Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mfanyabiashara na (influencer) Niffer hivi karibuni amkataa shabiki aliyejichora tattoo yenye sura yake, huku akisisitiza kuwa hatatoa msaada wowote wa kifedha kisa tu mtu amejichora picha yake.
Tukio hilo limekuja kufuatia kusambaa kwa picha za shabiki huyo aliyetumia tattoo kama ishara ya upendo na kumkubali msanii huyo.
Ingawa shabiki huyo alilenga kuonyesha heshima na mahaba ya dhati, Niffer alichukua msimamo tofauti kabisa kwa kuweka wazi mipaka yake kupitia ujumbe aliochapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Niffer ameeleza kuwa, akiwa Muislamu safi asiye na tattoo yoyote mwilini mwake, hawezi kuunga mkono wala kuhamasisha kitendo kinachokwenda kinyume na misingi ya imani na maadili yake.
Aliongeza kuwa kupokea kitendo hicho kwa furaha kungewapa picha isiyo sahihi jamii na mashabiki wengine kwamba ni jambo linalofaa kuigwa.
Mjadala huo ulipata mwelekeo mpya kwenye sehemu ya maoni wakati mfuatiliaji mmoja alipoeleza kuwa huenda shabiki huyo alifanya hivyo akitarajia kupata msaada wa fedha pengine TSh Milioni 2 za kuanzia maisha. Niffer alijibu kwa ukali na uwazi:
"Siwezi kutoa hela kisa mtu amechora tattoo yangu bro, siendeshi maisha yangu hivyo."
Kupitia kauli zake, Niffer amewataka mashabiki wake, hasa vijana, kufanya maamuzi kwa kuwaza kwa kina kabla ya kuchukua hatua za kudumu miilini mwao. Amesisitiza kuwa upendo wa dhati kwake haupimwi kwa tattoo au kutarajia malipo ya fedha, bali kwa dua, kumtakia mema, na kumpa support kwenye kazi zake.