Nifanye nini wasichana waache kunitania?

Nifanye nini wasichana waache kunitania?

Punguza tabia ya kuzoeleka kirahisi. Unapowafanya wanawake/wasichana kuwa ni rafiki zako kwa kiasi kikubwa inafika point wanakuchukulia kama nawe ni miongoni mwao. Wanakuweka kundi moja na marafiki wengine wa jinsia yao/shoga yao. Jitenge nao mkuu, maana inaonekana hata kuwatafuna huwezi. Jifunze kuwa mwenaume.
 
Mkuu usikatae kutaniwa maana inakufanya unakuwa karibu na watu na hata ikitokea shida unakuwa wa kwanza kusaidiwa maana utakua watu wanaweza kukukabili ipasavo. Ila usikubali kutaniwa mpaka kupitiliza... Nakwambia hivi kwasababu hata mimi nipo sector fulani nataniwa sana mpaka kuna watu nikiwaona kwa mbali nageuza njia ila haijafika hatua ya kuitwa boya maana mda mwingine nakua serious hususani wakati wa kazi. Ninaowazidi cheo wananifaham nikiwa kazini hususan wanawake nakua kauzu ila tukimaliza majukumu wanaanza kujiuliza ndo huyu kweli??? Ni hayo tu mkuu.
 
Ingekuwa mimi kwa jinsi maisha yalivyo magumu nisingeangalia cha dada wala mama zaidi ya performance nzuri darasani kwa sababu baada ya miaka kadhaa kila mtu atatawanyika na kuelekea alikotokea.

Ushauri wangu, komaa na book achana na maisha ya ki muonekano, hata mimi wakati niko O Level watu walinisema kwamba nina natatizo ya uzazi maana hawaoni hata siku moja nikijipenyeza kwa mademu hadi namaliza,ila kiuhalisia niko vyee na sina tatizo lolote lile "jogoo yuko active"
 
Punguza tabia ya kuzoeleka kirahisi. Unapowafanya wanawake/wasichana kuwa ni rafiki zako kwa kiasi kikubwa inafika point wanakuchukulia kama nawe ni miongoni mwao. Wanakuweka kundi moja na marafiki wengine wa jinsia yao/shoga yao. Jitenge nao mkuu, maana inaonekana hata kuwatafuna huwezi. Jifunze kuwa mwenaume.
Hakika umeongea point sana bro.mazoea yake na hao viumbe inabidi awe nao makini sana maana itafika mahali atadhalilishwa sana haswa public
 
Ingekuwa mimi kwa jinsi maisha yalivyo magumu nisingeangalia cha dada wala mama zaidi ya performance nzuri darasani kwa sababu baada ya miaka kadhaa kila mtu atatawanyika na kuelekea alikotokea.

Ushauri wangu, komaa na book achana na maisha ya ki muonekano, hata mimi wakati niko O Level watu walinisema kwamba nina natatizo ya uzazi maana hawaoni hata siku moja nikijipenyeza kwa mademu hadi namaliza,ila kiuhalisia niko vyee na sina tatizo lolote lile "jogoo yuko active"
Lakini kwa upande mwingine nionavyo kwa mtazamo wangu, hadi mtoa mada kutishia kuua ni kwamba yawezekana ni kind of bullying anaipitia hususan kwa peer group inayomzunguka
 
Hivi jamani, nifanyeje ili niogopwe na wasichana? Yaani wawe na hata ile hofu wanaponiona, nipo chuo mwaka wa 2. Inafika kipindi nataniwa hovyo hovyo hata kama sitaki.

Pia naitwa majina ya hovyo, natamani kuwa kauzu kama baadhi ya wanaume wenzangu, inafika wakati msichana ananiita "wewe boya njoo", naumia sana. Kwa nini mimi? Mbona wengine wanaheshimika? Au kisa ni makauzu?

Nipo nasoma Aircraft Engineering degree. Karibuni kwa ushauri!

Wewe kweli ni boya, kwani kulikuwa na haja gani ya kutaja unachosomea...!?
Waendelee tu kukuita boya, tena ikibidi bumunda!
 
Hivi jamani, nifanyeje ili niogopwe na wasichana? Yaani wawe na hata ile hofu wanaponiona, nipo chuo mwaka wa 2. Inafika kipindi nataniwa hovyo hovyo hata kama sitaki.

Pia naitwa majina ya hovyo, natamani kuwa kauzu kama baadhi ya wanaume wenzangu, inafika wakati msichana ananiita "wewe boya njoo", naumia sana. Kwa nini mimi? Mbona wengine wanaheshimika? Au kisa ni makauzu?

Nipo nasoma Aircraft Engineering degree. Karibuni kwa ushauri!
Pole sana. Hiyo kitu unayofanyiwa inaitwa bullying na ni tabia ambayo si ngeni ni ya miaka na miaka na almost kila mtu aliipitia kwa namna moja au nyingine.

Na hufanywa na watu ambao hawajapevuka kiakili kuwa andama wale ambao wameonyesha kutojitetea au kuwa wapole.

Hii kitu huwa na madhara kwa muhusika ingawa jamii huchulia sio issue kubwa na huwa ni michezo tu ya kitoto ingawa kwa wahanga (victims) hii kitu huwanyima amani na muda mwingine hata kufikia hatua mbaya ya hao victims kujiua (suicide) au kudhuru wengine kwa kuwashambulia kwa silaha za moto hadi kuwaua au kujeruhi na kuharibu mali.

But bila kukuza mambo hii kitu haiwezi kuwa tatizo lisilosuluhishika especially kwako wewe mtoto wa kiume. Watoto wa kiume wako exposed kupata bullying attacks mapema sana kuliko wa kike maana huwa wanajitegemea katika kujilinda tofauti na wakike ambao hulindwa na jamii nzima.

Bullies furaha yao ni kukuona unakasirika , unadhurika au unakuwa affected na yale wanayokufanyia. Kile wanachokufanyia kisipokufanya ureact wao huwa wanakuwa irritated na kuona wamekosea mtu wa kumchokoza.

So jua kuwa bullies huchochewa kukuchokoza zaidi pale wanapoona unarespond ule ukorofi wao.

Kuna namna kadhaa za kudeal nao. Ya kwanza ni kisurrender yaani uwe mpole wakuonee hadi wachoke , au kuwajoin na kuwa kilaza wao ili wasiendelee kukufanya target wao au tatu ni kuretaliate au kwa kiswahili tunasema ni kujibu mashambulizi.

Mimi kwa upande wangu huwa retaliation inafanya kazi haraka. Ila kutumia hii mbinu inabidi uwe na akili timamu (sane), smart(mwerevu), patient (subira) na muhimu zaidi uwe na mipaka ya kimaadili. Sio mtu amekupiga au kakudhalilisha wewe unakwenda shambulia mzazi wake, mtoto wake, mke wake au ndugu yake hiyo sio sawa.

So the best unaweza fanya na hii technique ni kumjua kiundani huyu adui yako. Trust me hakuna mtu ambaye hana matizo, shida, au siri ambazo hataki jamii izijue. Kwakifupi tafuta weakness yake au jambo ambalo ukimgusa nalo utamvunja spirit yake into pieces.

Ukifanikiwa kujua center of weakness ya adui yako ni rahisi sana kumrudishia maumivu mara mbili na kumfanya akikuona abadili njia au kuwa na adabu na akakupa heshima yako.

Kuna dogo mmoja alikuwa arrogant sana. Anapenda sana kuongea pumba anapokuwa na audience. Na ana enjoy sana kuwa roast wenzake kwa maneno makali anayoweka katika kivuli cha utani (sarcasm). Kamati ya fitina tukaja kujua kuwa gari anayotumia, biashara na nyumba anaishi ni mwanamke wake anaprovide.

Ilichukua siku moja tu kumfanya atupe heshima kila aliekuwa anamletea upuuzi.

So hao watu wachunguze kimya kimya maisha yao hawakosi weakness then itumie kuwarudi kwa utulivu kabisa.
 
Hayo ma aircraft engine unayosomea si unapata access ya petroli ? Nunua dumu mtie kibiriti mmoja ya hao wanaokudharau, kwisha kazi yake watakuheshimu....au nunua bunduki kunywa bia nyingi halafu uwe unawatishia kama unataka kuwaua !
Yaani umetumia matukio kujibu comment [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbe nimeamini genye zikizidi unacheka cheka hovyo hadi unadharaulika
 
Hivi jamani, nifanyeje ili niogopwe na wasichana? Yaani wawe na hata ile hofu wanaponiona, nipo chuo mwaka wa 2. Inafika kipindi nataniwa hovyo hovyo hata kama sitaki.

Pia naitwa majina ya hovyo, natamani kuwa kauzu kama baadhi ya wanaume wenzangu, inafika wakati msichana ananiita "wewe boya njoo", naumia sana. Kwa nini mimi? Mbona wengine wanaheshimika? Au kisa ni makauzu?

Nipo nasoma Aircraft Engineering degree. Karibuni kwa ushauri!
Nimecheka, eti we boya njoo.
Njoo hapa mwembe mgomo nikufundishe.!
 
Ingekuwa mimi kwa jinsi maisha yalivyo magumu nisingeangalia cha dada wala mama zaidi ya performance nzuri darasani kwa sababu baada ya miaka kadhaa kila mtu atatawanyika na kuelekea alikotokea.

Ushauri wangu, komaa na book achana na maisha ya ki muonekano, hata mimi wakati niko O Level watu walinisema kwamba nina natatizo ya uzazi maana hawaoni hata siku moja nikijipenyeza kwa mademu hadi namaliza,ila kiuhalisia niko vyee na sina tatizo lolote lile "jogoo yuko active"
Ahsante sana kaka!
 
Back
Top Bottom