kuna nyuzi zinatrend jukwaa la Jamii Intelligence mfano utakuta uzi unasema 'Wadudu kumi hatari duniani' au 'Magonjwa kumi hatari duniani' au 'Watu 10 warefu duniani'

Zile nyuzi wanazitoa online kutoka kwenye website ya Listverse. Now Listverse hawawezi kuandika kila kitu wao hivyo wanaajiri freelancers wa kuandika maudhui yao.

Wanalipa Dola 100 wakikubali utakachowaandikia. Isipokua wanalipa kwa kutumia Paypal ambayo kwa Tz ukiwa na akaunti ya Paypal hautaweza kupokea pesa hivyo hakuna mtu aliye Tz ataweza kulipwa.

Websites ambazo hazitumii Paypal hulipa pesa kidogo. Mfano Mysterious world wanalipa dola 25 hivyo tafuta website itakayokuridhisha, fanya nao kazi. Fuatisha masharti yao ya uandishi ukikubaliwa article yako wanakulipa.

Picha ulipwaji wake utategemea na unapoupload na camera yako pia. Mfano picha za smartphone huwezi kuziweka Getty image au Stock photo ukatarajia pesa ndefu.

Pia malipo ni tofauti na website. Mfano sehemu nyingine watakulipa kadri watu wanavyodownload picha yako na sehemu nyingine watakulipa hapo hapo ila watu wakidownload picha ulizoweka haupati tena kitu.
Asante
 
Njoo pm sinamfanyakazi wa ndani... Ntakupa kila kitu na mwisho wa mwezi nakupa 500k
 
Kwa hyo upo ladhi kuuza ila kinachokukela ww ni hatufu ya beberu tu,
 
Tafuta websites au blogs ambazo unaweza kuwaandikia na ukalipwa. Mshahara unaanzia dola 25 mpaka dola 500 kutegemea na umashuhuri wa website husika.

Kama upo Tz ni tatizo kwakua kinachotukwamisha ni Paypal haipo supported Tz.

Sasa hivi Hovatek wanatafuta waandaaji maudhui, wacheki.

Sites zingine ni za kuupload video au picha nazo zinalipa, mshahara unaanzia dola 5 nafikiri dola 50 ni kiwango cha juu zaidi.
Hii ya Ku upload picha na video Ni IPI mkuu!!?
 
Hii ya Ku upload picha na video Ni IPI mkuu!!?
Youtube, Dailymotion unaupload video na nafikiri ndiyo sites maarufu.

Stock photo, Getty Image unaupload picha.

Ukicheki mtandaoni utakuta hadi websites unazoweza kuweka picha za simu.
 
Habari zenu wadau
Pitia uzi wangu ulopita wa kujenga kwa m. 3, ha ha haikutosha badala yake nilitumia kama m. 6 nyumba ya vyumba viwili na choo imesimama na bati imegongewa sasa tatizo milango na madirisha na plasta, kwa sababu mimi ni mtumishi wa umma nategemea kuchukua likizo mwezi ujao, hapa nawaza nifanye kazi gani nipate angalau laki tano tu niweke dirisha nyumba yangu??

Ushauri pulizi
JF kwa watu kujikuza hamjambo
 
Una mtaji Wa shi ngap nikusaidie
 
Back
Top Bottom