kuna wakati nami niliwaza kama wewe, watu wa karibu walionipa ushauri ni kwamba nisome vitabu nami nafanya hivyo ilakiukweli maandishi mengi yenye kugawa maarifa yapo katika lugha ya kiingereza, so anza kujifunza kiingereza kwanza.
Endelea kufikiri!
Endelea kufikiri!
Ubongo wa binadamu muda wote huwa unafikiri. Popote ulipo, kazini, unatembea barabarani, unakula, unaoga, umekaa, n.k ubongo huendelea kufikiri. Sio kwamba nilipoleta huu uzi hapa JF ubongo wangu ulisimama kufikiri, la hasha! Nilihitaji kujua ni namna gani ya kuongeza au kukuza uwezo wa kufikiri zaidi ya huu nilionao kwa sasa sababu mazingira yanabana unaweza kujikuta ume-perish! Kuna ka kauli alikasemaga 'Darwin' kuwa viumbe watakaoweza kukabiliana na mabadiriko ya mazingira ndio watakao endelea kuishi na watakaoshindwa basi watatoweka duniani.
Soma , Cheza.. Mengine yote ni assumption tu. Chakula kina upa ubongo wako capacity au potential ya kuwa critical thinker. lakini kuwa critical thinker unahitaji tu kusoma vitabu na kucheza michezo. hii ni kwa sababu kusoma ni kupata maarifa. na kucheza ni kutumia maarifa. kwahiyo ukisoma tu bila kucheza michezo au kufanya ubongo wako uchambue na kuunganisha maarifa uliyo nayo kutatua matatizo ni bure.
Kwa kifupi niseme ukitaka kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, Basi Fikiria sana.
Haya maelezo hapa juu inaonyesha bado unasita kufikiri, nasema endelea kufikiri hii ina maana sana.
Ubongo haufikiri, ubongo unafanya kazi ipasavyo, Ubongo haufikiri kamwe!
Kama ubongo ukifikiri tu kwa dakika moja binadamu hupata msukosuko na hatimaye hufa.
Mkuu nikipitia majukwaa mengine hayatasaidia kuongeza uwezo wangu wa kufikiri isipokuwa jukwaa la critical thinker tu? Naomba unifafanulie kidogo!
Naomba unifafanulie kazi ya ubongo ni ipi mkuu? "Ubongo unafanya kazi ipasavyo" ni kazi gani hiyo ambayo ni tofauti na kufikiri? Hoja yako bado sijaielewa mkuu hebu tuweke wazi hata sisi wenye uwezo mdogo wa kufikiri na kupambanua mambo tuweze kuelewa.
Hoja yako bado sijaielewa mkuu hebu tuweke wazi hata sisi wenye uwezo mdogo wa kufikiri na kupambanua mambo tuweze kuelewa.
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?
Hapa ulisita kufikiri sababu mwanzoni ulitoa mada ukionesha nafsi ya kwanza umoja, lakini kwa sasa unasema "sisi wenye uwezo mdogo wakufikiri..." Inaonesha mko wengi je wewe na nani?
Hapa mimi najaribu kufikiri!
The fear of the Lord, is the beginning of the knowledge (proverbs 1:7)
For the Lord giveth wisdom: out of his mouth cometh knowledge and understanding (Proverbs 2:6)
Know the love of Christ: which passeth knowledge, (Ephesians 3:19)
Tragedy of the commons
Mkuu nashukuru kwa mchango wako ntaufanyia kazi
!Nilipo post hii thread nilimaanisha ni mimi binafsi sababu hayo mawazo ya kuongeza ufikiri wangu yalinijia nikiwa peke yangu, lakini kadri watu wanavyo endelea kuchangia kwenye hii thread baadhi yao wanaonyesha wanauhitaji wa kuongeza uwezo wao wa kufikiri ndio maana nilipo kujibu kwenye ile post yako nikawajumuisha na nafsi ya tatu uwingi ambao wanauhitaji wa kuongeza uwezo wao wa kufikiri.
1.jishughulishe na mambo ya kufikirisha!
2.tumia muda wako mwingi na watu walio kuzidi uwezo kifikra!
3.acha kujishughulisha na mambo ya kipuuzipuuzi!
Kwa umri niliokuwa nao nimejifunza kuwa katika maisha vipo vitu ambavyo huwa vinahitaji seriousness otherwise you will end in trouble, especially wakati watu wanajadiri important issues afu we unaingiza joking, Hilo ni tatizo (I accept correction)Chukua dictionary pamoja na vitabu vingine vya maarifa mbalimbali ( kama physics , biology , philosophy etc) kulingana na eneo unalotaka kuongeza maarifa. Chukua sufuria kubwa ( kama huna azima) chemsha pamoja dakika tatu then weka mbilimbi au ndimu na tokosa pamoja kwa dakika 15. Kunywa maji yake angalau nusu lita kwa siku muda wa miezi mitatu mpaka minne. Ukitaka kuwa genious kunywa mchnaganyiko huo kwa muda wa mwaka mzima......Mimi nilifanya hivyo sasahivi ni Professor Mlimani............