Nifanye nini nimsahau mtu niliyekuwa navutiwa naye kimapenzi ila sikufanikiwa kuwa naye?

Nifanye nini nimsahau mtu niliyekuwa navutiwa naye kimapenzi ila sikufanikiwa kuwa naye?

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,479
Reaction score
1,348
Habari za muda huu Ndugu zangu. Poleni na changamoto za kupambana na Uviko 19.

Nije moja kwa moja kwenye mada, hivi ukimpenda Msichana au Mvulana unayeweza kuongea nae kimapenzi ingawa hujatembea nae.

Mawasiliano yake muda mwingine yamekua ya kusuasua anaweza kujibu meseji na wakati mwingine simu hapokei ,unawezaje kumsahau mtu kama huyu?.

Na wakati mwingine unaweza unaamua kabisa kumsahau na kujisemea huyu sita mpigia tena simu lakini ikipita wiki unaanza mkumbuka na kumpigia tena.

Ni namna gani unaweza kuacha kumkumbuka mtu wa namna hii na kuachana nae kabisa bila kumtafuta tena?
 
Fahamu shida yake kubwa kwa sasa ni ipi?
Jaribu kumsaidia hiyo shida bila ku force mapenzi...mpe nafasi aone unavyomjali...

Halafu kaa pembeni muache Aku miss kwanza..
Binafsi ni ngumu kueleza shida yake ingawa ukikaa kimya muda mrefu na yeye anauchuna ila ikija siku ukampigia inaonesha kwamba kama umemsahau.
 
Muulize .. anafanya nini?Ndoto yake ni ipi?
Anaishi na nani?Maisha anaonaje?Mipango yake ikoje?Utajua Tu shida yake
Kwasasa anaishi peke yake na huwa naenda mpaka kwake ingawa kwenye baadhi ya mambo mengine hataki kueleza kama mipango yake, maisha kwa ujumla nk
 
Delete namba yake,kisha hasira zako zielekeze kwenye kutafuta Pesa,life is very short,kwanini uwe mtumwa wa mtu? Kwanini uteseke? Unaonekana wewe ni mtu dhaifu sana,usiforce mapenzi,huko mbele atakuja kukuumiza zaidi,

Grow up.
 
Pesa inatafutwa kama kawaida ndugu na napambana kisawasawa,ila sema namba hata nikidelete naitafuta tena[emoji23]
 
Fahamu shida yake kubwa kwa sasa ni ipi?
Jaribu kumsaidia hiyo shida bila ku force mapenzi...mpe nafasi aone unavyomjali...

Halafu kaa pembeni muache Aku miss kwanza..
Ushauri mzuri
 
Delete namba yake,kisha hasira zako zielekeze kwenye kutafuta Pesa,life is very short,kwanini uwe mtumwa wa mtu? Kwanini uteseke? Unaonekana wewe ni mtu dhaifu sana,usiforce mapenzi,huko mbele atakuja kukuumiza zaidi,

Grow up.

Aisee haiusiani na kutafuta hela au ukubwa

Kuna mtu nilimwona kama mara mbili Hivi ila amegoma kuondoka kichwani ni mshirika wa Mr

Ila kila nikikaa picha ya yule jamaa inanijia moyo unajazwa na mahaba

Kiukweli ni kazi ngumu kupingana na upendo unaokuja automatic
 
Back
Top Bottom