Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mfanyabiashara maarufu Jennifer Jovin, anayefahamika kama Niffer, ametoa majibu yake baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kumtaja katika hotuba yake ya hadhara akitaka afuatiliwe na kueleza nani aliyempa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia ajali ya kuporomoka kwa gorofa la Kariakoo.
Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
Kupitia majibu yake yaliyojaa shukrani na kueleza nia njema, Niffer amesema:
"Kwanza kabisa, Alhamdulillah, namshukuru sana Allah kwa kunipa nafasi ya kuiona siku ya leo. Kwa kweli, ni jambo kubwa sana kwangu kuona Waziri Mkuu wa nchi yangu ametaja jina langu mbele ya hadhara ya watu mashuhuri. Hii ni ndoto kubwa iliyotimia kwa ulimwengu wa roho."
Niffer ameeleza kuwa nia yake kuu ilikuwa kusaidia wahanga wa ajali hiyo, akisisitiza kuwa hakujua sheria zinazohusiana na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya mafaa kama hayo. Ameeleza:
"Nilikuwa tayari tangu mwanzo kutoa ushirikiano kwa Serikali na jamii kwa ujumla. Niliomba muongozo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza zoezi hili. Ninaamini nia yangu haikuwa mbaya, na kupitia changamoto hii, nimeona umuhimu wa kuwa na taasisi inayotambulika rasmi, Niffer Foundation."
Waziri Mkuu Majaliwa, wakati akizungumza eneo la Kariakoo, alisisitiza kuwa hakuna mtu anayepaswa kuchangisha fedha bila kibali maalum kutoka serikalini na akatoa agizo kwamba Niffer atafutwe ili aeleze ni nani aliyempa mamlaka hiyo.
Soma, Pia: Jeshi la polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
Baada ya agizo hilo, taarifa zilitolewa kuwa Niffer ameshapatikana na yuko tayari kushirikiana na mamlaka husika.