Nifanyeje ili niepushe uadui na huyu mfanyakazi mwenzangu?

Wewe ni mlinzi? au Mtumishi wa guest/lodge au unafanya kazi bar? tuanzie hapo ili tukushauri vizuri
 
Asilimia kubwa ya maboss hawana busara
Nishakutana na matatizo kwasababu ya boss kutamka maneno kama hayo
Hua yanaumiza kwa upande mwengine
Mweleze Boss atumie busara kutuliza bahari
 
Badili shift uangalie, labda wateja wengi wako nyt... ila bado hujajibu wadau! kuna mahala unajiongeza juju au ni ufanisi wako na kismati tu?
 
Endelea kupiga kazi. Ila ata ukisifiwa mbele yake take it easy. Angalia usije ukaanza majivuno kwa mfanyakazi mwezako kwa kuwa unasifiwa. Lolote linaweza kutokea.
 
Hospital nyingi ikishafika usiku watu huwa wanapungua kwa sehemu nyingi nilizoziona
 
Huenda una kauli nzuri kwa wateja wako au una kitu kingine cha ziada kinachokufanya wateja wafurahie kuhudumiwa na wewe, endelea kufanya kazi kwa bidii lakini usimdharau mwenzako muheshimu na msaidie pale inapobidi.
 
na wewe mnunie!!
 
Mkuu mtu akinuna wewe inakuhusu nini labda kama kuna kitu umechezesha
 
Huyo boss wenu ndio mpuuzi.
Kama kazi ni hiyo maana yake usiku ndio wateja wapo na sio mchana muda anaongia huyo mwenzako.
Au na wewe unataka kusema wateja wanakuja kwasababu upo wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…