Biashara mpya kwa mtaji huo mkubwa is too much risk kama hautasimamia mwenyewe mkuu
Ila kuna option ya kununua mazao ya chakula hasa Mpunga gunia zako za kutosha na kuziweka store na inapofika kipindi cha Masika unafanya kuzikoboa gunia zako na kupata mchele wako swafi tayari kwa kuingiza sokoni kwani kipindi hicho uhitaji wa mchele unakuwa mkubwa sana hapa Dar es Salaam na Zanzibar
Minimum profit calculation
Katika centre nyingi ninazo zifahamu kwa muda huu gunia moja la Mpunga lina range kwenye TSH. 50,000/=
Hivyo basi kwa Pesa uliyonayo yaani TSH. 12,000,000, utaweza kupata gunia zenye debe sita sita 240 za mpunga na kuzihifadhi.
Kipindi ambacho Masika imechanganya hasa mwezi wa kwanza au wa pili, wewe ndo unafanya kukoboa mpunga wako ili upate mchele na gunia 1 la mpunga la debe sita linatoa debe tatu za mchele na debe moja la chenga za mchele
Hivyo basi katika zile gunia 240 unazidisha mara 3 na utapata debe 720 za mchele clear na debe 240 za chenga za mchele
Ukija sokoni debe moja la mchele lina range kwenye 35,000/= kwahyo unazidisha mara debe zako 720 za mchele na utapata kiasi cha TSH. 25,200,000/=, pia debe moja la chenga za mchele ina range kwenye TSH 10,000/= ukizidisha na debe 240 utapata kiasi cha 2,400,000/=
Total itakuwa ni Tsh. 27,600,000/= na ukitoa mtaji wako wa 12,000,000/= utapata net profit ya TSH. 15,600,000/= katika kipindi cha miezi mitano cha kuhifadhi mpunga wako
Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu.
Centre zenye mpunga mzuri ni kama zifuatazo Kyela, Kamsamba na kilyatundu, Usangu, Kahama ila kwa Morogoro sizifahamu vizuri
Naomba kuwasilisha na ninakaribisha maswali