nilifahamiana na huyu kaka miaka kumi na mbili iliyopita, alisha propose mara tatu na zote sikukubali,na pia nimemfanyia vituko vingi sana ili akae mbali na mimi, miezi kama mitatu imepita siku moja nikanza kumuwaza in a positive way,nikakumbuka mazuri yake na kutamani niwe nae, uwezi amini the same day nawaza akanipigia simu nikaongea nae vizuri kwa utulivu mwingi, hakuamini kama ni mimi na usiku wa siku hiyo akanipigia tena na kupropose kwa mara ya nne, nilimkubalia, tupo kwenye mahusiano sasa hivi yamekolea balaaaa, ila mwenzangu ana wasi wasi mwingi kwamba naweza kumwaga muda wowote, na anataka anijaze mimba kabla sijabadili mawazo,sipo tayari kubeba mimba kabla ya ndoa
nifanye nini ili aniamini nampenda kwa dhati na sipo tayari kumpoteza. ili asubiri tufunge ndoa kwanza ndo nipate ujauzito