Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Mkuu angalia namna ya kuongeza hiyo 250 kwa trip kama kwa trip hiyo 1 unatumia 5mil.

Maana yake trip moja ukipata hasara ya 1mil... itakuchukuwa trip nne kurudisha faida ..
Na hapo ni kama hizo transaction zote ziende sawa bila shida
Sawa mkuu naupokea ushauri wako nitaufanyia kazi ,kwa maana ya kutafuta soko sehemu nyingine.
Wapo wanaopata faida ya 2M kwa mtaji huohuo wa 5M lakini ni baada ya miezi miwili au zaidi.sasa mimi nikaona nipate kiduchu tu Ila niwe na mzunguko mkubwa.
 
Sawa mkuu naupokea ushauri wako nitaufanyia kazi ,kwa maana ya kutafuta soko sehemu nyingine.
Wapo wanaopata faida ya 2M kwa mtaji huohuo wa 5M lakini ni baada ya miezi miwili au zaidi.sasa mimi nikaona nipate kiduchu tu Ila niwe na mzunguko mkubwa.
Ndio mkuu, jaribu kuangalia namna yakuongeza faida, kama kuna madalali kwa upande wa kununua au kuuza hapo kati au matumizi mengine ya uendeshaji wa biashara yako yasiyo ya lazima yapunguze..
Pamoja!!!!
 
Chukua tu million 8 chukua simu ndogo ndogo kwa ambazo sio smart phone,chukua na flash na memory then uwe unasambaza kwenye maduka ya kawaida utanishukuru sana.
"Maduka ya kawaida" ndio maduka gani sirajj john!? Ni maduka haya yaitwayo "ya mangi" au ni yale yanayouza simu hapo Msimbazi "round about" au maduka gani? Na hilo soko lenyewe la hivyo vifaa lipo?
 
Kopesha milioni 10 bot kwa mda wa miaka 20 au 25 inakua kama hazina yako ambapo kila mwaka wanakupa milioni 1 lakitano na kitu ukitaka kwa pamoja iyo 1.5 au kila baada ya miez 6 wanakupa laki 7 baada ya miaka 20 au 25 inakuja kucheza kwenye milioni 35+ na ile milioni 10 yako unapewa kama ilivo unakua kama umejitengenezea ki biashara chako mbadala au pesa za ada kwa watoto na kujikimu ki maisha incase main plan ikisumbua inatambulika kama treasure bonds (hatifunganii)
 
Salaam Alleykhum,

Wadau kwa kutumia uzoefu wenu, nishaurini nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa million 12 nilionao ili kila mwisho wa mwezi at least nipate Net profit ya milioni mbili.

Nipo tayari kufanya biashara ktk mkoa wowote Tanzania au hata kama ni importation business kama mtaji unatosha nipo tayari.

Nipeni ushauri ili nami nitoboe.
Njoo tusafirishe Mkaa kwenda Dsm na maeneo mengine
 
Salaam Alleykhum,

Wadau kwa kutumia uzoefu wenu, nishaurini nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa million 12 nilionao ili kila mwisho wa mwezi at least nipate Net profit ya milioni mbili.

Nipo tayari kufanya biashara ktk mkoa wowote Tanzania au hata kama ni importation business kama mtaji unatosha nipo tayari.

Nipeni ushauri ili nami nitoboe.
Kama kweli hii pesa unayo ukipewa mchongo wa kuingiza 10M ndani ya wiki mbili ama mwezi, utakubali kutoa 40% ya Faida utakayopata?
 
Kama mimi ningekuw ndiyo nin hizo hela kwa muda huu
Ningefany tafiti fast ya hawa wanaouza spea za simu,afu nikishajua namna ya kuiendesha hiyo biashara basi ningefungua ofic kweny uhitaji kwa sababu
Vifaa vya simu ni bei ndogo afu vinahitajik kila wakati mf mic,chaji system,vioo,betr,camera,nk
Hivo unawauzia mafund kwa bei ya jumla
Kwa siku unaingiza pesa nying nzuri bcs hata uhitaji ni mkubwa kibongo bongo weng wanatumia simu za kichina hazidumu
 
Kaka km una kwako au kwenu eneo kubwa tuu, anza kufuga kuku wa layers kuku wale wa mayai, niamini utapiga zaidi ya hiyo milion 2 kwa mwezi ila yakupasa tu uvumilie ndan ya miez mitano hutovuna kitu ila baada ya hapo adi miaka 3 ijayo ww unavuna mamilioni.

1. Toa 2,500,000 nunua vifaranga 1000
2.Toa mil 2 uje ufungiwe cage ya kuingiza kuku 1000
3.Gharama za chanjo za siku 28 kwa vifaranga.
4.Vyakula vya kuku kuanzia starter Mash na kuendelea. Mfuko wa kilo 50 @49000 ila hapa wakishafikisha wiki tatu unaweza kuwachanganyia pumba+layers premix+layers mash
5. Vyombo vya chakula na maji.
6. Chumba maalum cha joto kwa vifaranga kwa miez 2

Yani inshort utatumia milion 7 tu mpaka kuku wanafika miezi 5 kuanza kutaga, na wakianza kutaga it means una uhakika wa kukusanya mayai 1000 kila siku iendayo kwa Mungu na hapo kuna kuku wengine wakishiba vizur wanaweza kukuangushia mayai 2 kwa siku.

Sasa chukua unakusanya mayai 1000 tu kwa siku, haya mayai 1000 ni sawa na trey 33 na mayai 10.

Trey kwa sasa ni sh 8000
Kwahiyo kwa siku 33x8000=264,000

Kwa mwezi sasa 264,000x30=7,920,000.

NB: Kwahiyo ukiwatunza vizur vifaranga kwenye chanjo, chakula braza wewe ni milionea unapiga zako Milion 7,920,000/= kwa mwezi kama faida haina tax hyo wala VAT. Na ukumbuke kuwa hawa kuku watakuwa wana uwezo wa kukutagia ndani ya miaka 3 wakichoka unawatoa unawauza nako unapiga hela kuku 1 sokoni 8000. 8000x1000= 8000,000/= baada ya miaka 3 utavuna Mil 8 km pesa yakuwauza nyama hapo umekosa nn kaka!!.


Yan ungejua mm nina shida ya milion 2 tu nitanue nitoke hapa kwny kuku 55 ambapo kwa mwez wanaingiza 440K tu.
12 M haitoshi kutunza layers 1000
Itakata njiani, ufugaji umekua GHARAMA sana kwa sasa, labda aanze na layers 700 na aachane kwanza na mambo ya cages.pia awe na mabanda tayari nje ya hiyo 12M
Na kwa kiasi kikubwa yeye mwenyewe awe nguvu kazi.
Lakini ni biashara ambayo akifuata masharti ya ufugaji, kuzingatia huduma za chakula bora, maji safi na usafi hatapoteza pesa,
Itaanza kurudi baada ya miezi 7, na kwa mwaka wa pili atatengeneza faida.
Pili ukitaka kupotea katika ufugaji wa kuku wa kisasa ni uanze kuchanganya chakula kienyeji,
Layers kwa wiki ya tatu bado wapo kwenye starter, wiki ya 6 Ndiyo wanaanza kuchanganyiwa starter na growers mash, wiki ya 8 ndiyo wanaingia kwenye grower moja kwa moja na hiki chakula hua ni punje ndogo ndogo siyo pumba!
Anyways
Kwa ufupi ufugaji unalipa haswa kwa kuku wa mayai, lakini siyo kirahisi hivyo ulivyoandika, pia ni long-term businesse, faida ataanza kupata mwaka wa pili wa ufugaji.
 
Mkuu habari za majukumu. Nimeona thread ukiuliza ufanye biashara ipi kwa milioni 12. Mimi ningependa kukushauri ufungue chuo. Biashara ya chuo inalipa sana, hivi sass wanafunzi wanaohitimu shule za kata ni wengi Sana, na asilimia kubwa hawapati Nafasi ktk vyuo vya serikali na pia wazazi wengi hawapendi watoto wao waishie kidato cha NNE. Hivyo hii ni fursa kubwa Sana. Binafsi ninafanya kazi Kama afisa masoko katika chuo kimojawapo jijini arusha pia Nina uzoefu katika haya masuala. Kwa hiyo pesa uliyonayo inatosha kabisa kuanzisha chuo bila tatizo lolote. Endapo utapenda kufanya biashara hii tunaweza wasiliana 0717051576
Mbona miujiza ml12 ufungulie chuo rabda madrasa !!!
 
Mbona miujiza ml12 ufungulie chuo rabda madrasa !!!
Imagination never work, endelea kukaa hapo watu wanatajirika....kila kitu uki complicate hakiwezekani na pia unapaswa kujua juhudi zako ndio mafanikio yako... lazy people always do challenges not focusing
 
Back
Top Bottom