Kwa hapa kwetu ni vigumu kupata mwanasiasa anayepractice siasa then ukamtegemea awe pia political analyst na akawa fair... wengine si walipojaribu wamekolimbwa na tunakumbuka? Hata nyerere kuna wakati walitishia kumpoka kadi baada ya kuwasema, Sitta naye amekuwa akijaribu (though kwa motives zake) na cha moto ameshakiona kwani ilibidi tupate hata spika mwanamke bila kupenda wala kujiandaa...pengine tuangalie waliopo nje unaweza kukuta wachache....very few of them.....wapo watu kama kina Jenerali Ulimwengu pengine nikikumbuka mwingine nitarejea....Bongo kila kitu ni kipya na ni vigumu kukiandikia maana tupo unique kwenye mambo mengi.
KIONGOZI
Chanzo cha Tatizo ni vyuo vyetu, na sasa hali ndio mbaya sababu wakufunzi wetu wameamua kushiriki siasa actively, hapo usitegemee vyuo (ambavyo ndio chungu cha kupika watu wenye uwezo wa kuhoji na kujadiri bila uoga mambo ya msingi katika jamii yoyote ile) kutoa maintellectual (nakumbuka tulikuwa tunajiita hivyo chuoni)
Ushahidi ni namna wanavyuo wetu wanavyoshiriki katika siasa, wale walio vyuoni na wale fresh from college, mategemeo ni kwamba hawa bado yale mambo mazito yanayofundishwa huko yako kwenye finger tips hivyo watuletee sisi tuliokitaa kwa muda mrefu hoja nzito ambazo kimsingi tutakubaliana nazo tu, sababu nyingi zina mantiki kubwa sana, lakini wapi? na wao wamekuwa watu wahovyo zaidi.
Muangalie mtu kama DR Kitilya Mkumbo, mkufunzi pale UDSM na ni kada kindakindaki wa CHADEMA, unategemea anaweza kuwapitisha wanafunzi wake kwenye tanuru la hoja zinazohoji msimamo na muelekeo wa kisiasa wa chama chake? au BAREGU? na hawa afadhali hawajaharibika, Muangalie Benson Bana, Profesa na Mkuu wa kitengo kikubwa tu, mtazame jinsi alivyokuwa biased kiasi kwamba anaonekana kama kichekesho anapoongea, wote hawa wamejishusha na kufikia viwango vya siasa za Lowasa, Cheap,unethical,self centered, currupted politics.
Na bado, hata bila kuangalia siasa uchwara zilivyoingia vyuoni na kuharibu mahala pale, hata kabla, mambo yaliyokuwa yakifundishwa huko siyo mambo yanayoweza kuzaa watu wenye uwezo wa kudadavua maswala haya kwa undani wake.
Na sikumbuki kuona mjadala matata japo juu ya sera za ujamaa,ubepali,democracy, n,k na hata wakufunzi waliokuwa wajijaribu kuteka wanafunzi kwa hoja zao walikuwa one sided.
Kwa mfano ufundishwe na Profesa Baregu alafu utegemee kutoka apo na mtazamo chanya wa aina yoyote ile kwa marekani, thubutu.
Ndio maana tuko hivi.