Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo

Kwani huyo nifa ana wadhifa gani maana wengi naamini hatumfahamu mwenye CV yake Tafadhali.
Huyu wa kushoto mwenye light blue top
Screenshot_20241118_143653_Instagram.jpg
 
Mfanyabiashara maarufu Jennifer Jovin, anayefahamika kama Niffer, ametoa majibu yake baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kumtaja katika hotuba yake ya hadhara akitaka afuatiliwe na kueleza nani aliyempa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia ajali ya kuporomoka kwa gorofa la Kariakoo.

Kupitia majibu yake yaliyojaa shukrani na kueleza nia njema, Niffer amesema:

"Kwanza kabisa, Alhamdulillah, namshukuru sana Allah kwa kunipa nafasi ya kuiona siku ya leo. Kwa kweli, ni jambo kubwa sana kwangu kuona Waziri Mkuu wa nchi yangu ametaja jina langu mbele ya hadhara ya watu mashuhuri. Hii ni ndoto kubwa iliyotimia kwa ulimwengu wa roho."

Niffer ameeleza kuwa nia yake kuu ilikuwa kusaidia wahanga wa ajali hiyo, akisisitiza kuwa hakujua sheria zinazohusiana na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya mafaa kama hayo. Ameeleza:

"Nilikuwa tayari tangu mwanzo kutoa ushirikiano kwa Serikali na jamii kwa ujumla. Niliomba muongozo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza zoezi hili. Ninaamini nia yangu haikuwa mbaya, na kupitia changamoto hii, nimeona umuhimu wa kuwa na taasisi inayotambulika rasmi, Niffer Foundation."

Waziri Mkuu Majaliwa, wakati akizungumza eneo la Kariakoo, alisisitiza kuwa hakuna mtu anayepaswa kuchangisha fedha bila kibali maalum kutoka serikalini na akatoa agizo kwamba Niffer atafutwe ili aeleze ni nani aliyempa mamlaka hiyo.

Soma, Pia: Jeshi la polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya agizo hilo, taarifa zilitolewa kuwa Niffer ameshapatikana na yuko tayari kushirikiana na mamlaka husika.
Kwahiyo niffer anatuaminisha hajakamatwa na kwamba polisi wamemdanganya waziri mkuu?
 
Huyu binti

Ni muislamu?
 
Ignorance of the law does not afford any excuse for any act or omission which would otherwise constitute an offence unless knowledge of the law by the offender is expressly declared to be an element of the offence.

Kutokujua sheria siyo kinga, hakuna anaejali nia yako ni njema au mbaya kitakachoangaliwa ni umefata sheria au laa.
 
#UPDATES Wakati zoezi la kutoa misaada mbalimbali likiendelea Kariakoo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu. Dkt. Jim James Yonazi amewataka wananchi kuwa makini kuhusu michango inayoendeshwa ya kuwasaidia wahanga ambapo ameweka wazi kuwa akaunti inayokusanya michango ya fedha ni moja pekee na sio nyingine.

Dkt. Jim James amesema michango yote inayohusu tukio hilo inakwenda kwenye akaunti maalum ambayo ni ya serikali #EastAfricaTV
 
Back
Top Bottom