Nigeria ilianza kuchimba mafuta 1956, bado inauza mafuta ghafi nje na kununua yaliyosafishwa. Tanzania tutatoboa na gesi?

Nigeria ilianza kuchimba mafuta 1956, bado inauza mafuta ghafi nje na kununua yaliyosafishwa. Tanzania tutatoboa na gesi?

Huu ndiyo huo ubinafsi wa kipumbavu nilioutaja.
Mkandarasi anapata faida ya moja kwa moja kifedha katika mradi huo.
Hivyo anatakiwa afanye kwa ufanisi ili apewe miradi mingine faida ziongezeke.
Miradi ikikamilika kama ilivyokusudiwa ni faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Hivyo hao makandarasi wanaogawana pesa na viongozi ni maadui wa taifa na kazi za usalama wa taifa ni pamoja na kuwashughulikia watu hawa.
Hata hivyo, kama watagawana faida halali siyo shida kubwa ikiwa miradi itakamilika kwa ubora uliokisudiwa na hawakuiba pesa ya uma.
Wakati mwingine hata hao usalama taifa wanatimba kwenye rushwa ndiyo maana nchi inataabika kupata maendeleo haraka kama inavyo tarajiwa.

Kama usalama wangeweza kudill na wahuni wote wanaoisababishia nchi yetu hasara tungekuwa mbali sana.

Katiba mpya nimuhimu sana itakayo weka mufumo mzuri wa taasisi zote kusimamiana kwa masilahi ya nchi.

Kuliko sasa watu wanateuliwa na mtu mmoja na akifanya kosa haguswi
 
Hivii TIPER Refinery yetu kule Kigamboni bado kipo? Mbona bado tunaagiza mafuta kutoka nje, kulikoni?
 
Nchi zilizojaa rushwa haziwezi piga hatua yoyote ya maendeleo. Sababu zitakuwa kulalamika kuhusu wazungu kwamba wanakwamisha maendeleo kumbe ukweli ni kwamba hatuna akili ya kujitawala.
Wachina wananyonga Hawa mafisadi ambao ccm inawalea Kwa kuwa wote wameoza na kunuka rushwa
 
Nadhani umeongea vizuri sana, kuna external forces huwezi kuzikwepa kwenye uchumi wa dunia.
Sasa si jamaa wanatupenda mno na kutupatia msaada hapa inakuwaje wasitupe msaada tukajitegemea kwa hili wenyewe tukaanza kuwauzia.
 
Asante kwa pongezi ndugu meneja,
Nakumbuka Tanzania ina mkataba wa Tangu 2022 na wawekezaji kuibadili gesi asilia kuwa CNG wenye thamani ya zaidi ya trilioni 70.


Kuhusu kutandaza mabomba, changamoto watakayokutana nayo ni mipango miji, haitaweza kufika maeneo mengi ndio maana mpaka sasa imeweza kufika Oysterbay na maeneo machache kama hayo.
Mkuu asante sana kwa bandiko lako.

Mkuu gesi inayozungumziwa kwenye huo mkataba sio CNG bali ni LNG. CNG ni gesi asilia iliyoshindiliwa. LNG ni gesi asili iliyokatika kimiminika.

Lengo la kuibadilisha gesi asilia kuwa katika kimiminika ni kurahisisha usafirishaji. Ni rahisi zaidi kiuchumi kuisafirisha gesi asilia kwenda katika masoko ya mbali hasa huko ulaya ikiwa katika hali ya kimiminika kuliko ikiwa katika hali ya gesi.

Lakini ikisha kufika mahali inapopelekwa kuuzwa itatakiwa ibadilishwe tena na kuwa katika hali ya gesi ili iweze kuingizwa katika bomba ili iweze kutumika kupikia majumbani.

Naomba kukazia tena ili gesi asilia iweze kutumika majumbani inatakiwa kuwa katika bomba (PNG). PNG ni piped natural gas.
 
Mkuu Replica , una hoja ya msingi ila hujaiweka vizuri. Nchi za kiarabu zimetumia mafuta kujenga uchumi wake sasa baadhi ya nchi hizo hazitegemei tena mafuta. Nigeria na Angola zina mafuta lakini mafuta hayo hayajaweza kujenga nchi hizo. Tanzania sasa ina gesi, jee LNJ itaisaidia Tanzania kujenga uchumi imara?.

Jibu.
Uchumi wa dunia japo unatawaliwa na nguvu soko, marked forces, nchi mabeberu ndio wana influence hizo market forces.

Mfano Africa, South Africa, Angola, Ghana, Tanzania, tunachimba sana dhahabu, lakini bara la Africa lote hatuna gold smelter hata moja, wakati nchi ya Uswiss haina hata pune moja ya dhahabu ina gold smelters 6!. Mabeberu wamefanya hivyo ili gold inayochimbwa Afrika ipelekwe huko.

The same applies to crude oil, Africa tuna mafuta hata Uganda, mafuta inayoyachimba, japo yanatosha kuifanya Uganda ijitegemee isiagize mafuta, Manmade market forces ziko designed in such a way Uganda haiwezi kujenga oil refinery yake, ikasafisha mafuta yake, lazima yapelekwe kwa nchi mabeberu kusafishwa ili Uganda iendelee kununua mafuta.

Hata Tanzania, tutayapokea mafuta ya Uganda pale Chongoleani na kuyasafirisha yote, badala ya kujenga refinery, ili tuendelee kuagiza mafuta.

The same applies to LNG gas yote ni for export, huku tukiendelea kuagiza LPG kwa matumizi ya majumbani!.

Huo ndio uchumi wa dunia.
P
Ni udumavu wa akili wa watawala wa kiAfrica ,kwani mbona Dangote kajenga refinery , wewe unafikiri wazungu watakuja wakujebfde refinery ya malighafi zako ?
Ni wajibu wetu serikali itengeneze sera nzuri na kuencorage wazawa matajiri hata kuungana na kuanzisha refineries za malighafi zetu na kuacha utegemezi wa nje .
Watawala wa Afrika wanawaza kutawala milele na kuiba mali za uma basi
 
Back
Top Bottom