Nifanyeje ili niepushe uadui na huyu mfanyakazi mwenzangu?

Nifanyeje ili niepushe uadui na huyu mfanyakazi mwenzangu?

Mimi ni kijana ninaefanya kazi mahali Fulani na muda wangu wa kazi ni usiku tu....tupo wawili Mimi na mwenzangu ambae tunabadilishana zamu sasa nikiingia Mimi wateja wanakuwa wengi Hadi wananizidia uwezo lkn akiingia yeye anapata wateja wachache Hadi boss anatamka Hilo swala mbele yake na imepelekea yeye kuninunia...sasa imekaaje hii kiroho na nifanye nn ili kuepusha uadui
Wewe ni mlinzi? au Mtumishi wa guest/lodge au unafanya kazi bar? tuanzie hapo ili tukushauri vizuri
 
Asilimia kubwa ya maboss hawana busara
Nishakutana na matatizo kwasababu ya boss kutamka maneno kama hayo
Hua yanaumiza kwa upande mwengine
Mweleze Boss atumie busara kutuliza bahari
 
Badili shift uangalie, labda wateja wengi wako nyt... ila bado hujajibu wadau! kuna mahala unajiongeza juju au ni ufanisi wako na kismati tu?
 
Mimi ni kijana ninaefanya kazi mahali fulani na muda wangu wa kazi ni usiku tu na huwa tupo wawili

Mimi na mwenzangu ambae tunabadilishana zamu.

Katika zamu yangu huwa wateja ni wengi hadi wananizidia uwezo lakini akiingia yeye anapata wateja wachache hadi boss anatamka hilo suala mbele yake na imepelekea yeye kuninunia

Hii imekaaje?

Na nifanye nini ili kuepusha uadui?
Endelea kupiga kazi. Ila ata ukisifiwa mbele yake take it easy. Angalia usije ukaanza majivuno kwa mfanyakazi mwezako kwa kuwa unasifiwa. Lolote linaweza kutokea.
 
Hospital nyingi ikishafika usiku watu huwa wanapungua kwa sehemu nyingi nilizoziona
 
Huenda una kauli nzuri kwa wateja wako au una kitu kingine cha ziada kinachokufanya wateja wafurahie kuhudumiwa na wewe, endelea kufanya kazi kwa bidii lakini usimdharau mwenzako muheshimu na msaidie pale inapobidi.
 
Mimi ni kijana ninaefanya kazi mahali fulani na muda wangu wa kazi ni usiku tu na huwa tupo wawili

Mimi na mwenzangu ambae tunabadilishana zamu.

Katika zamu yangu huwa wateja ni wengi hadi wananizidia uwezo lakini akiingia yeye anapata wateja wachache hadi boss anatamka hilo suala mbele yake na imepelekea yeye kuninunia

Hii imekaaje?

Na nifanye nini ili kuepusha uadui?
na wewe mnunie!!
 
Huyo boss wenu ndio mpuuzi.
Kama kazi ni hiyo maana yake usiku ndio wateja wapo na sio mchana muda anaongia huyo mwenzako.
Au na wewe unataka kusema wateja wanakuja kwasababu upo wewe?
 
Back
Top Bottom