Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Dagger-V nashukuru kwa ushauri mzuri.
Kwa kuheshimu mawazo ya wengine, naomba niseme kwamba ninapitia kila ushauri uliopo hapa then nauchambua na nikikwama napiga simu kwa waliotoa ushauri ili ku-share uzoefu.
Pia niwashukuru wote ambao wamekuja mpaka inbox kunishauri, nawathamini sana.
Wadau, naendelea kupokea ushauri, nafurahi sana mnapotoa mawazo yenu, Mbarikiwe sana.
 
Mkuu hii kitu waweza anza na minimum capital ya sh ngapi?
 
Mkuu vipi unaweza recommend wapi kwa Kahama hasa mtu anaweza kupata huo mpunga? Kuna mtu ananisumbua Sana anahitaji mchele Kla
 
Mkuu, mrejesho wa faida hapa huonekana baada ya muda gani??
Inategemea unaifanyaje. Kwa mfano hiyo ya nguruwe unanunua wa miezi miwili wa kisasa unapiga msosi mzuri ambapo chakula chake ni wanga mwingi na madini ni bei rahisi kuliko cha protini ambacho wanahitaji wakiwa wadogo. baada ya miezi miwili au mmoja kwa formula maalumu unauza au uanchinja. Lets say umemnunua 150,000/= ukimtunza akazidi 100 kg unauza 380,000/= ukichinja ukauza lets say kilo ni 7,000 x 80 = 560,000/=

Au ukanunua mbegu ya kisasa wakubwa ambao hawatunzwi vizuri, choma vitamin, choma iron piga msosi vizuri, mwezi unamuweka sokoni.

Inategemea umekuja na plan gani.
 
Inaweza kuwa kweli lakini nadhani ushindani ni mwingi sana kwani naona Ilala yote imejaa spare hizo chini ya Wapemba ambao najua wanazipata kwa bei nafuu au "bure" au kwa msaada kutoka kwa ndugu zao huko Uarabuni na hivyo kuziuza kwa bei che! Labda uangalie chimbo jingine nje ya Dar!
 
Kwa mkoani nadhani patafaa zaidi
 
Kwa mkoani nadhani patafaa zaidi
Hasa mikoa yenye uchumi unaokua kwa kasi na yenye shughuli nyingi za kibiashara; hapa nafikiria hata mikoa ya pembezoni mwa nchi kama Mara au Kagera au Songwe na mingine ya aina hiyo au hata Kibaha kwenye mpishano wa magari mengi. Sijui nawaza kimya kimya tu!
 
Upo sawa
 
Kama ungekua na walau 20M
Ningekushauri nenda mgodini kahama/geita au Tarime
[emoji117]Nunua crusher machine(karasha) 7M
[emoji117]kodi eneo bei 60k per month(though inategemea na makubaliano yenu)
[emoji117]ingia share/agreement na wamiliki wa duara nzuri
[emoji117]nunua mawe usage na kuosha
In the next two or three months unaenda leaching plant kwa ajili ya kuozesha trust me faida utaipata nzuri tu kama ulipata mtu mzuri wa kusort mawe kwenye duara
 

kwahiyo Mkuu hiyo 12M mgodi haitoshi mbona nasikia kuna kalasha used mpaka 4M
 
Nisipotoa maoni yangu. Ntakua najinyima na nakunyima kitu mkuu. Kwanza i was interested kuona hiyo m12. Pili i was getting more interested kadri nilivyosoma thread, ni hivi;

1. Kuna jamaa hapa kakukazia sana swala la spear used. Miminaongezea hapa both used and new. Aisee kama alivyokaza, hii biashara inalipa haswaaa. Nunua mzigo weka hata chumbani kwako utaisha tu. Market your products. Hyo return ya 2m mbona ndogo sana. Used dubai,new china. Agiza usiogope. Fanya research then ona utafanya nini bora. Kama unavyoona magari yanavyonunuliwa, ndivyo hivyo spare. Zinanunuliwa kwa wingi. In a year utapiga hata milioni 500. Ukitulia na kukazana. Hii sio mahesabu ya kusema tu. Nakwambia from experience.

2. Ukishindwa vyote chukua frame kkoo, agiza mzigo wa nguo weka iwe jeans, tshirts, tights au hata chupi. Zinalipaaaaa saaaaaaana.
agiza mzigo wako china njoo uuze kkoo. Hata milioni 20 utapiga kwa siku. Faida hapo sichini ya milioni 2 kwa siku. Kkoo ni rahisi kwa nguo. Congo tower, aggrey nk.

boss.. biashara ni kupambana na uvumilivu. Hizo kazi zote zinahitaji uvumilivu na uthubutu. Ukileta mzigo week umeisha.
 
Hii thread imenipa unasiri sana mkuu. Kwa sababu unauzoefu kwenye hayo maeneo drop your contacts bro ili nikutafute unipe madini zaidi
 
Hii thread imenipa unasiri sana mkuu. Kwa sababu unauzoefu kwenye hayo maeneo drop your contacts bro ili nikutafute unipe madini zaidi
Ni watu wachache sana tunapenda kufahamika au kufahamiana humu JF ndio maana ya hayo majina ya bandia, hivyo kazana tu kuhojiana humu JF hadi kieleweke. Suala la kutoa contacts litakuja baadaye. Uliza maswali yako humu humu kweupe! Na majibu utapata bila shaka yoyote.
 
nunua Toyota IST 2 kwa million 12 kila moja jumla 24.

weka uber au mpe mkataba mtu kwa miaka 3 awe analeta hela .

hela unaiona chapu
 
Deal Done mkulungwa
 
biaahara ya kuhifadhi mavuno haina presha sana sawa but haina faida sana pia hawezi pata mil 2 kwa mwez
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…