kuwa na akili ya kutambua vitu na kukabiliana navyo ninaweza kusema ni 1]kipaji
2]mazingira
3]changamoto
4]Elimu
Nilibahatika kusoma vitabu vya dini kimojawapo ni cha hekima ya sulemani
kina mapana sana,
kwa mfano huyu sulemani aliletewa kesi ya akina mama wawili walikuwa wanabishana[wakimgombea mtoto
kila mmoja akisema ni wa kwake. hiyo kesi ilipofikishwa kwa sulemani akawaita wale akina mama, akamchukua yule mtoto akawauliza ni nani mama wa huyu mtoto?
kila mama akasema ni wa kwake.
kwa haraka haraka na kwa kuwa sulemani hakujua ni nani mwenye uhalali wa yule mtoto akawaambia, ni sawa kila mmoja anadai kuwa mtoto ni wa kwake na mtoto ni mmoja, sasa mimi nitampasua katikati kila mmoja wenu achukue kipande kimoja. baada ya sulemani kusema hivyo yule mama ambaye mtoto hakuwa wa kwake akasema ni sawa.
kwa sababu hakuwa na uchungu naye na hakuwa mtoto wake. lakini yule ambaye alikuwa mama halali wa mtoto akasema hapana usimpasue mtoto, ni bora mimi nimkose apewe huyo mama aliyetaka mtoto apasuliwe vipande viwili awe wa kwake. hapo sulemani akamtambua mama wa mtoto kuwa ni yule aliyekuwa na uchungu naye. nina maana sulemani hakusoma ila alikuwa na kipaji cha kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ya haki.
ninaungana na wachangiaji kuwa unaweza kusoma sana lakini usiwe na maarifa. ni mara ngapi wasomi wetu tuliowaamini wanashindwa hata kuingia mikataba mizuri na wawekezaji? badala yake wanaingia mikataba mibovu ya kutugharimu maisha yetu yote?