Tangu nimehamia hapa mtaani ni takribani mwaka sasa umekatika. Mtaa ninaoishi ni nje kidogo ya mji ambapo watu wamejenga nyumba zao wamezungusha fensi na mageti. Pia wengi (pamoja na mimi) ni wafanyakazi ambapo mara nyingi ni watu wa kutoka asubuhi na kirudi jioni wakiwa ndani ya magari yao.
Sasa leo nimekaa nikatafakari, nikagundua kuwa zaidi ya majirani niliopakana nao upande wa kushoto na kulia, hakuna jirani mwingine ambaye walau hata namjua kwa jina. Hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati yangu na majirani zangu, hakuna tukio lolote linalotukutanisha, na hata ikitokea mtu akapata tatizo, sidhani kama kuna mtu atajitokeza kusaidia.
Mimi naona kama hii hali sio nzuri ila nashindwa kujua nifanyeje ili kujenga ujirani mwema, hasa kwa hawa majirani wa mbali kidogo nyumba ya tatu ya nne huko?
Mimi nilihamia sehemu sina jirani wa karibu kabsa. Nipo kama kisiwa yani nmezungukwa kulia kushoto mbele nyuma ni viwanja tupu na jirani wa karibu yupo mita 30 halafu nipo ndani ya ukuta....
Nikawa nikichomoka asubuhi narudi saa 4 mpaka 6 usiku.
Kumbe wajuba wananichora....
Nikapigwa tukio la kwanza nikachomoa....
Nikapigwa la pili nikachomoa....
Nikapigwa la tatu wakaniweza wakaniibia laptop na vitu vingine vidogo....
Baada ya hapo nikatafakari maisha nayoishi nikaona ni ubatili mtupu....
Hatua nilizochukua.
1. Nikaongeza kuhudhuria jumuiya yani hata nirudi home chakari saa 10 asubuhi saa 12 nipo jumuiya ..
2. Siku moja moja nikawa nakunywa mtaani na hata nisipokunywa nikawa nakaa kwa mangi nanunulia hata watu vichungu...
3. Kuhudhuria shughuli za kijamii misiba sherehe n.k
4. Vuta demu home... Wanawake wana nguvu za kuvuta majirani acha tu mzee...
5. Jua boda boda kadhaa .....
Baada ya hapo nina miaka miwili sijawahi vamiwa tena....
Na sasa nina majirani watatu wa karibu kabsa.....
Na mtaani najua almost kila mtu atleast kwa jina....
Kuishi kivyakovyako sio kabsa... Utajifia gheto watu wasijue.