kibla matata
JF-Expert Member
- Mar 3, 2020
- 412
- 380
Habari za mida hii wapendwa
Mimi ni wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto wawili. Katika makuzi yangu tokea Primary School nilikuwa naishi kwa style fulani ya kujitenga tenga na wenzangu. Ikafika kipindi wenzangu niliokuwa nikisoma nao shule wakawa wananiita mimi mchawi.
Kwa mfano labda kama kuna kitu shuleni ambacho kinahusisha wingi wa watu mimi lazima nitatoroka shuleni au kama zile group discussions basi mimi lazima nitajitenga. Nilikuwa sipendi kuwa na rafiki kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anapenda kuwa karibu na mimi lakini ilifika mahali hata akija nyumbani kuniuliza nilikuwa namkwepa.
Sasa wadau tatizo limekuwa sugu hadi sasa hivi nimekuwa sina rafiki hata nikisema nijichanganye kwa watu nakuwa sijisikii kujiamini. Kuna muda nasema labda nianze kushabikia mpira lakini sina muda navyo hivyo vitu kwa kifupi hadi saivi sina rafiki hata mmoja.
Kuna wengine nawaona wanaoenda kuwa karibu na mimi lakini nimekuwa mtu wa kujitenga nao. Kwa kifupi nikienda kazini ya huko nayaacha huko huko nikirudi nyumbani napenda kujifungia ghetto kuangalia movies kuchati nikitoka mgahawani narudi tena mbio nyumbani. Bahati nzuri nyumba niliyopanga niko peke yangu yule mama kashanizoea naweza kukaa na watu nakuwa mpenzi msikilizaji tu siongei neno hata moja, wakinisemesha najibu short ama nakuwa mkali.
Naombeni ushauri jamani, kuna muda nawaza hadi nafika mbali. Kwanini nimekuwa mtu wa kujitenga?