Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Sababu ilikua nini, ama walikua wanachafua mazingira hawasafishi maganda ya viazi aaubuhi??
Kwahiyo pale amekuja mpika chipsi mwingine, ama Daruso bar ilishafungwa kabisa??
Pale daruso kulikuwa na jiko ambapo vyakula vilikuwa vikiuzwa,Duka kubwa la vitu pamoja na uuzwaji wa vinjwaji!!! Bar nzima including na sehemu ya chips na chakula ilikuwa ni miliki ya mtu binafsi,ilifikia hatua walikuwa wanauza kweli kweli mpaka ikatokea idadi ya wanafunzi wanaoenda kula kwenye zile cafeteria kubwa idadi ikapungua, ndipo wakumuundia zengwe kwamba ile bar inachangia uvunjifu wa amani pindi wanafunzi wanapolewa hivyo akatakiwa aifunge, kwa sasa cjajua kama imefunguliwa mkuu, ni mda sijapita mazingira hayo
 
Zipo biashara za kupata laki 2 kwa wiki lkn sio kwa mtaji wa m 1..

Na ukilazimisha saana basi hela yako itapotea huku unaiona,,,.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda, commitment, determination, goal setting(unataka kufikia nini, lini na vipi), resources, location, market research na partner ambaye mna same vision and commitment, above all, Love what you do, usifanye kwa ajili ya watu au kwa ajili ya shida.

Nimeyachukua aya maneno yako nayatengenezea frame kabisa nabandika chumbani kwangu ili kila siku niwe nayasoma

Sentensi moja tu,iliyojaa elimu mpaka ya chuo kikuu

Asante sana mkuu,hapa umemaliza kila kitu.
 
Zipo biashara za kupata laki 2 kwa wiki lkn sio kwa mtaji wa m 1..

Na ukilazimisha saana basi hela yako itapotea huku unaiona,,,.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu fafanua zaidi ni biashara zipi hizo. tatizo ninaliona kwenye huu uzi ni kutazama mtaji zaidi ya fursa yenyewe na uwezekano wa kufikia hiyo target
 

Mkuu nakushauri Fanya biashara ya supply gas (oryx or mihan).
Kama huna gari ya kusambazia unaweza kuingia mkataba nawenye gari (Suzuki carry) kwa siku 20,000. Uwe na driver mzuri, wages 15,000 kwa siku. Mafuta kwa siku 30,000.
Nunua mitungi 6kg 30 kila kampuni, na 15kg 10 kila kampuni. Faida ya kila 6kg ni 1000 na 15kg ni 3,000. Kama upo dar uwezo wa kuuza 6kg kwa siku kwa wastan ni 60 na kubwa ni 20. Kwa dar hakuna msambazaji anaeweza kumudu soko la dar, ni kubwa sana. 60 x 1,000 + 20 x 3,000 = 120,000 - 65,000 (fixed expenses) = 55,000 per day. Some time biashara ina fluctuate lakini hukosi faida ya 200,000 kwa wiki. Am in the same business eneo langu ni ubungo, kimara, mbezi, goba na kibamba. Segemu kama Tabata, g'la mboto, chanika, masaki, mikocheni, bunju, buza, Temeke, kigamboni, Mbagala, Vikindu, kinyarezi, kitunda nk. Soko ni kubwa sana. Ufahamu wa kutumia nishati ya gas umekuwa mkubwa sana. Demand ya supply ni kubwa sana.
 
ili wazo ni solid sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
inategemea na mahali ulipo pana fursa gani,,
mfano dogo langu anaenda kwa wavuvi wa samaki ananua wale sangara wakubwa sana then anatoa kitu flani kwenye yule samaki kinaitwa bondo,,

iilo bondo anauza kwa wachina mpaka laki nne,
huyo samaki ana mnunua laki mpaka laki na nusu
akishatoa bonndo samaki anamuuza fasta kwa watu wa hoteli au migahawa,,,

sasa hapo ulipo ww kuna fursa zipi,,kilimo dhahabu,,mifugo,,utalii,,,
mkuu fafanua zaidi ni biashara zipi hizo. tatizo ninaliona kwenye huu uzi ni kutazama mtaji zaidi ya fursa yenyewe na uwezekano wa kufikia hiyo target
 
Talking from experience, hiyo biashara inalipa nilishaifanya japo hiyo million tatu kidogo nina mashaka nayo, Nilikuwa napata 20 elfu kila siku na hiyo ni minimum profit
 
Ongeza mtaji ufike bei ya kununua kagari chenye engine ndogo, kisha kasajili uber na taxify..

Utaingiza hiyo hela
 
Kama mtaji ni mdogo jitahidi usijiingize kwenye vitu ambavyo unaweza kukukwepa.
 
Na uko ndo wanapopelejwa kama sio account management [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hahah utasikia kilio muda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…