Nifanyeje nipende mpira wa miguu

CUBICBOY

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
306
Reaction score
223
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira
 
Wala usihangaike mkuu.kuna kitu kinaitwa hobbies,hiki kitu huwa hakilazimishwi.binafsi kama wewe nilijitahidi sana kutaka kuupenda huu mchezo but wapi,nakesha nikiangalia match kubwa zote za timu zinazopendwa sana mitaani ila hakuna lolote nililovuna.yaani ilikuwa mechi ikiisha nusu saa tu ukiniuliza kilichokuwa kinaendelea uwanjani sijui hata nijibu nini mwisho nikakubali kwamba hobbies yangu ni kuangalia movie na kusikiliza muziki{sio kwenda club}nasikiliza tu home na huwa na-enjoy kweli kweli yaani hunitoi hapo.
 
dah kweli unakosa raha.. michezo inapunguza sana stress hata kama huichezi kuishangilia tu raha...
 
kwa mfano mechi za usiku najitahidi Sana kuzifuatilia najikuta nasinzia ila wenzangu wanashangilia kweli
 
kwa mfano mechi za usiku najitahidi Sana kuzifuatilia najikuta nasinzia ila wenzangu wanashangilia kweli
Utajiumiza bure kaka tafuta kile unachokipenda.kila la heri
 
Endelea kuangalia tuu huenda ukaanza kuipenda
 
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira

Ingia you tube andika messi ,, then chukua ratiba ya La Liga angalia mechi zao... Mpira utaupenda
 
kwan ww boss ni mshabiki wa timu gan ngoja tuanze na hilo.. kisha kama ww mshabiki wa arsenal bora endelea hvyo hvyo kutoupenda ukija kupenda na tim yako pasua kichwa hyo arsenal utapata ugonjwa wa moyo bure ww endelea kupenda movie na music vitu vya recorded lakn mpira kitu cha live bira chenga
 
Acha kupenda mpira wa miguu. Jitahidi uangalie basketball tu. Basket burudani tele alafu magoli mengi. Mpira unaangalia dk 90 hamna hata goli.
 
Pole sana mkuu hobbies zako ni zangu ila mpira naupenda sana


Mnakosa kipunguza stress
 
Mkuu nitumie njia gani au we ulifanyaje angalau nipate kulifresh
Kwanza unajua football inavyochezwa?? Kama ndio safi, kama hapana tafuta mtu akuelezee.

Ukishaelewa au kama unaelewa, tafuta shabiki wa timu yeyote anae elewa hiyo timu na akusimulie mchezaji au wachezaji fulani wa hiyo timu uwezo wao pamoja labda na kocha.

Pia akuelezee na mifumo pamoja na timu hasimu za hiyo timu anayoipenda.

Hayo hapo juu yafanyike kabla ya kwenda kuangalia timu hiyo ikicheza.

Sasa kaangalie mechi moja ukiwa na huyo muelekezaji wako mkaangalie hiyo timu anayoipenda na awe anakupa dondoo ya kinachoendelea.

Pia akuelezee kuhusu ligi na umuhimu wake na mafanikio yanayopatikana timu ikishinda kombe la ligi fulani.

Kama atakua muelekezaji mzuri basi utaanza kuifuatilia hiyo timu kila ikicheza huku ukilinganisha na timu zingine na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla huku ukifuatilia zile dondoo alizokupa.

Nakuhakikishia utapata timu ya kuishabikia na sumu itakuingia tu inapofungwa na utaanza kulia kabisa ila usijinyonge.

Mfano mie nilijikuta naishabikia Manchester United hapo zamani na kuna baadhi ya wachezaji walinivutia. Walipoondoka au kuondolewa nilikasirika sana. Nikasoma article moja ilimhuhusu mchezaji mmoja aliitwa Makelele akinyanyasika wakati yuko real madrid, akahamia Chelsea nikawa namfuatilia ili nione huo uwezo wake.

Nikawa kila mechi ya Chelsea lazima niangalie....hapo nikajikuta nimehamia kuishabikia Chelsea mwishowe nikavutiwa na Mourinho. Basi nikabaki huko hata Makelele alipoondoka.

Naamini mchango wangu utakusaidia walau kiduchu.
 
Wakuu habarini, huwa naona watu wakishangilia kwa furaha wengine hata kula Hawali kisa mpira nifanyeje niupende mpira
Wala usijishughulishe sana, we penda hata siasa inatosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…