Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?
Kuna uzi mwingine kama huu upitie watu walijaribu kuelezea mengi. Bofya hapa:
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/138113-naweza-kuongeza-uwezo-wa-kufikiri.html
Epuka kusoma au kusikiliza habari ambazo zinazungumzia upande mmoja tuu. Kwa mfano, nimeona
LumumbaDAR akikushauri ujiunge na Chadema kama vile tayari anajua wewe ni mfuasi wa chama kingine. Ni lile lile tatizo la kufikiria kila kitu kwa kutumia siasa.
Siyo yote yanayosemwa na Chadema ni sahihi na siyo wote walioujiunga na Chadema wana uwezo mkubwa wa kufikiri. Na kwa siasa zetu hizi za maji taka sidhani kama kuna lolote la maana la kujifunza.
Kwa hiyo, jitahidi na usiruhusu ubongo wako ufungamane na upande wowote ule. Hata kama unafungamana na upande mmoja, uwe huru kuangalia au hata kukubaliana na upande mwingine wa hoja pale inapolazimu. Hii itakusaidia kupanua uelewa wako kwenye mambo mengi.
Usikubali au kumkataa mtoa hoja, bali kubali au pinga hoja yake kwa kujaribu kuja na hoja yako. Kama huna hoja unaweza kukopa hoja ya mtu mwingine kusizitiza unachokisema. Usiwe unakubaliana na hoja moja kwa moja. Kuwa na desturi ya kutaka kuhoji. Hata kama unakubaliana na hoja yake, uwe na sababu za kufanua hivyo. Usikubaliane au kukosoa hoja kwa vile tuu imetolewa na mtu fulani.
Naelewa Tanzania kuna tatizo la mtu kuonekana mhaini pale unapohoji jambo. Mwanasiasa anaweza kusema kitu, ukaanyoosha mkono na kuuliza swali la kuhoji alichosema, baada ya hapo utajikuta umepigwa "Tanganyika jeki". Hatuna desturi ya kukubali kuhojiwa bali tunataka kukubaliwa na kila kitu tunachokisema hata kama siyo sahihi. Ukifanikiwa kuepuka hilo utakuwa na uhuru wa fikra.
Jaribu kusoma mara kwa mara. Hapa utakumbwa na tatizo maana vitabu vingi vimeeandikwa kwa Kiingereza. Hata hivyo, mababu zetu hawakusoma sana na wanatoa hoja nzuri sana kwa kutumia busara na hekima zao.
Huitaji uwezo mkubwa sana kuelewa au kuhoji mambo. Tumia uelewa na ujuzi wa kawaida ambao kila mtu anao (common sense) hata kama hajaenda shule. Kwa mfano, kama
LumumbaDAR anakushauri ujiunge na Chadema ili uwe na uwezo mkubwa wa kufikiri mhoji kwani wote walioko Chadema wana uwezo mkubwa wa kufikiri? Au wale wooooote wasio Chadema hawana uwezo mkubwa wa kufikiri? Vipi wale ambao hawapo upande wowote ule?
Jibu atakalokuja nalo utagundua kuwa pamoja na yeye labda kuwa na elimu ya chuo kikuu na wewe kuwa na elimu ya darasa la saba, wala hamjapishana sana katika kufikiri na kuhoji. Tumia busara, hekima, na common sense (uelewa na ujuzi wako wa kawaida ulionao).
Tatizo la watu ambao hawajaenda shule wanaamini kuwa walioenda shule wana akili sana. Hata hivyo, wengi hawakufanikiwa kwenda shule kwa sababu mbalimbali. Na kama wale walieonda shule wana uwezo mkubwa sana wa kufikiri, basi nchi yetu isingekuwa hapa ilipo. Si inaendeshwa na "first class economists" (wasomi waliofaulu vyuo vikuu kwa alama ya "A")?