Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Mkuu ukisema biashara unayoifanya nitakuwa nimekutoa kwenye list ya watu wenye roho za kimasikini.. wano amnini wenhine wakifanikiwa wao watafeli.., karibu share nasi!!
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.
 
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.
Duhh mkuu 5mil faida yake 250,000/=? Hapa risk zikitokea inakuwaje?

Labda sikaelewa vizuri , vyema ukanielewesha
 
Ww si mfanyabiashara unataka kufata mkumbo tu
 
[emoji120][emoji120]
 
Sawa. Mkuu

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Nakushauri omba mawazo ya biashara lakini usianze kupanga hadi kiasi cha faida cha mil 2 kwa mwezi kama faida ghafi. Utakwama kabla hujaanza

Hakuna biashara ya hivyo labda ukajumue cocaine
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.

Soko lako lipo wapi mkuu?
 
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.

Million 5 namimi ninayo mkuu nipe connections namimi nitoke asee
 
Kweli..
Ila kumbuka biashara nyingi pia ni huduma, mfano: shule, hospitali, usafirishaji, mighahawa, ushonaji, vinyozi/ususi, nk...

Kanisa ni huduma ya kiroho ambayo ikisimama yenyewe haiwezi mpatia anachokitaka
Zaidi yeye ndio anatakiwa kutoa mahitaji
 
Asante sana
 
Duhh mkuu 5mil faida yake 250,000/=? Hapa risk zikitokea inakuwaje?

Labda sikaelewa vizuri , vyema ukanielewesha
Ikitokea imetokea na isipotokea ndio hivyo kila wiki laki tano, biashara ni kujitoa mhanga tu , unaweza ukafanya biashara ya faida kubwa na ukakata hata mtaji wenyewe.
 
Mkuu habari za majukumu. Nimeona thread ukiuliza ufanye biashara ipi kwa milioni 12. Mimi ningependa kukushauri ufungue chuo. Biashara ya chuo inalipa sana, hivi sass wanafunzi wanaohitimu shule za kata ni wengi Sana, na asilimia kubwa hawapati Nafasi ktk vyuo vya serikali na pia wazazi wengi hawapendi watoto wao waishie kidato cha NNE. Hivyo hii ni fursa kubwa Sana. Binafsi ninafanya kazi Kama afisa masoko katika chuo kimojawapo jijini arusha pia Nina uzoefu katika haya masuala. Kwa hiyo pesa uliyonayo inatosha kabisa kuanzisha chuo bila tatizo lolote. Endapo utapenda kufanya biashara hii tunaweza wasiliana 0717051576
 
Ikitokea imetokea na isipotokea ndio hivyo kila wiki laki tano, biashara ni kujitoa mhanga tu , unaweza ukafanya biashara ya faida kubwa na ukakata hata mtaji wenyewe.
Mkuu angalia namna ya kuongeza hiyo 250 kwa trip kama kwa trip hiyo 1 unatumia 5mil.

Maana yake trip moja ukipata hasara ya 1mil... itakuchukuwa trip nne kurudisha faida ..
Na hapo ni kama hizo transaction zote ziende sawa bila shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…