kamjabari
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 1,144
- 1,668
Wakati mwingine hata hao usalama taifa wanatimba kwenye rushwa ndiyo maana nchi inataabika kupata maendeleo haraka kama inavyo tarajiwa.Huu ndiyo huo ubinafsi wa kipumbavu nilioutaja.
Mkandarasi anapata faida ya moja kwa moja kifedha katika mradi huo.
Hivyo anatakiwa afanye kwa ufanisi ili apewe miradi mingine faida ziongezeke.
Miradi ikikamilika kama ilivyokusudiwa ni faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Hivyo hao makandarasi wanaogawana pesa na viongozi ni maadui wa taifa na kazi za usalama wa taifa ni pamoja na kuwashughulikia watu hawa.
Hata hivyo, kama watagawana faida halali siyo shida kubwa ikiwa miradi itakamilika kwa ubora uliokisudiwa na hawakuiba pesa ya uma.
Kama usalama wangeweza kudill na wahuni wote wanaoisababishia nchi yetu hasara tungekuwa mbali sana.
Katiba mpya nimuhimu sana itakayo weka mufumo mzuri wa taasisi zote kusimamiana kwa masilahi ya nchi.
Kuliko sasa watu wanateuliwa na mtu mmoja na akifanya kosa haguswi