Nifanyeje, nahisi Mume wangu ameniwekea mtego wa kishirikina

Nifanyeje, nahisi Mume wangu ameniwekea mtego wa kishirikina

Salaam wapendwa.

Niende direct kwenye hili suala linalonitatiza, mimi nimeolewa na huyu mumewangu tukiwa hatujuani sana kiundani wa tabia, yani hatujapitia Courtship before marriage.

Kwasasa tumejaaliwa mtoto mmoja na tuna miaka miwili ya ndoa. Tatizo ni kwamba kila ninachofanya siku yangu nzima, au kuongea popote na yoyote huwa anajua. Na sometimes huwa anarudia maneno yaleyale ambayo mimi niliongea na either mtu anaemjua or neno lilomkwaza ktk maongezi yetu mi na uyo mtu.

Kiufupi ukoo wao wana asili ya Uganga. Lakini kimuonekano wake sikutegemea kama na yeye anaweza kuwa amerithi hayo mambo. Kiukweli nakwazika sana yeye kunijua kwa kila kitu sina privacy kwake.

Naomba msaada na ushauri nifanye nini kujitoa kwenye huu mtego wa kishirikina. Nahitaji kuwa secure niwe huru nsaidieni jamani🙏😒.
Haya mawazo na imani za kishirikina zitavunja ndoa yenu bure. Fanya uchunguzi na utafiti badala ya kutoa hitimisho la haraka
 
Chukua kijiti simama kwenye mlango wa kutokea nje kwenu. Katikati ya mlango umegeukia ndani yani kisogo ndo kinaangalia nje halafu shika kijiti nyuma ya kisogo Anza kikivunja huku unanuia “nazuia mtu yeyote asinione” kila unapovunja kijiti nuia. Vunja mara saba na nuia mara saba kwishaa.
Asante sana🙏🙏🙏🙏🙏🙏❣
 
Ishi nae vzur, wanakuaga na msaada watu km hapo pale jambo baya limepangwa juu yako au ktu kbaya kinataka kutokea kwako

Pia usiogope kuongea nae khs yy alivyo

Mtangulize Mungu kwanza
Chukua huu ushauri.
 
Ni ndoa halali kabisa. Kama mume kuna ambayo anapaswa kuyajua na ambayo hatakiwi kabisa kujua. Dunia imebadlika mkuu. Kuna kuachana japo siombei, imagine mtu anajua hadi unachofkiria/ kukiwaza!!! Kweli!!! Yaani ajua mipango yako yote hadi maongezi ya wewe na familia yako!! Heh, mi siwezi jamani.
hakuna kiumbe hata majini hayawezi kujua unachofikiria, narudia hakuna
 
Sijawahi kucheat wala kuwaza hilo. Sipendi anavoniona kila nachofanya. I just need my privacy
Privacy ikusaidie nini,akati ulishanunuliwa kwa mahari,na umwili mmoja kaa kwa kutulia au nawew mtege
 
Unaanzaje kuolewa na mtu mshirikina? Kaa nao mbali washirikina, kama ukijiridhisha ni kweli amekufanyia mambo ya kishirikina vunja ndoa dada, Washirikina sio watu wazuri kabisa. Ni washenzi tu.
 
Mwamba kasha install mobile tracker kwenye Simu yako na ameificha huko kwenye bila vault ( Ina muonekano wa saa).
 
Back
Top Bottom