Da vinci jr
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 202
- 34
Nashukuru kwa michango yenu wakuu! Lakini, watu wa vijijini wanakula sana nafaka zisizokobolewa lakini uwezo wao bado ni mdogo hata kuweza kuzitambua fursa zilizopo katika mazingira yao ziwakwamue katika umasikini ulio kithiri inakuwa bado ni shida, hii inakuwaje? Waliochangia na kusisitiza nafaka zisizo kobolewa naomba waelezee kidogo kuhusu hili jambo.
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, naomba unipe falsafa moja tu nianze kuufanyia kazi ushauri wako kwa kuitafakali hiyo falsafa iwe kama mwanzo wa utekelezaji wa ushauri ulionipa.
OK mimi ninauelewa ili kuongeza uwezo wako wa kufikiri kwanza unatakiwa ujitambue wewe ni nani na unafanya nini kwa manufaa ya nani kwa muda gani, mpaka hapo utakuwa umeanza kuiumiza akili itoke nje ya boksi halafu anza kufikiria unakabiliwa na changamoto gani? chanzo chake ni nini? utazimalizaje? Utatumia njia gani? hapo pia itakusaidia kuanza kuwa na mawazo chanya. Pia penda kuwa unakaa na watu wa tofauti na kiwango chako cha maisha kwa maana ya juu yako hawa mara nyingi watakusaidia jinsi ya kufanya mambo kwa namna na kiwango chao itakupa changamoto na utakuwa unaendelea kukua siku hadi siku.
Mengine usile bila mpangilio kula kwa-
NB: WATU WENGI HUCHUKULIA MATATIZO YAO NI KAMA MIKOSI AU HAYATAKIWI KUJA KWAO, MATATIZO YAPO NA LAZIMA YAJE, CHUKULIA KILA TATIZO NI CHANGAMOTO SIO TATIZO .
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?
Soma vitabu vya ma great thinker kama kina aristotle,smith,kiyosaki pia soma magazeti yenye kuelimisha zenye makala nzuri achana na magazeti ya rangi rangi upe mazoezi ubongo kwa kureason reason vitu utakavyoviona n.k
Kwa kifupi niseme ukitaka kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, Basi Fikiria sana.
Kula sana mayai
kuwa na akili ya kutambua vitu na kukabiliana navyo ninaweza kusema ni 1]kipaji
2]mazingira
3]changamoto
4]Elimu
Nilibahatika kusoma vitabu vya dini kimojawapo ni cha hekima ya sulemani
kina mapana sana,
kwa mfano huyu sulemani aliletewa kesi ya akina mama wawili walikuwa wanabishana[wakimgombea mtoto
kila mmoja akisema ni wa kwake. hiyo kesi ilipofikishwa kwa sulemani akawaita wale akina mama, akamchukua yule mtoto akawauliza ni nani mama wa huyu mtoto?
kila mama akasema ni wa kwake.
kwa haraka haraka na kwa kuwa sulemani hakujua ni nani mwenye uhalali wa yule mtoto akawaambia, ni sawa kila mmoja anadai kuwa mtoto ni wa kwake na mtoto ni mmoja, sasa mimi nitampasua katikati kila mmoja wenu achukue kipande kimoja. baada ya sulemani kusema hivyo yule mama ambaye mtoto hakuwa wa kwake akasema ni sawa.
kwa sababu hakuwa na uchungu naye na hakuwa mtoto wake. lakini yule ambaye alikuwa mama halali wa mtoto akasema hapana usimpasue mtoto, ni bora mimi nimkose apewe huyo mama aliyetaka mtoto apasuliwe vipande viwili awe wa kwake. hapo sulemani akamtambua mama wa mtoto kuwa ni yule aliyekuwa na uchungu naye. nina maana sulemani hakusoma ila alikuwa na kipaji cha kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ya haki.
ninaungana na wachangiaji kuwa unaweza kusoma sana lakini usiwe na maarifa. ni mara ngapi wasomi wetu tuliowaamini wanashindwa hata kuingia mikataba mizuri na wawekezaji? badala yake wanaingia mikataba mibovu ya kutugharimu maisha yetu yote?
Mkuu kwa hili jibu nimekukubali! Nilikuwa nahitaji jibu kama hili, yaani kufikiria ili uweze kutatua changamoto zinazo kukabili kwa wakati huo. Ni njia nzuri ingawa inategemea na tatizo lenyewe aidha linahitaji majibu ya papo kwa papo au ya muda mrefu. Pia inategemea na maamuzi yako aidha ya haraka au ya polepole. Thanks!
"Unaweza kudanganya watu wote kwa wakati fulani, na unaweza kudanganya watu fulani wakati wote lakini huwezi kudanganya watu wote wakati wote" wadau watakusaidia kujua ni mwanafalsafa gani huyo, wewe ifikirie kwanzan hiyo kama ina maan kwako
Mm jana nilikwenda kumpa pongezi mzazi aliyejifungua,mtoto alikuwa hata hajatimiza masaa 24,nikapata udadisi wa kujua huyu mtoto kwa sasa ubongo upo vp,unavyofanya kazi and the like. Nikaingia intaneti nikasoma. Ukiwa na mawazo haya inasaidia sn.