Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Kijana acha tamaa.

Anza kidogo kidogo,
kuwaza vikubwa wakati hata vidogo huviwezi ni hatari na UTAPOTEA.

Kwa kijana mpya asokua na uzoefu wa biashara.

Kwa huo mtaji wa million Moja,
Faida yake inastahili kua elfu 20-30 kwa wiki.

NB: Hiyo faida (Mapato-Matumizi) ya laki 2 kwa mtaji wa million Moja ni Ndoto.

Vinginevyo unaongelea MAPATO ya laki 2 kwa wiki.

Kiuhalisia,
Kama unataka Faida ya Laki 2 kwa wiki,
Itakubidi uwe na MAUZO yasopungua Millioni 2 kwa wiki.

Sasa,
MAUZO ya million 2 wakati Mtaji wako ni Millioni 1 ni KICHEKESHO CHA MWAKA itakua.

Sent using Jamii Forums mobile app
kama yupo makini hiyo faida anaipata mkuu ukimbana vizuri mfanyakazi
 
Pale udsm kulikuwa na daruso bar, kuna jamaa mmoja alikuwa anauza chipsi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa saba usiku, huyo jamaa kila siku alikuwa anafunga hesabu si chini ya million 2 mpaka 3. Kwaiyo haya mambo yanawezekana ukipata location nzuri, bahati mbaya jamaa walipigwa fitna wakawa awaruhusiwi kuuza pale tena, kwaiyo fitna nayo ni muhimu sana ktk biashara usipozijua utaishia pata loss tu
"KWA SIKU ANAFUNGA MILIONI 2 MPAKA 3,

WASTANI KWA WIKI ANAFUNGA MILIONI 10 MPAKA 15,

KWA MWEZI ANAFUNGA MILIONI 40 MPAKA 60."

JAMANI NDUGU ZANGU WATANZANIA,
TUACHE SHUGHULI ZINGINE ZA KUPOTEZA MUDA,
TWENDENI TUKAUZE CHIPSI DARUSO BAR, UDSM.

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
 
Back
Top Bottom