Nifanye nini ili kesho ninayoiwaza isiwe ya majuto?

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,236
Reaction score
7,583
Habari wakuu,
Hopefully wengi wenu mpo poa kabisa, Ikiwa basi una itilafu yoyote ya kiafya basi zingatia tiba na Mungu akufanyie wepesi ukae poa kabisa.

As you know mimi kijana wenu sasa naelekea kutimiza 23yrs mwaka huu, Sasa lengo la uzi huu ni kwa sababu nafahamu humu kuna watu wengi sana ambao wameshapita umri niliopo mimi kitambo sana, na kama ilivyo kawaida yangu watu hao mimi ni halali yangu na siwezi kuwaacha wakafa na madini ya chumvi walizokula, Me nawaambiaje wakuu ni hivi "Hayo madini mimi kijana wenu _Flames mtanipa tu" sio kama nipendavyo mimi tu bali mpendavyo ninyi pia.

Mimi ni kijana ambae sijabahatika kupata elimu kivile ila nashuku Mungu basi nilifika hata 4M-4 ambapo vitabu vya Passed like a shadow na Three suitors one husband vimenisaidia ku-mprove my english na sasa kidogo naweza nikawasiliana na mteja wangu kutoka US tukaelewana.

Baada ya kumaliza tu o-Level nikajikuta jiji la Dar na hadi sasa ndo napambana hapa, Jua la Dar limehusika kunipa ujasiri wa haya maisha ambayo nilikuwa nikiyaogopa hadi sasa najitegemea na maisha yangu kwa harakati zangu hizi za ku-force... Nawish sana nipate pesa nyingi niwafanye wazazi wangu nao wa-feel ile moment ya kuishi kwenye nyumba zao ila kiuwezo bado sana nilichokiweza basi ni kuhakikisha sikukuu ya Chrismas miamala inasoma kwenye simu zao ili wapate walau kula pilau na nyama nyingi na kinywaji pembeni na Wakajibu "Barikiwa sana mwanangu"

Okay twende fasta, Mimi ni yule kijana ambae sina circle ya marafiki, Sina dem kwa sasa, Sina mtoto wala sina ninachokiwaza akilini kwangu zaidi ya Hela na Future yangu... Kwasasa sina shida ndogondogo kama kula wala kuvaa, wala kulala, wala kutoka out. Ni kijana ambae nipo real all the time kwani nikisema naenda Shoppers pale mlimani city basi sio kununua ice-cream kama vijana wenzangu wengi ninaowakuta hapo bali nitanunua Sukari,Unga,Mchele,Tomatos,Mikate n.k kwaajili ya matumizi ya gheto kwangu. Mimi ni kijana ambae nikikosa chini 1m kwa acc na 50k kwenye wallet kama pocket money napungua mwili kutokana na stress ana lack of happiness... Napenda uhakika kinoma noma, Sipendi vipengele that's why hata nikidawa napambana kulipa deni la mtu fasta nimalize niwaze mambo mengine.

Furaha yangu inashindwa kuwa full kwa sababu ya kesho yangu, Kesho inaninyima furaha natamani ningeiona ili nijiandae, Sipendi familia yangu ije kuwa na baba ambae hajajipanga, Sipendi kuja kugombania daladala na mvi...

Nimeeleza hapo juu ili mtu ambae atanishauri anipe ushauri kuendana na mimi nilivyo basi nini cha kufanya... Nishauri nini cha kufanya ili kesho ninayoiwaza kwa akili yangu isiwe ya majuto.

Nishauri kwa umri wangu huo ni watu wa aina ganinnatakiwa kuwa nao close, Nishauri ni muda gani ukifika nioe, Nishauri aina za marafiki, Nishauri chochote cha kufanya kwa wakati huu, Nishauri ni tabia gani niachane nazo, Nishauri kutokana na mimi kutokuwa na elimu ya Dunia au CV's za kuniwezesha basi nipambanie kitu gani zaidi ili niweke uhakika wa kesho yangu zaidi, Naomba usipite bila kunishauri chochote wewe kama Kaka,Baba,Dada,Mama n.k

Me Love Goes To You ❤️
 
Mipango ni muhimu mkuu, Panga kisha omba kibali... Mungu anakutengenezea njia na wepesi kufanikisha
Sipingi ila minishapanga mengi lakin mtekelezaji ni yeye.

Hivyo basi ukimaliza kupanga mwambie hivi "MIMI NDIMI MTUMISHI WAKO NITENDEWE UNAVOTAKA".

Utakuja nishukuru baadae🤝
 
Sipingi ila minishapanga mengi lakin mtekelezaji ni yeye
Hivyo basi ukimaliza kupanga mwambie hivi "MIMI NDIMI MTUMISHI WAKO NITENDEWE UNAVOTAKA"
Utakuja nishukuru baadae🤝
shukran mkuu, na pole kama unavyopanga inaenda sivyo.
 
Umri mzuri huo wa kuwa na focus nzuri ya shule, kazi au business kama unayo, ukiweza usijiingize kwenye sigara, madawa au malaya, tunza afya yako ndio mtaji wako
 
shukran sana mkuu
 
spirit yako ni kali sana dogo,endelea nayo hivyo hivyo as ndiyo iliyokifikisha hapo! Endelea hivyo hivyo,ishu za mahusiano na marafiki zitakuja zenyewe tu! Time will tell and allow! Keep it on
 
nashukuru sana mkuu, ila sometimes nahisi kama isijekuwa kutokujichanganya kukanikosesha connections maybe
 
Dogo umri wko bado sana kipindi nipo age yko nlikua nakesha kwenye PS usiku kutwa na kuenda viwanja na totoz kibao ila baada ya kupata umri wa umakamo akili ilipata mageuzi wenyewe Katika kujipambania ,,usiwe na stress ukaja ukaforce maisha alafu ukaishia pabaya chamsingi Fanya Kazi ndogondogo maana maisha ni kama curve yanapanda kushuka
Habari wakuu,
Hopefully wengi wenu mpo poa kabisa, Ikiwa basi una itilafu yoyote ya kiafya basi zingatia tiba na Mungu akufanyie wepesi ukae poa kabisa.

As you know mimi kijana wenu sasa naelekea kutimiza 23yrs mwaka huu, Sasa lengo la uzi huu ni kwa sababu nafahamu humu kuna watu wengi sana ambao wameshapita umri niliopo mimi kitambo sana, na kama ilivyo kawaida yangu watu hao mimi ni halali yangu na siwezi kuwaacha wakafa na madini ya chumvi walizokula, Me nawaambiaje wakuu ni hivi "Hayo madini mimi kijana wenu _Flames mtanipa tu" sio kama nipendavyo mimi tu bali mpendavyo ninyi pia.

Mimi ni kijana ambae sijabahatika kupata elimu kivile ila nashuku Mungu basi nilifika hata 4M-4 ambapo vitabu vya Passed like a shadow na Three suitors one husband vimenisaidia ku-mprove my english na sasa kidogo naweza nikawasiliana na mteja wangu kutoka US tukaelewana.

Baada ya kumaliza tu o-Level nikajikuta jiji la Dar na hadi sasa ndo napambana hapa, Jua la Dar limehusika kunipa ujasiri wa haya maisha ambayo nilikuwa nikiyaogopa hadi sasa najitegemea na maisha yangu kwa harakati zangu hizi za ku-force... Nawish sana nipate pesa nyingi niwafanye wazazi wangu nao wa-feel ile moment ya kuishi kwenye nyumba zao ila kiuwezo bado sana nilichokiweza basi ni kuhakikisha sikukuu ya Chrismas miamala inasoma kwenye simu zao ili wapate walau kula pilau na nyama nyingi na kinywaji pembeni na Wakajibu "Barikiwa sana mwanangu"

Okay twende fasta, Mimi ni yule kijana ambae sina circle ya marafiki, Sina dem kwa sasa, Sina mtoto wala sina ninachokiwaza akilini kwangu zaidi ya Hela na Future yangu... Kwasasa sina shida ndogondogo kama kula wala kuvaa, wala kulala, wala kutoka out. Ni kijana ambae nipo real all the time kwani nikisema naenda Shoppers pale mlimani city basi sio kununua ice-cream kama vijana wenzangu wengi ninaowakuta hapo bali nitanunua Sukari,Unga,Mchele,Tomatos,Mikate n.k kwaajili ya matumizi ya gheto kwangu. Mimi ni kijana ambae nikikosa chini 1m kwa acc na 50k kwenye wallet kama pocket money napungua mwili kutokana na stress ana lack of happiness... Napenda uhakika kinoma noma, Sipendi vipengele that's why hata nikidawa napambana kulipa deni la mtu fasta nimalize niwaze mambo mengine.

Furaha yangu inashindwa kuwa full kwa sababu ya kesho yangu, Kesho inaninyima furaha natamani ningeiona ili nijiandae, Sipendi familia yangu ije kuwa na baba ambae hajajipanga, Sipendi kuja kugombania daladala na mvi...

Nimeeleza hapo juu ili mtu ambae atanishauri anipe ushauri kuendana na mimi nilivyo basi nini cha kufanya... Nishauri nini cha kufanya ili kesho ninayoiwaza kwa akili yangu isiwe ya majuto.

Nishauri kwa umri wangu huo ni watu wa aina ganinnatakiwa kuwa nao close, Nishauri ni muda gani ukifika nioe, Nishauri aina za marafiki, Nishauri chochote cha kufanya kwa wakati huu, Nishauri ni tabia gani niachane nazo, Nishauri kutokana na mimi kutokuwa na elimu ya Dunia au CV's za kuniwezesha basi nipambanie kitu gani zaidi ili niweke uhakika wa kesho yangu zaidi, Naomba usipite bila kunishauri chochote wewe kama Kaka,Baba,Dada,Mama n.k

Me Love Goes To You ❤️
 
Mwaka huu nagonga decades 3.4 af mpaka sasahivi sielewi life linavyoniendea. Kuna muda natafakari naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kwenye maisha yangu, mimi sio wa kupoteza direction kiasi hiki! Hivi kweli mimi wa kufokewa na mtoto wa 25!? Kisa tu ameniajiri.

Wakuu hili life acheni tu. Naona kabisa kuna sehemu nilikosea sana kuyaseti maisha yangu, na leo hii haya ndo matokeo ninayoyapata.

Nakupongeza mdogo wangu kwa kujitambua mapema [emoji122]
 
Back
Top Bottom