Niffer, Amefanikiwa Kukusanya Shilingi Milioni 111 Ndani ya Siku Mbili Kuokoa Maisha ya Mwanafunzi wa CBE, Najath Ibrahim

Niffer, Amefanikiwa Kukusanya Shilingi Milioni 111 Ndani ya Siku Mbili Kuokoa Maisha ya Mwanafunzi wa CBE, Najath Ibrahim

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Jitihada za kibinadamu zimeleta matokeo makubwa baada ya mfanyabiashara na mshawishi wa mitandao ya kijamii, Niffer, kufanikisha ukusanyaji wa Shilingi milioni 111 kwa ajili ya matibabu ya mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Najath Ibrahim, anayesumbuliwa na tatizo la figo.

Najath, ambaye figo zake zote mbili zimefeli, alikuwa akihitaji kiasi cha Shilingi milioni 40 kwa ajili ya kufanyiwa upandikizaji wa figo. Baada ya kuona kasi ya uchangishaji iliyokuwa ikiendeshwa na kikundi cha Mwanachuo Family ikisuasua, Niffer aliamua kuchukua uongozi wa kampeni hiyo ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa fedha.

Matokeo ya hatua hiyo yameonekana ndani ya siku mbili tu za kampeni hiyo mpya, ambapo kiasi kilichopatikana kimevuka lengo la awali kwa zaidi ya mara mbili.

Uamuzi huu wa Niffer unaonyesha nguvu kubwa aliyo nayo katika jamii na namna anavyoweza kutumia ushawishi wake kuleta mabadiliko ya haraka. Kazi aliyoifanya si tu kwamba imefanikisha gharama za matibabu ya Najath, bali pia imetoa matumaini mapya kwa familia na jamii inayomzunguka.

Hatua hii inaendeleza mfululizo wa matendo yake ya hisani, ikiwa ni pamoja na kujitolea kumsomesha mtoto wa mfanyabiashara wa ndizi wiki iliyopita na kumchangia DJ Choka Shilingi milioni 1 kwa ajili ya matibabu ya figo.
1789643382799.png

1789643405317.png

1789643426217.png
 
Zamani wazee ndio walikuwa wakiumwa maradhi ya Figo ila siku hizi vitoto vidogo kabisa zama zinabadilika.

Kinachonisikitisha hizo pesa zote zinaenda serikalini kwann serikali isijitolee kugharamia matibabu ya watu kama Hawa?
 
Acc zozote aswa za watu binafsi bila auditing lazima ubadhirif utokee
 
Back
Top Bottom