Dada yangu AshaDii sijui una umri kiasi gani ila unanifurahisha sana kwa michango yako mizuri. Nimepita kule kwenye jukwaa la fikra pevu na kusoma maandiko yako, kweli kuna mengi nimejifunza. Pamoja na hayo uliyomshauri kisana moja nami namuambia apitie thread za huko nyuma miaka ya kuanzia 2006 kuna wachangiaji na wachambuzi wengi ni hazina nzuri ktk jukwaa hili.
Sangarara, tofauti yake ipo katika hili... Kuwa "Open Minded" nafasi yake ipo kwa mhusika kuweza kupokea ideas/hoja mpya na kuzitafakari endapo anakubaliana nazo ama lah. Kuna mtu yupo "Closed Minded" haijalishi yupo makini vipi kukusikiliza, yeye kabla hata hajaanza kukusikiliza anakuwa kisha conclude ama judge kuwa hiyo idea/hoja haina maana wala uzito. Take note: si kila ambalo mtu husimamia ni sawa, with time watu hubadili misimamo tokana na sababu ambazo huwa msingi kwa wao kuweza kubadili hiyo misimamo.
Kukisimamia unacho amini, iwe kwa sababu za msingi ambazo unaweza kuzitetea. Unaweza ukawa unaamini hata iweje Anna Makinda ndiye raisi come 2015, lakini akaja mtu akakwambia si kweli hiyo imani yako na akakupa sababu zake za kupinga kwake hoja - hapo itapaswa uwe Open Minded ili kusikiliza hizo hoja na kuzipima kama kweli Imani yake ni ya msingi kuliko yako huku ukijaribu kufananisha na hoja zako zinazofanya uwe na msimamo huo ulio nao.
Au sijaeleweka nazidi kuchanganya?
Nimeona sehemu AshaDii kanitaja lakini mie siyo mchambuzi wa siasa. In fact, nilikuwa nim-PM ili anipe hints za kuandaa threads za mapenzi, urafiki na mahusiano maana kila niki-draft thread inaishia kati.
Kwa hiyo, mie siyo mchambuzi wa siasa, bali critical zaidi based on how I see things. Ukipitia threads zaidi napenda zaidi ku-inform wanajamvi kinachoendelea na pia kusikiliza maoni yao. Nasikiliza zaidi ya kuongea.
Kuna hii article hapa inaweza kukupa mwangaza jinsi ya kuwa mchambuzi mzuri au mpiga debe.
==============================================
Siyo umuhimu tuu. They have to. Mwanasiasa mzuri ni yule anayeweza kuchanganua/chambua/pambanua hoja. Hapa kwetu wanasiasa wengi siyo wachambuzi wa siasa. Wanasiasa wetu wengi wanaendekekeza siasa siasa za majitaka. Wamewaambukiza mpaka wafuasia wao.
Siasa za siku hizi zinanzia kwanza kwenye masilahi binafsi, baada ya hapo masilahi ya chama na na mwisho kabisa masilahi ya taifa. Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru, Dk. Mary Nagu alisema kuwa kama wenye jimbo la Arumeru wangemchagua mbunge ambaye si wa CCM, basi asingempa hatampa ushirikiano.
Huyu mama ni waziri na analipwa kwa kazi hiyo siyo kutokana na pesa inayotoka mfukoni mwa chama chake. Waziri kama huyo anaweza kuikwamua nchi, ikiwemo jimbo la Arumeru? Ukija kwa wabunge wengi, mazungumzo yao rasmi bungeni yanamfanya mtu ajiulize kwa nini kati ya Watanzania wooote tulionao, huyo huyo mbunge alifikia ngazi hiyo ya ubunge?
Hii yote imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wenye nchi wengi ambao badala ya kuwachambua wanasiasa wanashabikia wanasiasa mithili ya mashabiki wa soka. Matokeo yake tumekuwa na wanasiasa uchwara ambao wengi wao ni viongozi na wako kwenye nafasi ya juu kabisa ya kuamua mustakabali wa maisha ya hao hao wenye nchi.
Uomeona eh? AshaDii anasukumia wengine wakati yeye ni moja wa hao hao vinara.
Mie nishambook kwa ajili ya semina endelevu ya jinsi ya kuchambua nyuzi za MMU.
looks fine, japo bado nimebaki na maswali ngoja nijichunguze kidogo, nadhani nachanganya mambo mawili kwa wakati mmoja juu ya hitaji la huyu bwana kati ya kuwa "fair minded mchambuzi wa mambo ya kisiasa" au "fair minded mwanasiasa"
My thinking is, kama anataka kuwa mchambuzi maana yake amekwishaamua kutoside na upande wowote ule zaidi ya kutoa opinions kitu kinachonifanya nione haitaji kuwa na msimamo what so ever.
Nafikiri hapa ndipo ilipo demarcation kati ya politician na political analyst..sidhani pia kama ni dhambi kwa political analyst kuwa na anachokiamini (side) kwasababu as human being ni ngumu kuzuia...ni sawa na refa mtanzania ambaye sio mpenzi wa ama Yanga au Simba....ni ngumu kutokea. La Msingi anakuwa fair hata kukosoa kile anachoamini. Hili ndilo linalokosekana hapa JF miaka ya karibuni....
Katika siasa zetu ambazo tunaambiwa madhumuni ya chama cha siasa ni kushika dora, inakuwa ngumu sana kuwa na fair minded politicians, ambao wanashika dora watahakikisha wanawapinga wanaotaka kushika dora na wale wanaotaka kushika dora watawapinga wale wanaoshika dora hata katika mambo ya msingi kabisa ili mradi tu ama waendelee kushika dora ama wawaangushe wenzao.
Namna moja ya kuhakikisha tunakuwa na wanasiasa wanaosimamia majukumu ya kisiasa ya Taifa hili kwa manufaa ya Taifa, na sio wao au vyama vyao ni kuwa na bunge huru, namna ingine ni kuelimisha wananchi ili waelewe makujukumu ya kisiasa ni yepi ili, japo wakati wa uchaguzi waweze kupambanua na kuchagua wale wanaoweza kuyatimiza.
Lakini hata mazingira ya kisiasa yakiwa mazuri namna gani, sidhani kama ni sawa kutegemea kuwa na mwanasiasa fair, hasa hapa kwetu.
Habari Wakuu,
Kwa watu wanaopenda kutoa maarifa kwa manufaa ya wengine ningependa wanisaidie kwa hili; nahitaji kuwa mchambuzi wa masuala ya Siasa ila sijui njia itakayo niwezesha kuwa mchambuzi.
Msaada wenu tafadhali.
Kwa hapa kwetu ni vigumu kupata mwanasiasa anayepractice siasa then ukamtegemea awe pia political analyst na akawa fair... wengine si walipojaribu wamekolimbwa na tunakumbuka? Hata nyerere kuna wakati walitishia kumpoka kadi baada ya kuwasema, Sitta naye amekuwa akijaribu (though kwa motives zake) na cha moto ameshakiona kwani ilibidi tupate hata spika mwanamke bila kupenda wala kujiandaa...pengine tuangalie waliopo nje unaweza kukuta wachache....very few of them.....wapo watu kama kina Jenerali Ulimwengu pengine nikikumbuka mwingine nitarejea....Bongo kila kitu ni kipya na ni vigumu kukiandikia maana tupo unique kwenye mambo mengi.
Tuwe wakweli, wapiga kura wa tanzania wanauwezo wa kuchanganua mambo ya kisiasa?
hata wanasiasa wenyewe (majority) wanaelewa makujumu ya kisiasa? wanaweza kuchanganua maamuzi ya kisiasa?
wamepata op opportunity ya kulitumikia taifa katika mchakato wa katiba, unawaona wanachokifanya? wanashiriki?
Kuna hawa watu sikuhizi siwaoni humu ndani sijui wako wapi? ...
Wakitaka wanaweza tena sana tuu. Ni kutokana na wao kutofanya hivyo kumesabanisha kuwe na wanasiasa wasioweza kuchanganua mambo ya siasa.
Wapo wengi wengi tuu wakitaka wanaweza tena sana. Wengine mpaka maprofesa wa chuo lakini lakini wanashindwa kuchanganua au hata kupima madhara ya kauli zao.
Kwa nini hawashiriki?
looks fine, japo bado nimebaki na maswali ngoja nijichunguze kidogo, nadhani nachanganya mambo mawili kwa wakati mmoja juu ya hitaji la huyu bwana kati ya kuwa "fair minded mchambuzi wa mambo ya kisiasa" au "fair minded mwanasiasa"
My thinking is, kama anataka kuwa mchambuzi maana yake amekwishaamua kutoside na upande wowote ule zaidi ya kutoa opinions kitu kinachonifanya nione haitaji kuwa na msimamo what so ever.
Sasa nimeelewa kuwa ni wapi tumepishana. Hiyo para yako ya mwisho ni haswa inavyotakiwa kuwa... Nadhani ni kheri tukaenda step by step tukajaribu kuwekana sawa. Unaweza kuta kuwa pengine mimi ndiyo nachanganya habari hapa na nakosea mtazamo.
Naamini kuwa hata ukiwa Mchambuzi ambaye huegemei upande wowote kuna principles ambazo one has to hold. Kusimamia unacho amini, si tu kwa misingi ya kipi unaamini kati ya makundi mawili - nadhani hata pia kile ambacho unaamini in relation ya makundi hayo mawili.