Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

nimeifanya kwa almosr 2yrs..ikawa inakata sana bas tu unakuw unakaakiba unaongezea..mitumba ukitaja ikulipe anza na bello 4 hv..sio 2 lazima utajikuta umerudi kwenye zero tu..na nenda minada yt uijuayo ww..hapo itakulipa..kuna minada kutoka j3 had jpl
Hii ya mitumba uliifanya kwa mda gani mkuu? au mpaka sasa bado unaifanya.
 
Anza kukopesha kwa riba ya 20% hapo ofisini kwako na ukata huu wa JPM utaanza pata 1m + riba 200k kwa mwezi. Grow the business that can scale out from profit ya 200k per month to 800K as your target. M-PESA shop also will do
Pasipo kuwekeana dhamana yeyote, baadae ni tafrani tu
 
nimewaza sana hili jambo. Ni jambo ambalo linawezekana kabisa. inahitaji kujitoa sana. nimegundua unaweza kuingiza hata kiasi kikubwa zaidi ya hicho. inahitaji ujue namna ya kuweza kuuza. aidha wewe mwenyewe au utafute wasaidizi. hapa kwenye kuuza nazungumzia chochote kile mradi uweze kukiuza na kufikia target hiyo. kuna kitabu ameandika Grant Cardon kinaitwa sell or be sold ni nondo moja nzuri ambayo itakusaidia
 
kitabu chenyewe hiki hapa. sasa najua maswali yatakuja mengi maana sii kila mtu anaamini anaweza kupata maarifa ya kumfaa katika vitabu sasa hapa pia naambatanisha ushuhuda wa mtu ambaye ameweza kufanya hivyo.


INSI BIASHARA YA SAMBUSA ILIVYOBADILISHA MAISHA YANGU NILIANZA NA ELFU KUMI SASA NATENGENEZA ZAIDI YA MILIONI TATU!
Kama ni mhitimu wa masomo ya ualimu hasa wale wenzangu wa masomo ya Arts naamini sina haja ya kukuambia niliyokua nikipitia miaka miwili iliyopita. Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo mwaka 2015 nilikua na matumaini makubwa ya kuajiriwa moja kwa moja nikiamini ualimu ni dili. Lakini haikua hivyo, hata katika shule binafsi ambako niliomba kujitolea nilikosa kabisa hivyo kuamua kurudi nyumbani kusubiria ajira za Serikalini zitangazwe.
Lakini muda ulikua unakimbia na miezi sita ilipita hakukua na cha tangazo la ajira wala nini, nilishachoka kusubiria ajira hivyo nilitaka kutafuta kitu cha kufanya kwa maana ya biashara. Nilikua na mawazo mengi ya biashara lakini tatizo lilikua ni mtaji, kila wazo lilikua linahitaji mtaji si chini ya milioni moja, sikua na hata Shilingi ndani hivyo mawazo yote mazuri yalikufa kabla ya kuanza.
Mimi najua kupika na siku moja nilikua napika Sambusa za nyama, nilikua napika kwajili ya kula nyumbani. Sambusa zangu ni nzuri sana na watu huzipenda. Hivyo siku moja wakati ninapika niliwaza kwanini nisianze biashara ya kupika na kuuza sambusa. Nilipiga mahesabu kwa kuanza nilihitaji mtaji wa kama Shilingi elfu kumi tu, hiyo nisingeikosa lakini bado nilikua na mawazo nikiona kama ni kazi ya kudhalilisha elimu yangu
.
Niliachana na hilo wazo hasa nikifikiria kuwa sitakua nikipata hela ya maana na ajira labda zinakuja. Siku moja nilikua mjini, alikuja mtu anapitisha Sambusa, anauza moja Shilingi mia tano, nilinunua na kuonja hazikua na ladha kabisa, hata sikula nilitupa. Lakini wakati narudi nyumbani lile wazo lilinijia tena, niliona kuna fursa, nikiwaza kama nikiweza kupika sambusa 100 tu kwa siku, kwa bei ya Shilingi mia tano nitapata Shilingi elfu hamsini ukizidisha kwa mwezi ni kama Shilingi milioni moja na nusu.
Baada ya kupiga hayo mahesabu na kuwaza mshahara wa mwalimu ambao hautafiki hata laki sita nilijiona fala kuanza kuwaza watu watanionaje. Sikutaka kumuambia mtu kwani nilijua watanikatisha tamaa, nilikua na kama elfu kumi ndani, nikanunua Unga, nyama na kusaga kisha kutengeneza sambusa, nilitengeneza chache tu. Nikaziweka kwenye kikontena cha plastic, sasa kazi ilikua kwenye kuuza kwani kweli nilikua naona aibu. Nilizipeleka kwenye duka la jirani ilia niuzie.

Jioni hazikuisha, kwetu ni mjini mjini uswahilini hivyo kumechangamka, jioni baada ya kuona hazijaisha nilizisambaza mwenyewe jioni jioni kwenye vijiwe vya kahawa na maeneo mengine. Huwezi kuamini ziliisha na siku hiyo nakumbuka nilitengeneza kama smabusa hamsini hivi na ukipiga faida ilikua inakuja kama elfu kumi na tano. Siokuamini, kesho yake nilitengeneza sambusa mia nazo ziliisha kwani nilikua nazungusha mwenyewe.
Labda niseme na kuwa mwanamke kulinisaidia kwani wateja wengi walikua wanaume na mimi ni muongeaji sana. Baada ya hapo sasa niliamua kufanya hii kama biashara, nilianza kupika sambusa nyingi zaidi na kwakua nilikua na muda ilikua rahisi. Nilitengeneza kama kajiko flani hivi kamkaa kwajaili ya kubebea na kuuza sambusa za moto (nadhani mshawahi kukutana navyo mtaani vinauza sambusa za moto), nikatafuta kijana ambaye alikua akizunguka kuuza Sambusa hasa saa za jioni.

Nilikua nikimlipa Shilingi elfu kumi kwa siku kwa maana kutokana na anavyouza kwa maana kwamba kama ni kimpa sambusa mia atauza kwa kuchukua Shilingi mia kwa kila sambusa. Mambo yaliendelea hivyo mpaka kufikia kuajiri mtu mmoja wa kunisaidia kupika na wengine watatu wa kuuza mtaani. Lakini sikuishia hapo, nilianza kupika Sambusa kwaajili ya migahawa, nilizunguka kuna sehemu ambazo hawapiki Sambusa na kuwa nawapelekea.
Lakini pia nachukua oda za kuwapikia watu binafsi kwaajili ya majumbani ambapo bei inapungua kidogo kwakua huchukua nyingi, pia sasa napika pia kwenye sherehe ambapo nashirikiana na wale wapishi kwa kuwapelekea sambusa zangu. Kwa wengi biashara ya Sambusa huiona kama ndogo na ya kipuuzi lakini sasa nimeajiri watu saba ambao nafanya nao kazi na kwa mwezi mambo yakiwa mazuri naingiza mpaka milioni tatu kama faida.

Niko mbioni kufungua Sambusa Cafee (Nashukuru Kaka Iddi) hapa nitakua nikiuza sambusa za aina mbalimbali lakini pia nauza na Juice ila kitu kikubwa ni Sambusa. Lakini pia nitakua nikiuza Bites nyingine mabazo zinaendana na Sambusa au nyama ya kusaga kama Kababu na Egg Chops. Ni biashara nzuri kama ukiifanya kijanja, kama uko sehemu za mjini kwani pamoja na hali ngumu lakini mtu kutoa mia tano kula Sambusa haoni shida sana.
Mara nyingi nauza sambusa kama Bites na si kama chakula. Mwanzoni vijana niliokua nawatumia nilikua nawalipa kwa siku kutokana na mauzo yao, lakini sasa nawalipa kwa mwezi lakini pia ni kutokana na mauzo yao. Kwamba kama akiuza Sambusa mia anapata elfu kumi, basi mimi nazimtunzia na kwa mwezi namlipa laki tatu, lakini kama hatafikia mauzo aliyopangiwa basi inapungua kutoka katika mshara wake kile ambacho hakukiuza.
Katika Mahoteli, migahawa na sehemu za Mama Lishe, biashara ni asubuhi, huko nawapelekea nao huuza na tunagawana faida. Lakini katika kuzunguka mtaani jioni ndiyo kunakua na biashara kuanzia saa kumi na moja mpaka saa tatu za usiku. Kama unataka kufanya biashara hii usijikite katika sehemu moja changamka na sambaza kila sehemu.

Lakini pia kuna maeneo ya Stend hii ni mchana zaidi, silazima ufanye wewe tafuta vijana, kuna vijana wengi hawana kazi wapo mtaani tu watumie. Mimi kwa sasa suala la kuajiriwa halipo tena nina malengo makubwa ambayo yalianza kidogo kidogo, miaka miwili iliyopita nilikua najua tu kupika Sambusa sasa nimejiajiri kwa sababu ya Sambusa na kumbuka yote haya nilianza na mtaji wa kama elfu kumi tu hivi.
NB; Katika kuanzisha biahsara haijalishi umeanza na mtaji mkubwa kiasi gani bali namna ambavyo unaweza kuuza kitu kidogo ulichonacho na kukipanua kuwa biashara kubwa. Kama uko mtaani au umfanyakazi unataka kufungua biashara na hujui uanzie wapi Kitabu cha “Biahsara50” kitakusaidia kufanya hivyo. Kuna bishara nyingi unaziona kubwa lakini unaweza kuanza kidogo kidogo na nimefundisha katika Kitabu changu.

malizia mambo mengine kwenye hii page

 
nimewaza sana hili jambo. Ni jambo ambalo linawezekana kabisa. inahitaji kujitoa sana. nimegundua unaweza kuingiza hata kiasi kikubwa zaidi ya hicho. inahitaji ujue namna ya kuweza kuuza. aidha wewe mwenyewe au utafute wasaidizi. hapa kwenye kuuza nazungumzia chochote kile mradi uweze kukiuza na kufikia target hiyo. kuna kitabu ameandika Grant Cardon kinaitwa sell or be sold ni nondo moja nzuri ambayo itakusaidia
Hii ishu inawezekana sana, kuna mama ntilie aka mama "kifurushi"( huyu alikuwa anatupimia wali na ugali wa kushiba)mabibo hostel pale alikuwa anauza mpaka laki 3 kwa siku.gharama za uendeshaji kwa siku laki na nusu: mama ntilie yupo vizuri sasa kajenga nyumba nzuri ya kisasa tu mbezi- makabe. Kwaiyo sometym na location katika biashara inachangia sana.
 
Hii ishu inawezekana sana, kuna mama ntilie aka mama "kifurushi"( huyu alikuwa anatupimia wali na ugali wa kushiba)mabibo hostel pale alikuwa anauza mpaka laki 3 kwa siku.gharama za uendeshaji kwa siku laki na nusu: mama ntilie yupo vizuri sasa kajenga nyumba nzuri ya kisasa tu mbezi- makabe. Kwaiyo sometym na location katika biashara inachangia sana.
kweli mkuu kuna mama mmoja alikuwa anatuuzia kokoto na ubuyu pale UDSM sasahivi anasambaza kila chuo amejenga nyumba za maana watoto wako international schools na anapush prado kila siku kusambaza mizigo yake
 
kweli mkuu kuna mama mmoja alikuwa anatuuzia kokoto na ubuyu pale UDSM sasahivi anasambaza kila chuo amejenga nyumba za maana watoto wako international schools na anapush prado kila siku kusambaza mizigo yake
Pale udsm kulikuwa na daruso bar, kuna jamaa mmoja alikuwa anauza chipsi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa saba usiku, huyo jamaa kila siku alikuwa anafunga hesabu si chini ya million 2 mpaka 3. Kwaiyo haya mambo yanawezekana ukipata location nzuri, bahati mbaya jamaa walipigwa fitna wakawa awaruhusiwi kuuza pale tena, kwaiyo fitna nayo ni muhimu sana ktk biashara usipozijua utaishia pata loss tu
 
Pale udsm kulikuwa na daruso bar, kuna jamaa mmoja alikuwa anauza chipsi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa saba usiku, huyo jamaa kila siku alikuwa anafunga hesabu si chini ya million 2 mpaka 3. Kwaiyo haya mambo yanawezekana ukipata location nzuri, bahati mbaya jamaa walipigwa fitna wakawa awaruhusiwi kuuza pale tena, kwaiyo fitna nayo ni muhimu sana ktk biashara usipozijua utaishia pata loss tu
kweli mkuu wenye fursa kubwa fitna nazo zimo. mkuu tusaidie unawezaje kutambua location nzuri?
 
kweli mkuu wenye fursa kubwa fitna nazo zimo. mkuu tusaidie unawezaje kutambua location nzuri?
Mkuu hii inategemea na uhitaji wa bidhaa yako sehemu husika, ndio mana kabla ya kuanzisha kitu flani tuna shauriwa tufanye tafiti za kutosha kuhusu bidhaa na hata itakapouziwa, kuna watu wana mitaji mizuri na biashara nzuri lakini wameziweka sehemu ambazo si sahihi, matokeo ya haya ni anguko la biashara hiyo au faida finyu ktk biashara hiyo.
 
Back
Top Bottom