Nifanyeje nizoeane na majirani?

Nifanyeje nizoeane na majirani?

Tofauti na huko mbele, huku kwetu ukimkaribisha jirani kwako pamoja na kufaidika kwa fadhira zako, anatumia ku-scan nyumba yako nje ndani badala ya siku kadhaa unapata ugeni wa majambazi usiku mwigi.😀
Hahahha anakutumia wazee wa kazi
 
Kuna kijana mdogo sana amehamia hapa mtaani nyumba nzuri fensi nzuri, pesa anayo ila alijisahau akawa na madharau, Yuko bize na mambo yake tu, kuna siku alivamiwa na majambazi usiku akapiga kelele za kufa mtu hakuna aliyetoka, wezi wakachukua vitu vya thamani, asubuh ndo watu wanaenda kumpa pole.
Alijifunza siku hizi ndo anasalimia watu barabarani
Hahahahah alijiona star wakati kapanga uswahilini?
 
Wewe sijui ni wangapi.. Unatoa ushauri huu wa jumuiya.. Upo sahihi kabisa kabisa.. Jumuiya ni kitu muhimu sana sana.. Nimepitia situation za kuhamia mitaa ya vigogo aisee kabla sijajiunga jumuiya nilijuta kuishi huko. Ila baada ya kujiunga mimi ndie m.kiti wao.. Haijalishi mavyeo yao Serikalini au wapi? Maisha yamekuwa mazuri yenye amani na mshikamano mkubwa.

Walioanzisha jumuiya aisee. Mungu asiwasahau katika ufalme wake.
Utakuwa mtu wa ibada sana bila shaka
 
Nilifahamiana na jirani yangu salun baada ya mwaka tena bint yangu mdogo ndio alitutambulisha, tukaelewana Sana si Kwa kutembelea Ila ikitokea kitu mtaani tunaambizana, kuna siku niliona turubai nyumba ya tano au ya sita kutoka kwangu nikavaa kanga nikaenda japo na wenyewe siwajui nikaingia ndani na kuuliza hilo turubai kuna nini? Wakanijibu kulikuwa na msiba siku tatu zilizopita nikawaomba msamaha kwamba sikujua wakajibu hata jirani yako Hana habari maana hatujamuona nilipitia nikamuonyesha turubai alistuka nikamweleza akaenda kutoa pole. Napenda MAISHA haya tujuane shida, Raha wabiki nayo wenyewe
 
Mtu mwenye uwezo huwa hahudhurii hivyo sijui vi party sijui visherehe gani.. Uswahilini ukiandaa shughuri huhitaji kualika mtu. Watajileta hata kabla ya muda.. Ila hiyo mitaa hakuna mtu anatime na hivyo vitu. Zaidi utashitakiwa kwa kuleta kelele na wezi.
Hahahaha..that's true
 
Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kirudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.

Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha, na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.

Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?
Njia rahisi ni kutembelea vijiwe ambavyo unadhani utakutana nao! Kama kuna Car wash mtaani jimix hapo weekend nunulia vijana soda mpige soga! Kama kuna ka duka mahali unaweza pata hata mtindi ukawa unapiga piga story na watu maeneo hayo! Kama ni mtu wa dini jiunge na jumuiya uwe unakutana na wenzio kila weekend.
 
I don’t pretend to be alone,
I live my life to the fullest,

Binadamu ni wanafki na hao hao ni vyanzo vya matatizo

Hao hao unaotengeneza mazingira ya kuwasogelea wanaweza wakakuundia jambo ukashangaa na roho yako,

Sina mazoea ya kukaribisha watu Kwenye maisha yangu kwa sababu ya ujirani ,
Watu wanaflow kwenye maisha Natural kama nature inawahitaji muwe karibu mtakuwa bila kutumia nguvu.
Being genuine, being you.
Watu wanaogopa msiba kwamba utazika mwenyewe, mimi nakataa. Mtu anaenda kwenye msiba kwa sababu ya heshma ya marehemu na sio vinginevyo, haya mengine ni 'socialist way of life' ni uamuzi wako na 'perception' yako.
Naonaga misiba ya kimagharibi kwenye runinga, unakuta padri/mchungaji na wanafamilia ndugu na watu wa karibu hawazidi 20. Ukiona msiba una watu wengi basi marehemu ni mtu maarufu.
Muda unakwenda na maisha yanabadilika kwa kasi sana, tamaduni zingine nazo zitabadilika pia. Mfano sasa hivi serekali inataka watu wakazikwe kwenye makaburi ya uma na sio kwenye miji yao
 
Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kirudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.

Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha, na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.

Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?
msizoeane sana, jitahidi ukikutana nao salimia kwa unyenyekevu, ikiwezekana unashuka kwenye gari unawasalimia unaendelea na mmbo yako, hakikisha hamzoeani sana,na ukisikia kwa jirani kuna tatizo nenda kamsaidie endelea na mambo yako!!
 
Tatizo tunaogopana sana.
Watu wanaweza wakakuogopa kwa class uliojiweka ila ukiwa bro mchangamfu hata vijana watakupenda tu hapo mtaani! Weekend egesha hata car wash, tia nao strory mfano kuna mwana ni engineer life safi ila anachezaga draft na wana kitaani tu on weekends. Anazungusha kahawa bill kwake maisha yanaenda na anajulikana freshi!

Watu wakuzoee ila sio ile sana mpaka mtu anajua unafanya kazi wapi! Anajua una asset au biashara gani beyond ambavyo alitakiwa akufahamu inaletaga dharau at last. Mie hiki ndio sipendagi
 
Eid ya keshokutwa kagonge maget yao uwaalike hata wasipokuja watakuona na watauthamini utu wako kwahiyo hata ukiwa na shda unaweza kuwaomba msaada au wao kukuomba msaada
 
Watu wanaweza wakakuogopa kwa class uliojiweka ila ukiwa bro mchangamfu hata vijana watakupenda tu hapo mtaani! Weekend egesha hata car wash, tia nao strory mfano kuna mwana ni engineer life safi ila anachezaga draft na wana kitaani tu on weekends. Anazungusha kahawa bill kwake maisha yanaenda na anajulikana freshi!

Watu wakuzoee ila sio ile sana mpaka mtu anajua unafanya kazi wapi! Anajua una asset au biashara gani beyond ambavyo alitakiwa akufahamu inaletaga dharau at last. Mie hiki ndio sipendagi
Kuogopana ninakozungumzia ndio ile ukikaribisha jirani ataleta wezi,mara utalogwa,wataleta dharau yaani binadamu tunaogopana sana
 
Don't pretend like you're alone in this world, you're not alone at all. Na kuna maana yake ya wewe kuumbwa miongoni mwa wanadamu wenzio.
Compatibility!!!
Binaadamu tumeumbwa tuishi kijamii na nature imewekwa tukae hivo. Hakuna mtu asiyemuhitaji mwenzie hadi uone kua majirani si kitu au ushindwe kuingiliana nao.

Trust me nature inaweza kukupiga tukio moja tu hadi wewe mwenyewe ukarudi kwenye mstari... Mtoa mada kabla nature haijachukua njia zake get out na usalimiane na watu usije jutia. Tumeumbwa kama vidole vya mkono kidole kimoja hakiwezi jitenga pekee yake halafu kiseme kinaweza kutengeneza ngumi.

Kidole gumba ni kikubwa ila kinategemea vidole hivi vidogo kushirikiana ilie watengeneze ngumi imara. Hata kama una uwezo mkubwa mate hado hao watu wa chini unawahitaji kuliko kawaida.
Kama vipi na huku jamii Fulani atokemo ili asiingiliane na watu kwa stori ama kubadilishana stori mbili tatu.
Yeye si anaweza kuishi bila watu tuone Sasa.ulaya watu wanaugua Sana sijui Nini ule ugonjwa may be sonoma.mtu Ana socialize mtandaoni Ile live kabisa na watu hakuna kitu. Na binadamu tunahitaji binadamu wengine Ile live la sivyo ufanye hata mapenzi kidigital tuone.fanya party YouTube tu view tu comment,
Hata kanisani hudhuria tu kwa tv sadaka tuma mpesa.
Funga mdomo wako bila kuufungua kwa binadamu mwenzako tuone Kama wewe ni peculiar species.
Kuna sex phone,pia yaani life ni watu.
Mie nashukuru napita ni salamu tu na karibia wote ni mageti, nimekuwa wa kwanza kuleta umeme huu mtaa,simu wanaleta nawachajia,wakiwa wanachomelea mageti Yao umeme nawapa sema wananunua luku waliyoitumia wanaiweka wanatumia,
Maji tunapata once per week Nina tank wasio na tank wakiishiwa wananiomba nawapa.binafsi nafurahi Sana kuishi vizuri na kusaidiana na majirani vidogo vitu. Ila tu mazoea sio Sana kivile,yupo nikiyekuwa naazima jembe na ngazi, jembe baadaye nikanunua.
Mie ni watu bila watu mie sipo
 
Utashangaa jirani na mbali zaidi wote wanakufahamu wanakuangalia tu. Nikupe incident tatu zimetokea nikajua kumbe watu wanakuchora tu
1.niliharibikiwa na gari mbali kidogo na home nikachukua bajaj kurudi home kutafuta alternative, yule wa bajaj akaanza kukata mitaa nikamuuliza wewe unajua unapoenda? akasema blaza si unakaa pale pako hivi na hivi...nikaishiwa pozi
2.Nimeenda dukani hardware kununua vitu sasa nataka mtu apeleke nyumbani mimi naenda kazini, kaitwa bodaboda akapewa nampa maelekezo ananiambia aah blaza si kwenye kona pale hivi na hivi!
3.wengine nimekuta masela wanaziba mashimo barabarani wakaniwahi blaza wa pale hivi na hivi tutoe leo pozi likaisha
Yaani watu wote wanakufahamu unapokaa,unaendesha gari gani etc ila unapita huongei na mtu wanakuangalia tu. siku moja moja shusha kioo wasalimie watu mtaani.
Mkuu watu ambao hatuna mazoea na wengine huwa tunadhani hawa wengine hawatuoni kumbe wanatuchora tuuu.

Ulichosimulia kimenikuta na mimi...


Kuna siku nilienda dukani kuulizia kitu flani hapa ahpa mtaani,sasa nikaambiwa kile kitu hakipo,

yule muuzaduka kumbuka kuwa simjui jina ila tunajuana kwa sura tu

Basi wife akaenda baadae kuulizia tena kile kitu alafu alikuwa amevaa nikabu(ninja) katika duka lile lile.

Muuza duka akamuambia "hiki kitu sina na mumeo katoka kuulizia muda sio mrefu"

Wife alichoka akasema wamejuaje kuwa mimi na wewe ni wanandoa wakati ni mara chache mno huwa tunafuatana tena tukifuatana basi tunaenda safari na sio kuzunguka hapa mtaani na ajabu zaidi wife huwa anavaa ninja mara nyingi lakini bado wakamjua kwamba huyu ni mke wa safuher.

Hivyo mtaani watu wanakuchora tuu unaweza dhani hawana deta zako zozote vile wanavyojikausha ukiwa umekutana nao.
 
Back
Top Bottom