Nifanyeje nizoeane na majirani?

Ni bora kabisa kujitenga. Kadri unavyokuwa mbali na wengi,ndivyo unavyokaa mbali na matatizo. Kadri unavyokuwa na marafiki wengi ndivyo unavyokaribia kupata matatizo mengi

Mimi sitaki kuanzisha nao urafiki, nataka tu ule ujirani mwema na kujuana kwamba huyu anakaa mtaa huu na kukiwa na tukio lolote basi kunakua na ule ushirikiano wa kijirani. Sio mazoea ya ajabu ajabu.
 
Kwa kuwa wengi wenu wamezungishia fence nyumba zao (hata nahisi ni fence za kuta) basi jitoe Muhanga siku moja wewe simama nje ya fence ya nyumba yako..kila jirani akipita kwenye gari yake mpungie mkono na kumsalimia kwa sauti..fanya hivyo kama wiki nzima hivi watakuzoea maana hiyo kwao itakuwa kitu cha ajabu na pekee lakini ndio itauwa brand/identity yako hapo mtaani...watakuita "yule jamaa mpungia mkono" hahahaah!
Nashukuru mkuu, hili na mimi nimeliona sema sasa changamoto ni jinsi ya kujizoesha kwa watu usiowafahamu. Ningekua mtu wa ulabu labda ingesaidia maana wengi ningekutana nao ila sasa mimi ni mzee wa
 
Ondoa Ego jumapili toka nenda kwa jirani kusalimia piga stori mbili tatu rudi nyumbani. Mimi jumapili huwa nafanya hivyo.
 
Hata mimi nilikumbwa na hali kama yako kwa kipindi cha miezi 6. Nilipoanza kusali Jumuiya na siku moja wakaja kusali kwangu yaani nilipata marafiki wengi mpaka wakaniunganisha kwenye group lao la whatsup
 
Omba kiberiti asubuhi na jioni kaulize kama wanauza kuku au maziwa mgando huku ukiwaita "jirani salama huku?".
Jitahidi uoe na uwe na watoto, acha kukaa kihuni.Watoto huwa hawana mbwembwe ni mwendo wa kucheza na punde utaletewa kesi ndo mtajuana zaidi
 
Anza kusali Jumuiya utawapata majirani wengi sana
 
Kama hakuna ujirani mbaya basi kuna ujirani mwema.Hayo mazoea ya kuforce unayotaka yatakuja kuleta uadui.Ushauri wangu Relax.Majirania sio suluhu ya matatizo yako.Wengi tayari wanakujua na hio inatosha.Hayo mengine taratibu tu mtajuana.Je una watoto wadogo?Kama unao basi let them find their friends kwa namna yao.
 
[emoji3516]
HAO MAJIRANI WAWILI WA UPANDE WA KULIA NA KUSHOTO UNAOFAHAMIANA NAO WANATOSHA SANA-

VINGINEVYO,
WEWE UNATAFUTA KERO ZA WASWAHILI ZA KUWA NA MAZOEA YA HOVYO NA MAJIRANI!!!
 
story of my life
 
Umesubiri sana kujitambulisha mwaka umepita? Unaweza hata kugonga kujitambulisha na kazawadi kadogo na mubadili mawasiliano.Au mkikutana njiani tabasamu na wasalimie,jitambulishe.Hujui kesho utakutwa na nini!Jirani yako ndo mtu wa kwanza kukusaidia.Sio lazima ujuane na wote bali wachache wanatosha.
 
hapo mwisho ulipomalizia, please ainisha hizo hatari za kuishi bila kufaham neighbors
 
Utashangaa jirani na mbali zaidi wote wanakufahamu wanakuangalia tu. Nikupe incident tatu zimetokea nikajua kumbe watu wanakuchora tu
1.niliharibikiwa na gari mbali kidogo na home nikachukua bajaj kurudi home kutafuta alternative, yule wa bajaj akaanza kukata mitaa nikamuuliza wewe unajua unapoenda? akasema blaza si unakaa pale pako hivi na hivi...nikaishiwa pozi
2.Nimeenda dukani hardware kununua vitu sasa nataka mtu apeleke nyumbani mimi naenda kazini, kaitwa bodaboda akapewa nampa maelekezo ananiambia aah blaza si kwenye kona pale hivi na hivi!
3.wengine nimekuta masela wanaziba mashimo barabarani wakaniwahi blaza wa pale hivi na hivi tutoe leo pozi likaisha
Yaani watu wote wanakufahamu unapokaa,unaendesha gari gani etc ila unapita huongei na mtu wanakuangalia tu. siku moja moja shusha kioo wasalimie watu mtaani.
 
hapo mwisho ulipomalizia, please ainisha hizo hatari za kuishi bila kufaham neighbors
Sasa mkuu janga lolote likitokea wa kwanza si jirani zako? Mfano moto huku uswazi wazimaji si majirani maanake fire hadi ifike huko ni majivu. au umeanguka ghafla nani atakupeleka hospitali,mkeo anaweza kupata shock akabaki analia tu. Majirani ni watu muhimu sana.
 
You are right
 
Majirani huwa wanakuja automatic , nani aliyetangulia kuja hapo mtaani? Kama wamekukuta wakati wanaaza ujenzi hamjafahamiana? Kama mkristu shiriki misa za ujirani za kila jumamosi au j2 kama ni muislamu shiriki ibada za msikitini za mitaani hapo mtafahamiana na majirani.

Pili hamasisha kufanya mambo ya kimaendeleo ya mitaani eg ulinzi shirikishi ,ukarabati wa barabara vitawaweka karibu majirani.

Halafu usiwe "KAX" sana siku moja moja act kama mtu aliyepigika ili majirani wakuchukulie wa kawaida sio kila siku gari tinted vioo juu full ac watu watakuogopa.
 
Kuna kijana mdogo sana amehamia hapa mtaani nyumba nzuri fensi nzuri, pesa anayo ila alijisahau akawa na madharau, Yuko bize na mambo yake tu, kuna siku alivamiwa na majambazi usiku akapiga kelele za kufa mtu hakuna aliyetoka, wezi wakachukua vitu vya thamani, asubuh ndo watu wanaenda kumpa pole.

Alijifunza siku hizi ndo anasalimia watu barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…