Nifanye nini na huyu mzee jamani?

Elia

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
3,425
Reaction score
568
Alikuja kusalimia kwa shemeji yangu akapenda kunisalimia na mimi. (mambo ya extended family na kujuana)
Kwangu niliambiwa ataondoka baada ya siku mbili lakini ikawa wiki mara mwezi.
Akarudi kwa shemeji ikiwa ni safari ya kurudi mkoa nilimuaga na kumpa pocket money.
Alipofika kwa shemeji hakuondoka kama alivyoaga badala yake nikapigiwa simu tumchangie hela ili imsaidie maisha yake atapoondoka(mtaji) nilituma kwa M-pesa.

Miezi miwili ikapita kumbe bado yupo kwa shemeji hakuondoka…
Sasa wiki iliyopita amekuja nyumbani kwangu haniambii story yoyote yaani amefika. Nilichukia sana maana alikuja bila taarifa narudi kazini namkuta amejaa sebuleni sikupendezwa na ujio wake
Nimejaribu kuchunguza mkoani kwa nini huyu mzee hataki kurudi kwao.
Jibu nililopata ndio lililo niogopesha nasikia hawamtaki kijijini kwake sababu za kichawi yaani ni mwanga sana nimeambiwa yeye na mwenzake walifukuzwa na sungusungu
 

nyumbani kwako ni kwako. ki msingi hata kama angekuwa ni mzazi wako au ndugu wa damu ni jambo la kumuuliza tu kuwa uwepo wake hapo una sababu gani na ataondoka lini , basi. huhitaji kusema maneno mengi. kama hana jibu , tafuta nauli mkatie ticket , mpeleke huko kwenye usafiri wa kurudi alikotoka.
usipoweza kuwa muwazi mapema, utakuwa unaumia moyoni, utaanza kunung'unika na hata kuanza ku mtreat vibaya akaishia kukulaumu
 
Ni babako mzazi au mzee wa namna gani? Maana kama ni babako mzazi, nafikiri kuna ugumu mkubwa wa namna ya kumuondoa, lakini kama ni ndugu wa kawaida, naamini unaweza kutumia akili yako ya kawaida kumwondoa
 
mmmh, akuroge mna bifu?
Kwani hana watoto, trust me hurogeki kama hujihusishi na uchawi.
 
duuh hii mambo uwa siipendi hata kidogo
 
Ni babako mzazi au mzee wa namna gani? Maana kama ni babako mzazi, nafikiri kuna ugumu mkubwa wa namna ya kumuondoa, lakini kama ni ndugu wa kawaida, naamini unaweza kutumia akili yako ya kawaida kumwondoa
Sio baba ni anko wangu
 

Huyo mzee wala hajafukuzwa kijijin na wala sio mchawi kama unavyodai...ni chuki zilizosababishwa na udhaifu na uoga wako ndizo zilizokupelekea kumhisi ama kuamini maneno ya kuambiwa kuwa huyo mzee kafukuzwa kwa sababu za kichwawi.

Nashindwa kuelewa kuwa kuna watu wa namna yako i.e unahangaika kuulizia huko alikotoka wakati mtu uko naye nyumbani kwako,..na unaacha kumwambia ukweli,...unahangaika kuja kumsengenya huku kwenye mitandao

Ushauri:.mrudishie mwenye mzigo huyo shemeji yako badala ya kuumiza kichwa ufanye nini juu ya mtu ambaye sio ndugu yako.
 
Hapo ndugu yangu Elia inabidi ufuate ushauri wa Kindimbajuu kwamba sema nae usiogope maana tatizo la sie watz inapokuja suala la kumwambia ukweli mtu kwamba humtaki au ana kasoro flani ktk mfumo wa maisha inakuwa shida ndio maana imeathiri mpaka kwenye sehemu zetu za kazi including bungeni. Wewe mweleze kama ni mtu ambae hajavuka 25 years au 30 years kama amemaliza chuo at least maana extended family haziepukiki sometimes ila kiukweli mweleze maana watu wengine wazima wamezidi hata mshipa wa aibu hawana. Watu kama hao hutakiwi kumpa nafasi ya kumzoea sana nikiwa na maana akifika kwako unamtolea na shuka mpya badala yake kama hajaja na shuka unampotezea
 
Last edited by a moderator:
pole sana usiogope hiyo ni mitihani ya hapa Dunia keti na ndugu zako ili muweze kujadili kama familia I hope utapata jibu.
 
Hata kama baba yako Elia unaweza ukamtoa kiana maana kama hana shughuli hapo au hajaja kutibiwa katika hospitali kubwa ya mjini, inabidi tu utumie technique ya kumuondoa maana privacy inakuwa haipo pia anatakiwa akuache na wewe u-practice ubaba/umama wako kwa familia yako
 
Last edited by a moderator:

Asante mkuu, mgeni mwenyewe yupo above 60yrs. ila nashukuru kwa ushauri wako
 
yaani mungu anisamehe kwa kweli sijaoa ila nilishamuambia hata mama yangu nikipata familia yangu mimi na wife tu hata mama yangu kuja aje na kuondoka na kama tupo mbali nae sisi ndio tutakuja kukusalimia , nina uzoefu na haya mambo aisee yanacost cost sana na yanavuruga amani hapana aisee. kwanza pole sana kwa hilo naomba umpe makavu aisee please bora lawama kuliko hasara. maisha yamepanda sana kumtunza mtu mzima ni gharama sana sio kama zamani vyakula vilikuwa vya bei chee siku hizi hadi mchicha unanunua zamani unachuma hapo nyuma ya choo tu mnajilia leo unauzwa no haiwezekani.
 
Ooh! Leo inabidi ujikoki kisawaswa kwa maombi. Unaweza kuta mzee mwenyewe ni mwanajamvi. Utakomaje mkuu!
 
Duuh me naogopa hata kuchangia ukute babu anawaona wanaomdiss humu kwa TV ya asili,all the best kwa utakalo amua!
 
kazi keli kweli watanzania na imani tuko juu sana basi waunganike na prof maji marefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…